The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Mkuu hayo yote alifanya kwa pesa za walibya na ni si kutoka mfukoni mwake hata Adolf hitler nae alifanya tena mazuri zaidi yake! Lakini je! Hatakama ni wewe ukapewa kilakitu lakini ukakosa uhuru itakuwaje? Ukapewa vitu ukanyimwa utu itakuwaje? Just try to think before write this pumba.

Kama si u......huu ni nini? Uhuru wote ulionao Tanzania wakufaa nini? Acha pumba, uhuru ni baada ya tumbo kushiba...usidanganywe na Wamarekani, wao wanashiba. Nenda vijijini Bongo ukale uhuru wako!
 
Mkuu hayo yote alifanya kwa pesa za walibya na ni si kutoka mfukoni mwake hata Adolf hitler nae alifanya tena mazuri zaidi yake! Lakini je! Hatakama ni wewe ukapewa kilakitu lakini ukakosa uhuru itakuwaje? Ukapewa vitu ukanyimwa utu itakuwaje? Just try to think before write this pumba.
ingekuwa vizuri ukatoa mfano wa watu walionyimwa uhuru. Kwana si hata marekani kuna watu hawana uhuru, mbona hawalipui? Au kuna kitu ambacho wengine bado kukijua?
Haya wameuza nchi yao kwa gharama kubwa. Hivi vitu kama walivizoea wasahau....
 
**************

Source: Catholic News Agency:

{Vatican voices hope for Libya after Ghadafi's death}

**************

After Moammar Ghadafi's death, Libya must chart a new course based on human dignity and the rule of law, the Vatican said in a statement released Oct. 20.

**************

Hakika Hapo kwenye Red ndio ujumbe kwa Mtu yoyote anaetakia mema Libya na kukubali kuwa Mungu aliumba kila mwanadamu na kipawa chake na kuwa si kweli Libya pasipo Gadhafi HAITAKUWEPO.Maisha ya Walibya yataendelea pasipo yeye na kuwa HAKI HAIUZWI,BEI YA HAKI NI KUTENDA YALIYO MEMA KWA WENGINE.
 
Namfikiria mtu unamkamata na hayuko armed. Ya nini kumshindilia risasi? Na labda niulize watoto wake takribani wa3 wameuwawa kipindi hiki.Saif kakamatwa,hajauwawa hata Mutassim wangeweza k uwakeep hai.Anyways. Je Hannibal naye watamuua?
 
Hii ni aibu kubwa kwa mtu aliyejiita The King of Africa! Viongozi wetu nao ni lazima wajifunze kwa yaliyompata mwenzao!
Gaddafi's body on display 1.jpgGaddafi's body on display 2.jpg
 
Wapambe wengi wa Kanali Gaddafi humu jamvini ni wakali na hawaambiliki
(Sijajua ni kwa nini)


*Wengi wao hawapendi kusikia upande wa pili wa shillingi.
*Hawana tofauti na Kanali Gaddafi.
*Yaani wana chembechembe za udikteta.
*Ni bora hawana madaraka (kwani wengi wetu tungewakoma!).

Nimewasilisha!
 
Mjadala wa huu uzi wa kipuuzi umependezeshwa na husninyo na klorokwini. Big up kwenu!
 
Waafrika sasa, hasa wa Afrika mashariki , kama tumeshindwa kujifunza kilichotokea tangu mwanzoni mwa mwaka huu na kinaendelea mpaka sasa huko Afrika ya Libya, Tusije kujilaumu kama wakazi wa Bengharz wanavyosikitika/jilaumu kwa sasa kwa kuwaruhusu vijana wao wahuni kuanzisha ubomoaji wa nchi yao kwa msaada mkubwa wa NaTo. Kumbuka haitakuwa lazima Copy and Paste ya mazingira ya uanzishwaji wa vurugu za Afrika ya kaskazini kwa hapa kwetu Afrika ya mashariki, la asha.......... Tuchanganye na za kwetu kunusuru uhai halisi wa Umoja wa Afrika ambao ungezaliwa upya Septemba mwaka huu na sasa umeharishwa kwa wahuni wachache kukubali kurubuniwa.
 
Mleta mada umekuja kimajungu sana nadhani kuna chembechembe za ............................
Wacha nione watasemaje wadau wengine .Maana ujumbe ulivyo na kichwa chako cha habari mh.
 
Hii ni aibu kubwa kwa mtu aliyejiita The King of Africa! Viongozi wetu nao ni lazima wajifunze kwa yaliyompata mwenzao!

Mkuu
Aibu haiko kwa maiti. Aibu iko kwa wanaoifanyia maiti hivyo. Na jinsi mshindi anavyoitunza na kuiheshimu maiti ya adui wake ndio ushujaa.
Usisahau mayahudi walimsulubu Bwana Yesu. Je aibu ilikuwa kwa Yesu au wale waliomsulubu?
Tujaribu kuelewa maana. Mtu akishakufa hafikwi na aibu. Aibu ni kwa walio hai.
 
Angalieni video hii pia. Walibya wengi wanajieleza.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli mleta mada heading yake alivoijenga na habari yenyewe vinatofautiana sana, seems anasukumwa na ..........
 
Vatican is operated by people with ability and sound mind.they think before talking anything.
 
Binadamu hatuna shukrani. Kwa miaka kumi ijayo kutakuwa na ombwe la uongozi nchini Libya. Na hii kanseli ya ukombozi imeshaanza kuvutana.
Angalia Iraq. Marekani wakiondoka Iran ndiyo itakayojaza ombwe.
 
Back
Top Bottom