The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

.....Na mwisho, mmesahau kitu kimoja tu (mazingaombwe ya mtu mweusi) -CCM wana imani sana za kichawi.....mkiwa tishio lao kubwa mtaondoka wengiii?

Mkandara vipi tena na mambo ya kipapai? How come you believe that much?
 
Invic
CCM kwa madaraka wako tayari kufanay lolote as long as wan retain madaraka sasa sishangai leo mambo ya Vipapai
 
Na James Marenga


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema Rais Jakaya Kikwete, amelemewa na kazi na hataweza kuwaletea mabadiliko Watanzania wanayoyatarajia.


Mbowe alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, alioufanya nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, kuzungumzia tathmini ya ziara yake, ya kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura aliyoifanya kwenye mikoa kadhaa hapa nchini.


Alisema Tanzania ni nchi kubwa, ambayo haiwezi kuongozwa kutoka eneo moja tu la nchi kama inavyofanywa sasa na serikali ya Rais Kikwete.


“Rais Kikwete na Waziri Mkuu wake wamekuwa wakihaha, wanatoka Ulaya wanazunguka mikoani, nchi hii ni kubwa hawawezi kuzunguka na kutoa maagizo yatakayoweza kurekebisha uchumi wa nchi hii peke yao,” alisema Mbowe.


Alisema kuendelea kutoa maelekezo ya kuendeleza nchi kutokea Dar es Salaam, kutaendelea kuifanya mikoa kuwa maskini kutokana na ukweli kuwa haitumii vyema rasilimali zilizopo kwenye mikoa hiyo kwa maendeleo yake.


Alisema hivi sasa ni jambo la kusononesha kuona kwamba, mikoa na wilaya hapa nchini imekuwa ikigawanywa katika misingi ya kikabila badala ya kikanda na akasisitiza njia ya pekee ya kuepukana na hilo ni kuanzishwa kwa serikali za majimbo, ambazo chama chake kimekuwa kikipigia kampeni.


Alieleza kushangazwa na hoja zilizokuwa zikitolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni mwaka jana ambazo zilikuwa zikidai kuwa, sera ya majimbo itakuza ukabila wakati ukweli ni kwamba mfumo wa sasa wa mikoa na wilaya ndiyo hasa unaokuza ukabila.


Alisema katika baadhi ya wilaya alizopita wananchi kadhaa aliozungumza nao walionyesha kutowajua wakuu wao wa mikoa na wilaya kutokana na ukweli kwamba watu hao hupata nafasi hizo za kuteuliwa badala ya kuchaguliwa kama itakavyokuwa iwapo majimbo yataanzishwa.


“Hivi sasa rais anaweza akateua mtu kuwa mkuu wa mkoa au wilaya kwa sababu ni rafiki yake wa…au ni ndugu yake…Nimepita mahali watu hawamjui mkuu wao wa mkoa wala wa wilaya, kwa sababu watu hao hawakuwachagua,” alisema Mbowe.


Akiendelea na mifano alisema kuna sehemu Rais Benjamin Mkapa katika kipindi chake chote cha miaka 10 ya urais wake alifika mara moja tu, jambo ambalo ni ushahidi mwingine unaoonyesha kuwa nchi ni kubwa, ambayo kamwe haiwezi kuongozwa kutoka Dar es Salaam.


“Nchi kubwa kama hii, Waziri wa Elimu ndiye anaongoza sekta nyeti kama hiyo. Maamuzi ya elimu kwa nchi yote hii yanatoka Dar es Salaam. Hatuwezi kutegemea mabadiliko ya kweli kwenye sekta hiyo muhimu,” alisema Mbowe.


Akirejea sera ya chama hicho ya kugawa nchi kwenye majimbo kwa kuwa na kanda za kiutawala alisema, mikoa mingi imekuwa nyuma kimaendeleo kwa kukosa utaratibu wa kiutawala wa kuamua mipango yao ya kimaendeleo.


“CHADEMA tulikuwa tukisisitaza kuundwa kwa kanda, kwa mfano Kanda ya Ziwa ingekuwa na mikoa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga na Mara, kanda hii ingekuwa na uwezo wa kupanga mipango yake hasa matumizi ya rasilimali zilizopo na kujiletea maendeleo.


“Pato la mikoa ya Kanda ya Ziwa, hasa linalotokana na dhahabu pekee, ni asilimia 42 ya mapato ya nchi, kama mikoa hii ingekuwa na mikakati mizuri, ingeweza kujitosheleza na wananchi wake wasingalikuwa maskini,” alisema.


Mwenyekiti huyo alipinga hoja iliyojengwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kuigawa nchi kwenye kanda ni kuendeleza ukabila, kwa kusema mikoa hiyo imeundwa na makabila tofauti ambayo si rahisi kujenga ukabila.


Alisema sera hiyo pia ina lengo la kuhakikisha kuwa viongozi kwenye ngazi za mikoa wanatokana na ridhaa ya wananchi, na si uongozi wa kupeana kama inavyofanya serikali ya sasa.


Akizungumzia mkakati wa chama hicho kwa mwaka 2007, alisema kuanzia mwaka huu, chama hicho kinaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi kwenye ngazi mbalimbali ili kupata viongozi wapya watakaosimamia mikakati ya chama hicho.


Alisema utaratibu utakaotumiwa na chama hicho si kama ule wa CCM wa kuwa na uchaguzi mmoja, watakachofanya ni kuwa na uchaguzi ambao utatoa nafasi kwa wanachama wote, kwa wakati unaofaa kugombea nafasi hiyo.


“Mkutano mkuu ulibadilisha baadhi ya vipengele vya katiba, hata mimi nitamaliza muda wangu mwaka huu badala ya 2009, na anaweza kuchaguliwa mwenyekiti mwingine, chama chetu kina demokrasia,” alisema Mbowe.


Mwenyekiti huyo alisema chama hicho kimeandaa mpango mkakati wa miaka mitano na kumi, ambayo inalenga kuimarisha chama hicho katika ngazi zote kuanzia matawi hadi taifa.


“Tukimaliza ziara ya kuwashukuru wananchi, ziara ambayo tumeipa jina la ‘tumaini jipya’, tutahamia kwenye ziara ya ardhini, viongozi watakwenda wilaya kwa wilaya, mkoa kwa mkoa kukitangaza chama na kufungua matawi, kutoa semina na kueleza mkakati wa chama,” alisema.


Ziara hiyo alisema itawahusisha wabunge, madiwani wa chama hicho na watendaji wengine na watatumia makabrasha mbalimbali yaliyoandaliwa na chama hicho kwa ajili ya kuelezea mikakati mbalimbali ya chama hicho.

(Tanzania Daima 6/1/2007)
 
Hasara umefungua thread mpya nafikiri tulikubaliana tusifungue thread bila uchunguzi? Lakini ni vizuri kuunganisha na ya Mbowe niliibiwa kura ndio kisa nilifanya hivyo. Mtu akitaka kuchangia afuate hii link;

http://jamboforums.jamboo.co.tz/showthread.php?t=1201&page=7

Kwa wasio fahamu Habari Leo ni gazeti la Kiswahili lililoanza hivi karibuni.

Thank you.
 
Invincible,
Ndugu yangu mimi mwafrika kwanza!...hata niende wapi nitaendelea kuamini kuwepo kwa Voodoo. Hii inaweza kuwa thread nyingine!
I have seen things beyond my imagination and belief!...
Hiyo science na elimu dunia inapinga maswala haya lakini hiyohiyo Sayansi imeshindwa sehemu nyingi sana za maradhi ya ndugu zetu!.. watu hawa wamerudishwa makwao na wamekuja pona kupitia kwa waganga wa kienyeji ama wahubiri wa dini!..
Binafsi naamini unaweza kwenda kanisani na kumwomba Yesu (Mungu) akupe nguvu na uwezo wa kushinda uchaguzi fulani against me.... na Mungu akakusikia ombi lako!....Nimekwishaaa, unless nami nifanye mapambano sawa. Nyamuhanga wangu anaweza kushindwa kunisaidia kwa sababu sikutimiza masharti!
Msuya yalimkuta na hakuna kati yenu anayefahamu sababu ya mtu kama msuya kuwa nje ya siasa!
Mwanakijiji,
Sasa mkuu unaanza kuchemsha!... hao Chadema wanakufuata wewe na kukuahidi vyeo!...Vyeo gani walivyonavyo Kitaifa kama sio kuungana nao ktk kuijenga Chadema. Tena wapo wazi kila siku humu kutuomba kujiunga nao!...
Jamani tusiwe tunachanganya vitu hapa kwani ukipata cheo Chadema ni ktk kuisaidia Chadema tofauti kabisa na yule anayeahidiwa cheo na CCM Ki- Taifa. Yaleyale ya Asha Rose Migiro! Kuchaguliwa kwake UN hatuwezi kusimama hapa na kudai eti Marekani wamemfuata Asha Rose na kumuahidi cheo kwa maslahi ya TZ..beside all, Mzee Mwanakijiji kufuatwa kwako hakuwezi kuibomoa CCM hata kidogo bali kufuatwa kwa Freeman, Zitto na Mnyika kuna uzito tofauti kabisa kwa Chadema.
Come on Mwanakijiji, nilikuwa nakuamini kwa vimbwanga sasa vipi mbona unapoteza mwelekeo?
 


Kwa wasio fahamu Habari Leo ni gazeti la Kiswahili lililoanza hivi karibuni.

Thank you.


Sema ukweli zaidi kwamba ni gazeti la serikali lililoanzishwa kwa ajili ya propaganda za JK na Lowassa. LInapata ruzuku ya serikali (kodi yetu) na bado linashindanishwa na magazeti binafsi chini ya wizara ile ile inayoongozwa na serikali ile ile...huku pia likipatiwa matangazo ya serikali kwa upendeleo. Katika zama hizi, za soko huria, na serikali kujitoa katika biashara, kuna haja gani ya serikali kufanya biashara ya magazeti? Wanaharakati read between the lines!
 
Mzee Mwanakijiji ni mzee wa hoja nzito. Tatizo ni pale anapozidiwa, huwa jazba zinamjaa na ndipo hapo tena identity yake inapopotea. Katika hili la chadema ni wazi kabisa maji yapo shingoni. Ila tunaendelea kuheshimu umahiri wake wa kujenga hoja. Namini atajua tu siku moja kuwa CCM sio mahala pake, na wakisema CCM ina wenyewe, kwa jinsi nilivyompima kupitia hii forum, yeye sio miongoni mwao. Huwezi ukawa na upeo kama wa Mwanakijiji halafu ukaniambia wewe ni mwana CCM wa kweli. Yaani sioni kabisa connection kati yake na CCM.
 
Umenena mwanasiasa. Mpe somo mwanakijiji; waweza kumtoa kijijini, akaona taa!
 
Kichwamaji

Mie nipo out of Bongo hii habari nimeipata through the net, na hapo juu aliyeweka Hasara ameweka kama ni story yangu - its not mine sasa ukweli upi ambao unataka niseme. don't be a fool?

Follow the link
 
Kichwamaji

Mie nipo out of Bongo hii habari nimeipata through the net, na hapo juu aliyeweka Hasara ameweka kama ni story yangu - its not mine sasa ukweli upi ambao unataka niseme. don't be a fool?

Follow the link

Ndo hivyo sasa, I am not being a fool by giving you details on who owns Habari Leo. Nakoleza ujumbe wako, ili wadau waupate mzima mzima. JK hajaridhika na waandishi aliowanunua na makampuni ambayo yeye na swaiba zake wamenunua hisa. Bado anaanzisha gazeti jingine, kwa kodi zetu, ili liandike sifa zake. Kama linaweza mbona haliandiki uozo wa serikalini kama njia ya kuwasaidia kujirekebisha?
 
MwanaKJJ wewe ufuatwe na Chadema ? Basi nao watakuwa wagonjwa maana wanakuona haya akili yako ni kijani kama bendera la CCM lakini maajabu unaongelea USA na si Tanzania . Maana hata sijui wakufuate kwa huu msimamo wako ? Wewe unajua siasa za kubabatiza kwenye Radio yako na kukemea tabia ambayo iko kwa Lowasa . Unajua watu hawa kuelezi ukweli wanakuangalia kila unapo chemka. Chadema kukuomba wewe uwe nao wanataka kuji hatarishia kuongeza watu wenye hadithi kama akina Tambwe and the likes kwamba CCM ni better than upinzani .

Haya wacha waje kukunujua hao Chadema . Uongo mwingine bwana
 
Hapo nimekupata maana nilifikiri unanilaumu kwa kupotosha ukweli mimi sikujua kama ni gazeti la CCM au la Serikali.
 
Huu ushindi wa 80% najiuliza ni wa kweli ama ? HabariLeo ina replace Uhuru ambalo halina wasomaji .JK katika hotuba yake moja alitaja moja ya mafanikio makubwa ni kuanzishwa gazeti lao la uongo .Sasa najiuliza hilo gazeti linamsaidiaje Baba yangu hapa Namtumbo . Kazi kubwa .
 
sasa, hivi kweli mtu mwenye mawazo kama ya Mbowe atatafutwa ajiunge na CCM?!!

We unadhani wanamtafuta kumfanyaje? Wanajua mawazo yake ni mapevu mno kwao. Hawatayatumia. Lakini wanataka wamwondoe huko anakotemea cheche! Ndiyo nia yao.

Mwanakijiji usiwe na jaziba wanaokukosoa wanakupenda. Sasa ukimwaga upupu, ukazungumza kama mtu wa mwaka 1921 vijana wa karne ya 21 wakuache, eti tu kwa kuwa kauli zako za kijani? Hata ungekuwa shushushu. Hayo watu waliyaogopa zamani; si sasa. Kama we muungwana, basi, pokea ushauri unaopewa...using'ake!
 
Hili jamvi bwana usije kujua sana kuna wengi hapa yako ondoka wache tuje kukusifu . Kazi kubwa utatembea uchi ukicheza maana utachokonolewa na utachokonoka heheh
 
sasa, hivi kweli mtu mwenye mawazo kama ya Mbowe atatafutwa ajiunge na CCM?!!

Sasa kama walimfuata Kabourou, Tambwe Hiza, na wengine kibao ambao hata majina yao sio makubwa, unaona ajabu gani wakimfuata Mbowe. Yote hii inaonesha jinsi ambavyo huwajui CCM!
 
Wengi wanashawishiwa kurudi ccm kwa ahadi mbalimbali na nyingi ni maslahi binafsi ya wahusika, hasa njaa kali katika baadhi ya vyama. Na bado!

Waliowakilisha vyama kwenye uchaguzi wa mwaka juzi; hasa pale Dar, wanakumbuka jinsi mawakala wa baadhi ya vyama walivyolala an kushinda njaa hadi kutelekeza usimamizi wa kura za wagombea wao.

Hizi bajeti zinazoishia kurusha helikopta zingetumika kuimarisha matawi naamini demokarasia ingepiga hatua mbele.

Kumbuka, mkono mtupu haulambwi!
 
Wanabodi,
Naomba mchango wenu kuhusu kuondoka kwa hawa jamaa toka Chadema - Kabourou, Laurent Marwa,Chacha Okong'o na Chacha Mwitesya.

Wananchi wanatakiwa kupata ukweli. Tumeyasikia toka CCM, sasa inabidi tupate toka upande wa Chadema!...
Hawa watu ni viongozi wa aina gani?... na hayo madai yao yana ukweli kiasi gani?
 
Back
Top Bottom