The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Pascal Mayalla sikulaumu kwa kuandika haya, nikuulize swali ulikuwa wakala? umeongea na mawakala wa pande zote mbili? kama ndio uliongea na wangapi wa zanzibar na bara, uchaguzi wa tar 27 zanzibar uliushuhudia?. Ukiwa na jibu basi utatupa majibu
 
Ni kweli hao ni waongo! Uchaguzi ulikua huru na wa haki.
Mabox kujwaza pre-ticked ballots ni kawaida kwa Africa.
Halafu hawa New York Times siwapendi! Kwa mwezi wananipaga articles mbili tu za bure halafu wananipiga pini! Bora Washington Post na New Yorker wana ubinadamu, hoehae huwa tunapata articles kadhaa.
Gazeti la kufungia maandazi hilo.
 
Hao unaowaona waongo ndo ma-genius wa kuandika habari duniani mkuu! Wewe habari zako hufiki hata robo ya Kabendera, ndo maana uliona vema kumchongea. Habari za hao New York Times zinasomwa dunia nzima.

Wewe zinasomwa Jf, tena watu hata hawamalizi kusoma maana hazina mashiko, umekuwa bias na mwenye njaa ya uteuzi mno mno. Sometimes najiuliza, wakati unaandika unakuwaga conscious au unconscious mkuu??
 
Mayalla, siku zote ukweli unabaki kuwa ukweli. Kwa mtazamo wako ww uchaguzi huu ulikuwa wa huru na haki ?. Kama ulikuwa huru na haki kwanini mapolisi wajazwe vituoni na silaa za kizita ?. Uchaguzi ni mchakato unaanzia katika daftari la wapiga kura, uandikishaji ,upigaji kura , kuhesabu hadi matokeo. SWALI MBONA HATUONI WINGI WA POLISI WAKATI WA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KULA ?. KWANINI TUME IMETUNGA SHERIA INAYEMUNYIMA MPIGA KURA KUSUBIRI MATOKEO ?. Kwenye mikutano ya kampeni unaruhusiwa , kupiga kura sawa hofu yanini kwenye kwenye kusubili matokeo. Naomba unipe orodha wa wagombea wa CCM walioenguliwa, ama kukamatwa na kupigwa na polisi. Hivi OCD ANAPOKUWA NA NGUVU HADI KUMWAMBIA MGOMBEA KUWA, SHUKA JUKWAA NA HATA UFANYEJE HUWEZI KUSHINDA HICHO KIBURI KATOA WAPI ?. Nadhani ndugu yangu Mayalla unapiga debe upate uteuzi, lakini kumbuka AMBAPO HAIPO HAKI, HOFU UTAMALAKI.
 
Umeshinwa ku thibitisha kama gazeti hilo limeandika uongo .inaonyesha wewe ndo muongo
 
Nakushauri kanusha kinafiki kama ulivyozoea lakini ukweli unaujua!
 
Hayo maneno ya magazeti hayatusaidii chochote, sisi tunachohitaji ni vikwazo tu ili tuumie tu sawa lakini dikteta akose kiki na pa kusemea uongo wake kuwa wapinzani wanazuia maendeleo.
 
Uongo ni mrefu na ukweli ni mfupi.Kwahiyo kama unajua wameandika uongo hebu tuletee huo ukweli usio acha shaka tuone kama haitakuchukua nusu dakika kuaibika.
 
@pascalmayalla nikuombe ufanye kazi moja kama hujawahi kuwa wakala kwenye uchaguzi basi ongea na mawakala wasio pungua 10 wa Wilaya tofauti uchanganye wa vyama 3 CCM, CHADEMA na ACT halafu urudi hapa u comment kilichoandikwa kwenye gazeti la Marekani, kama huwezi kuwahoji maawkala ukapata maoni yao wote basi futa uzi wako.
 
Cha kushangaza, hata Paskali anakupa Hi! kwa hayo uliyoandika kumuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…