Hapo umesema kweli Wengi wangependa kupata dalili ya ukweli wa haya maneno.
Kama ambavyo tunajua hali zilivyo kwenye sayari ambako hatujafika kwa kutumia vile tulivyonavyo hapa ardhini.Vivyo hivyo kwa kutumia akili tulizonazo na matukio yaliyopita hatuhitaji kuingia mitaani Libya au ndani ya ngome za majeshi yanayopigana kujua hali inayofuatia baada ya hapa.
Ukweli tunaujuwa kwa kuangalia hali kule ambako US na allies waliingia kiulaini na hata kuungwa mkono na watu kabla hawajaerevuka baadae.Kwa sasa ni sahihi kusema Amerika na sera zote za vita tangu Bush kule Afghanistan hawajawashinda Taliban kiasi kwamba tishio lao linawafanya US washauriane kuondoka hata kwa aibu.
Iwapo hali kule ni hivyo, kwa Libya ambako mambo yamekwenda kombo tangu mwanzo itakuwa mbaya zaidi.Haitowezekana kuiteka Libya na kuikalia kwa vyovyote na mafuta hayatochimbika kama ilivyopangwa.
Gadhafi kama binadamu hatodumu lakini uhakika atawacha umma ambao hauna urafiki na waasi wala NATO.Baada ya hapo kilicho sahihi ni kuwa UN,NATO na US watakuwa wamefanikiwa kuivuruga nchi ya Libya lakini malengo yao yako hewani kama ambavyo wamefanikiwa kujenga barabara Afghanistan lakini wananchi hazijawashawishi kukubali ukoloni.Nafasi ya kutungua helkopta wakiipata wanaitumia.
Swali ni jee na Amerika nayo ina uwezo wa kuhimili hali hiyo kwa muda gani huku ulimwengu tofauti na zamani wanawaangalia kwa mtazamo wa watu waovu badala ya wakombozi na watetezi?.