Mkuu utantambua,
Hakuna mkamilifu na hilo ,mimi Nonda nimelisema mara nyingi tu. mbali na mapungufu ya Gaddafi hakuna kiongozi wa hata nchi moja ya Afrika ambaye amefanya kwa nchi yake kama Gaddafi amefanya kwa Libya na Afrika.
Kwa hiyo, ukitaka mtazamo mimi ningesema hilo la masofa na silaha ya dhahabu ni katika ufahari wa tamaduni za "waarabu". Lakini, yes, ni ufujaji wa fedha. Lakini jee hivyo vitu vimegharimu kiasi gani cha fedha? Hivi kweli kwa mchango wake wa maendeleo ya nchi ya Libya na yeye hakustahili "kastarehe kidogo"?
Nimalizie kusema kuwa kila mtu ana mapungufu na hilo unaweza kulitia katika mapungufu yake lakini mazuri yake yana uzito zaidi. Kwa bahati wengi wanasemea udhaifu wake mchache na wanaacha mazuri ,au kutokujali kabisa nini amefanya kwa nchi yake na Afrika.
Sasa na wewe, jibu hili. Je unajua jambo lolote jema, zuri ambalo Libya na Afrika ilipata chini ya uongozi wa Gaddafi?