kahtaan
JF-Expert Member
- Jul 11, 2009
- 18,760
- 11,343
Hivi pamoja na matatizo yote yanayotukabili kama taifa Mohamed Said anataka tujadili habari za Kighoma Malima hapa kwenye Jukwaa la siasa; kwa nini hii isipelekwe jukwaa la historia? Sasa hivi tunahangaika na namna ya kukinusuru chama tawala, chama chetu pendwa ambacho hivi sasa kinapanga kusherehekea miaka 37 ya uhai huku kukiwa na hofu ya kulazwa ICU kikichungulia kaburi. Tafadhali Ritz mfikishie mwalimu wako, Mohamed Said, hili ombi kutoka kwangu...atuache tupumue!
Mkuu hii kwa wewe unaweza kuiita HISTORIA lkn kwa vijana kama sisi wapenda haki NI FIKRA ZILIZO HAI MPAKA KESHO!
Na kama tutapata changa moto za namna hii basi yale Aliokuwa akiyapanga na kuyatamani yafanyike mzee wetu Kighoma Malima basi Kwa uwezo wake Mola SISI VIJANA TUTAYATEKELEZA!
Na kama sisi hatutofika huko kwa asili 100% basi watoto wetu watakamilisha!
Sasa kama wewe unaona Umebanwa na pumzi kwa haya maneno ya haki basi unaruhusiwa kutokuchangia chochote humu.
Na rather nenda ka support hizo kampeni zenu za mifumo ya kumaliza wengi kwa kuneemesha wachache.