The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Ndugu yangu samakai ndani ya maji haoni umuhimu wa maji. Wacha watie adabu, wamejitakia kuunga mkono watu wenye ajenda ya kuwadhoofisha.
 
Ndugu yangu samakai ndani ya maji haoni umuhimu wa maji. Wacha watie adabu, wamejitakia kuunga mkono watu wenye ajenda ya kuwadhoofisha.

Kwa kweli Gaddafi anacho chema cha kumueleza Mungu kuhusu yale aliyowafanyia watu wake, tofauti na wale walioangamiza watu wao kwa kujilimbikizia mali na kuwanyima huduma za msingi watu wao. Mobutu, Bongo, Abacha na wengine wengi ambao walikuwa ni vipenzi vya mabeberu.
 
Vyombo vya habari vya nchi tunazoziabudu sana walitufumba hili na watu wote wakaamini kwamba Gaddafi ni shetani. Kwa kweli namuomba msamaha Gaddafi kwa fikra potofu nilizokuwa nazo kuhusu yeye.
 
Jamani tusubiri tuone hao walioingia sasa wana mchango gani kwa taifa lao,inawezekana wakawapa walibya zaidi ya alivyowapa Ghaddafi,kwa hakika alichokuwa anawapa jamaa ni kingi ni si rahisi kuamini kama ni kweli maana ukikaa na kuangalia sababu ya kumuondoa madarakani wakati wanapata kila kitu,ingekuwa kwetu hapa nadhani mambo yangekuwa safi.
Tuwape muda na tuone watafikia wapi maana wameanza "na SHARIA" kama mwongozo wa namna taifa litakavyokuwa linaendeshwa.
 
Mbopo,
I conquer with all written 100%. One point missing is the connection between the deep sorrow shown by our Minister Membe and Mummar Gaddafi. I do take it as being grounded on personal interests, correct me if I am wrong. Christian have a common proverb which says: "You can't be a Christian more than the Pope"
 
Walibya wameingizwa mkenge na kuitupa almasi baada ya kupewa chupa. Dunia yote watu wanahangaika na kupigania hata nusu tu ya walichokuwa wanakipata wao.

Wakadanganywa kwamba hicho walichonacho ni upuuzi tu mbele ya usanii unaoitwa demokrasia, as if ndiyo inayojaza tumbo au kupeleka watoto shule.


Dah mkuu thanx...
 
Gadafi alikuwa akiwafadhili Janjaweed wa Sudan juzi Al Bashir wa Sudan kafurahia sana yaliyomkuta Gadafi huku akitamba naye alitoa silaha zilizomng'oa madarakani. Safi sana NTC.....BADO NA SISI KUM-GADAFI JK
 
Ni kweli alikuwa anasaidia nchi masikini lkn alikuwa na mapungufu yake,alitanguliza udini mbele zaidi kwenye kutoa misaada,smhn kma nimekuudhi

Askofu au Papa yupi aliwai kujenga mskiti au shule ya kiislama kama msaada kwa kuendeleza uislam?
 
According to several web sources, the National Transitional Council (NTC) announced its offer of amnesty/pardon to anyone from Gaddafi's family or circle of friends who can capture or kill him.

NTC spokesman Mustafa Abdel Jalil, who believes that "the end will only come when he's captured, dead or alive," said Gaddafi's captor or killer can get the money and remain a free man.

Gaddafi has a $2 Million bounty on his head | COOLBUSTER.net

pia hapa Gaddafi to The Hague | Geoffrey Robertson | Comment is free | The Guardian
 
According to several web sources, the National Transitional Council (NTC) announced its offer of amnesty/pardon to anyone from Gaddafi's family or circle of friends who can capture or kill him.

NTC spokesman Mustafa Abdel Jalil, who believes that "the end will only come when he's captured, dead or alive," said Gaddafi's captor or killer can get the money and remain a free man.

Gaddafi has a $2 Million bounty on his head | COOLBUSTER.net

pia hapa Gaddafi to The Hague | Geoffrey Robertson | Comment is free | The Guardian

This means the real Gaddafi killers are the NTC/NATO...kwisha habari
 
spin doctors at work..............na hiki kiinimachowanachotuhubiria nani anawasimamia kukitekeleza?
 
Marehemu Ghadafi wakati wa mapambano yake alipata kusema ya kuwa wale wapinzani wake ni paka,panya na mende tulishindwa kuielewa kauli yake hiyo , lakini sasa tumepata uhakika kweli wale ni Paka,Panya na Mende kwani kitendo walichomtendea Ghadafi kabla ya kumuuwa na baada ya kumuuwa ni cha kinyama ambacho hakiwezi kufanywa na mwanadamu.na hawa wazungu waliwaunga mkono wahuni hawa nao pia ni washenzi hawana ustaarabu hata chembe.
 
True! hawakuwa na ubinadamu tunaoutarajia kwa watu wa kawaida. Ila ili uwe kiongozi wa paka na mende lazima na wewe uwe mmoja wao. Hivyo Ghadafi alikuwa ni rais wa mapaka na mende wa Libya.
 
waacheni jamani na nchi yao watakavyoifanya ndivyo hivyo sisi tuangalie mwanzo wao na huo mwisho wao mimi ninaogopa isije Libya ikawa Second IRAQ?

Tofauti na IRAQ ambayo ina asilimia kubwa (zaidi ya 50%) waliokuwa wakiwa chini ya hatamu ya Sunni wachache na kiongozi Sunni Saddam Hussein, ni kwamba zaidi ya 95-98% ya waLibya ni Sunni. Waliobaki ni dhehebu moja linaloitwa Ibadhi na hakuna kabisa au negligible % ya Shia katika Libya. Ama mayahudi ndio wa kuhesabu mmoja mmoja kabisaaaaa.

Hivyo pamoja na uchochezi wa nguvu ambao Marekani na wafitina wenzake wanaweza kujaribu kupandikiza kama Iraq, itakuwa sio rahisi kufanikiwa kwa hilo. Hata uchochezi baina ya Sunni wa kweli kweli na Sunni wanafiki (secularists) utakuwa na kazi kubwa kufanikiwa kwa maana waLibya wengi generally wanakwenda sambamba katika usomi wa elimu zote mbili zinazowahusu, elimu ya dini yao na elimu ya dunia yao simultaneously. Sio rahisi kumkuna msomi wa Degree, Masters au Phd akawa mjinga wa dini yake kama ......

InshaAllah Mwenyezi Mungu awasafishie waLibya jihadi yao kutokana na malengo machafu ya Marekani na NATO na mafatani wenzao yaliyowapelekea kujidai kujihusisha kimizengwe mizengwe katika kumuondosha na kumuua Gadafi. Ni wao ndio waliolisambaratisha convoy lake kwa mabomu yao kwanza wakati akiwa anakimbia kuokoa maisha na usalama wake na sio kwamba alikuwa anafukuzia au anaelekea kuwadhuru waLibya, kitu ambacho ndio kinge-warrant NATO airstrike intervention kwa mujibu wa mandate za kifisadi walizojitangazia wenyewe.

Mungu awazidishie upofu ili kila wanaouona kuwa upenyo ugeuke kuwa kwao mtego, Afghanistan, Iraq, Kenya-Somali na kwengine kote watakakoelekeza fitina zao. Na Mwenyezi Mungu ailinde nchi yetu na fitina zao.
 
Mimi kilicho nishangaza ni pale walipokuwa wanamfanyia vitendo visivyo vya kibinadamu walikuwa wanapiga kelele wakisema Allah-Akbar wakimaanisha Allah Mkubwa hii haikuingia kichwani kwangu.
Ukitilia maana wao ni waislamu na wameanzisha Sharia katika nchi hiyo cha ajabu walikuwa wanafurahia vitendo vya kuua watu.
 
Back
Top Bottom