The Tussle Between the President and the Professor: The Story of Prof. Malima


We kijana mara nyingi umekuwa ukimkashifu Marehemu mzee Malima kwa kusema. Mara hakuwa na uongozi bora! Mara maongezi yake na lectures zake hazikuwa na maana!
Kumbuka yule muheshimiwa Alikabidhiwa WIZARA NYETI SAANA na NCHI!
Tena awamu zote mbili!

Sasa wewe na hao wenzako watoa kashfa! Kama nyie mna elimu saana na ni mahodari wa kuongoza
Chadema inasambaratika kwa kukosa watu wa kusimamia chama chao!

Hebu jisogeze huko ukasaidie.
Huwezi kujua. Muheshiwa Dr Slaa amesha halalisha GONGO!

Labda we ukikazana kidogo unaweza kuwa waziri wa hio wizara ya wasema ovyo!
 
nketi,

Keti chini ufunzwe kwanza tena kwanza ufunzwe adabu kisha ufunzwe elimu ya kweli, unaleta pumba za uzushi na uwongo hapa? At least umekiri kuwa mauwaji ya kimbari ya Zanzibar yamefanywa na wagalatia wenzio, mkristo gani wa kweli anajisifia mauwaji? Zanzibar ni mwiba waroho umewakaa baiana ya kuta za koromeo lenu kashindwa 'Baba yenu wa Taifa' mtaweza nyinyi "Yatima zake?"

Una quote wayahudi, hali wayahudi hao unaowasifu wanawabagua kule kwao wanasema Isarel sio pahala pa waafrika wewe bado unajibandika Uyahudi mweusi.
Wakati wa apartheid kule SA wao ndio walikuwa wakiwapa silaha na kuwafundisha makaburu namna ya kuwauwa waafrika na wakifanya hivyo hali ya kuwa UN imewawekea vikwazo Makaburu. Hao Wapalastini ndio waliokuwa bega kwa bega na ndugu zao wapigania uhuru kule Libya na kwengineko duniani.
Sasa wewe unatukana wasomi na waislamu kama sheikh Mohammed Said hali ukijisifia kuwa katika ile picha wale wazee walikuwa mbumbumbu kuliko wakristo watatu hayo ni matusi maana mwalimu JK alikubali kuwafuata mapaka akafanyiwa maduwa mazito na pia kufunga kwa ajili ya maelekezo yao aliyaona yanafaa. Hata hiyi speech ya UN mwaka 1952 hakuiandika mwenyewe muulize Maalim Mohammed Said atakujuvya.

Hutaki kujifunza basi katafute Mbwa muoane naona ndio wagalatia mumepata njia mpya ya uongofu.

Pole sana
 
Last edited by a moderator:

Teh teh teh!
Mkuu maneno yako kama msumari wa moto kwenye kidonda!

Duhh!
 
Last edited by a moderator:

Nitakuja kukujibu jioni baada ya kazi; kuna matatizo makubwa sana na baadhi ya wasomi, jambo ambalo itabiidi niliongelee kwani ukiangalia siasa za Profesa Malima wakati huo, hazina tofauti kabisa na siasa za Profesa Lipumba ambaye alikiri hadharani kuwa ingawa uchaguzi wa 2010 ulikuwa siyo huru, yeye alikubali matokeo kwa vile aliyeshinda alikuwa ni "mwezao" huko msikitini; yaani tatizo kubwa linakuwa ni Slaa na CHADEMA badala ya matatizo halisi ya nchi. Wasomi hao ufanya mambo hayo kwa kujua kuwa audience yao ni watu wa aina gani, ikiwa ni pamoja na wewe.
 

Sasa kwa nini alikwenda kutoa hiyo the so called Professorial Inaugural Lecture kwao kama alikuwa anajua ni pro-Nyerere, na yeye alikuwa ni against Nyerere. Lecture hiyo aliitoa wakati Nyerere alishatoka kabisa kwenye siasa na keshaachia hata uenyekiti wa CCM. Kwanza yeye malima mwenyewe alipoteuliwa kuwa waziri wa uchumi mwaka 1982 ndiye aliyekuja na ile SAP ya mwaka huo ambayo ilikuwa ni pro-Nyerere zaidi na ilipingana kabisa na mawazo ya Edwin Mtei.
 

Na wewe roho inakuuma saana ukiona kiongozi MUISLAMU anapewa SUPPORT NA WAISLAMU SIO??

Hizi chuki zenu huwa zinawasababishia magonjwa ya moyo na mnakufa vifo vibaya!

Kwanza ulileta hoja ya kuwa MALIMA HAKUWA KIONGOZI MZURI!
Nimekuonyesha kuwa Marais wako wawili walimkubali kuwa ANAFAA KUONGOZA WIZARA NYETI kama hizo!

Na wewe intelligence yako compare to the PRESIDENT ni kama umlinganishe tembo na uchafu tu!

Yaani there is no Comparison!

Sasa unaleta UDINI wa kuwa Audience wao WALIKUWA WAISLAMU!

Sasa we ulitaka wawe nani!?
Makafiri??

Mbona nyerere alipokuwa akipewa support na KANISA KATOLIKI na yeye kulineemesha hukusema kitu!

Au.ndio nyie mnao neemeka na jasho la wananchi na kukuza matumbo huku mkiangalia waislamu vipi wanaendeleza mambo yao.!! Na kufanya hila ili wasifanikiwe sio??

Mnfnssssssss!
 

Mheshimiwa Bwana Mkubwa,

Angalia maneno yako hayo niliyowekea bold. Iwapo ni kweli marais wawili walimpa wizara kuongoza na mmoja wao katika maneno yako akiwa ni "Kafiri" huoni contradictions na uwongo hapo. Kama Makafiri walikuwa wanawabana waislamu, basi Malima asingepewa Wizara kuongoza. Kushindwa kuona alikotoka ni weakness kubwa sana kwa uongozi na ndipo Malima alipoishia. Malima alibebwa sana na Nyerere hata baada ya Muislamu Mwenzie Abdulrahman Babu kumkataa bado Nyerere alimbeba lakini leo anasema Nyerere Kafiri alikuwa anawaonea Waislamu. Kama Nyerere alimzima kabisa Oscar Kambona alyekuwa mtoto wa mchungaji wa kilutheri, unadhani kweli alikuwa anashindwa kumzima Malima asionekane tena? Hizo ni sehemu ya pumba za Malima, ni mtu aliyekuwa hana busara.

Pili ewe Bwana Mkubwa wa wote jitahidi uelewa kuwa kuwa Waziri siyo kipimo cha uwezo, hata Mulugo naye aliwahi kuwa waziri lakini anajua kuwa Tanzania ni Muungano wa Tangayika na Zimbabwe. Iwapo Malima alikuwa na uwezo mkubwa kiasi hicho asingefukuzwa Ukatibu Mkuu na Babu (siyo Mgalatia wala Kafiri), na vile vile asingehamahamishwa wizara harakaharaka kwa kipindi kifupi; alihamishwa wakati wa utawala wa Mwinyi (siyo Mgalatia wala Kafiri), kwani alimtumikia Nyerere kwa miaka mitatu tu kabla Nyerere hajastaafu. Mawaziri wenye Uwezo katika Uchumi na mipango kama akina Cleopa Msuya na Amil Jamal walidumu sana katika Wizara hiyo ya fedha, ambapo Malima alirushwa rushwa na kuishia kutupwa nje tena kabla hajaanza kutuonyesha sisi watu wa nje mapungufu wake. Tuliokuwa wasomi wakati huo tulifurahia sana kupata waziri wa uchumi ambaye pia ni msomi na profesa wa uchumi lakini akaishia kuwa kama tunavyomjua leo. Elimu siyo busara, ni afadhali ukose elimu lakini uwe na busara kuliko kukosa busara ukawa na elimu kwani pumba zako zinakuwa zinaonekana sana unapokuwa na elimu kama aliyokuwa nayo Malima.

Kwa ufupi, ukosefu wa busara ndio uliomfanya Malima ashindwe kuongoza. Mara zote failures hupenda sana kutafuta scapegoats, na ndipo failure Malima akaja na kisingizio cha dini, ambayo alijua itamsadia atapata wafuasi wa aina yako wengi.
 

We.mkuu maneno yako meeeeengi unarudia tu!
Labda nikuulize swali kidogo hapa.

Profesa Kighoma Malima ALIKABIDHIWA WIZARA ZOTE HIZO MBILI kwa ELIMU YAKE? au.kwa nasaba yake. Au kwa sababu gani hasa!
Manake kwa maelezo yako unaonekana UNAFAHAMU KULIKO YULE ALIYEMPA KAZI.

Ule ugalatia na uislamu weka pembeni.
Haya hebu leta ufafanuzi hapo.
 

Muda mzuri sana huu kabla sijaenda kulala.

(1) Ugalatia na Ukafiri ni ajenda zako ambazo nilitaka kukuoneysha jinsi gani zina walakini. Unaowaita wewe pamoja wafuasi wa mMalima kuwa ni Wagalatia na Makafiri waliompiga vita ndio siyo tu waliomsomesha (yaani Nyerere) bali pia ndio waliomfanya wewe umjue (Nyerere huyo huyo), lakini unaowajua wasafi (waislamu) Abdulrahman Babu na Ali Hassan Mwinyi) ndio walimonwa kiutendaji hafai; Inakurudia wewe. Unakuwa na nguvu katika hoja unapokuwa unajua unaloongea siyo maongezi ya kubabaishababaisha kama haya unayoweka hapa. Mimi ninamjua Malima vizuri sana tena kwa undani kuliko wewe unavyoweza kuwa unamjua kwani nilikuwa kati ya wasomi wachache wa wakati huo tuliokuwa wafuasi wake tukifurahia mwenzetu (ingawa nilikuwa sijafikia levo yake wakati huo) kuwa mmoja wa waendesha nchi.


(2) Nimekukumbusha kuwa Malima hakuwa unique katika positions alizopitia; kuna wengi sana waliozipitia na kati yao kuna wajinga na wenye akili waliwahi kuzishika; sitaki kusema Malima alikuwa kundi gani kati ya hao bali rekodi inajisemea yenyewe. Kuwako kwake kwenye position hizo hakumfanyi yeye kuwa mtu wa ajabu katika jamii. Aliingia mahali asipoweza ndiyo maana akaamua kujaribu sehemu anazoweza zinazohusu ubaguzi wa dini, ambako alifanikiwa kuacha wafuasi wa aina yako lakini siyo jina la kihistoria katika nchi kama wenzake akina Nyerere, Karume, Kawawa, Sokoine, Jamal na wengineo wanavyokumbukwa.


(3) Nilitaka kuandika hapa mafundisho fulani kutoka kwenye saikolojia kuhusu walalamikaji ila nimejizuia kwa sababu ya upana wa tafsiri zake yasije yakachukuliwa out of context; ni mafundisho yanayokuhusu wewe kwa karibu sana na watu wa aina yako.
 

Narudia tena!
Maneno yako meeeengi lkn haya lolote la maana!
Hii ni thread ya nne unajiita WEWE NI MSOMI!
Zaidi ya hii jf sidhani kama wewe umo.ktk wale wenye kufahamika!
Nimekuuliza swali fupi , badala ya kutoa jibu. Unaruka ruka!

We huwezi kuja hapa kufundisha watu Historia za redio kifua!
Wewe wala mimi SIO waliomuweka malima ktk Nafasi alizokuwa nazo enzi zake!
Aliwekwa hapo KWA SABABU MAALUM! Na sio bahati mbaya!

Sasa wewe MSOMI inakuwaje ushindwe kututajia hizo sababu au hizo SIFA alizokuwa nazo ambazo ZILISABABISHA YEYE KUKABIDHIWA HIZO NAFASI?

Hapa sio nani kampa uongozi au nani kamnyang'anya!

Wacha kuzunguka zunguka halafu unaita wengine wababaishaji!

Toka mwanzo statement imetolewa kuwa ALIYE BADILI system ya mitihani ni Malima!
We unatuonyesha VYETI!

Sasa ina maana we mtu mzima hujui tofauti kati ya VYETI na MTIHANI??

Haya anza tena upya.
And this time be straight.

Bla bla inapoteza wakati.
 

Tatizo Lako Mohamed ni Kila issue you it a religious one. every time ni waislam wameonewa... Waislam hivi.... Waislam vile...., it time to move on.
 
Ni wajib wangu kuieleza dhulma. How can we move.on while all opportunities are blocked?
 

Ninajua kuwa kuna tofauti sana baina ya uwezo wa watu kujua mambo. Kuna wanaotaka kutafuniwa kila kitu ili wameze na kuna wanataka kupewa nyama na kuitafuna wenyewe. Maswali yako ni yale ya mtu anayetaka kutafuniwa na hiyo ni wazi kabisa kwa nini unamtetea Malima. Unatumia vigezo vya kiwango cha chini sana katika madaia yako.

(1) Kumtetea uwezo wa kuongoza kwa kutumia kigezo cha SIFA na kusema alipewa madaraka na watu wa juu kuliko mimi kwa sababu ya SIFA zake na hivyo alikuwa kiongozi mzuri ni upungufu mkubwa sana katika uwezo wako wa kufikiri. Unashindwa kujua kuwa kupewa madaraka kwa sababu ya watu kudhani una uwezo ni kitu kimoja, halafu kunyang'anywa madaraka hayo kwa sababu wamegundua kuwa huna uwezo huo ni kitu kingine. Sifa pekee ianyobaki kwenye rekodi ya Malima ni ile ya kunyang'anywa madaraka siyo ile ya kupewa. Kupewa madaraka ilikuwa ni matokeo hypothesis kuwa anaweza kuongoza, na kunyang'anywa madaraka ndiyo proof ya hypothesis yenyewe kuwa hawezi kuongoza. Sasa wewe nao unalilia hypothesis wakati proof ipo kuwa Malima alishindwa. Jifunze kuwa unakubali ukweli, kuwa msomi wako ashindwa madaraka; ni jambo la kawaida kabisa kwa wasomi wengi kushindwa madaraka kwa vile wanakuwa more technocrats, na wala isikuhuzunishe au kujiaminisha kuwa ni kwa sababu ya Wagalatia au Makafiri. Ni bahati nzuri kuwa alikuwa ananyang'nanywa madaraka hayo na waislamu wenzake, including Kikwete. Sijui ungetuambia nini leo iwapo yeye ndiye angekuwa katika position ya Kambona kihistoria!

(2) Malima alikuwa Waziri wa Elimu mwaka 1987 na tayari tulikuwa tunatumia namba za mitihani; nimekuonyesha vyeti vya mwaka 1980 na 1982 vikionyesha namba hizo, na hiyo ni kudhihirisha Malima aliwaambieni uwongo kuhusu namba za mitihani na nyinyi wameza pumba mkazimeza kavukavu bila hata kuzichambua na mpaka hapo hujaamini kuwa Mwaka 1980 watu tayari walikuwa wanatumia namba za mitihani kutokana na kulewa pumba za Malima.

Halafu Waziri wa Elimu siyo mtendaji wa baraza la mitihani, hawezi kusimamia utungwaji na usahihishaji wa mitihani; mitihani imekuwa inatungwa na Baraza la mitihani ambalo halikuwa na uhusiano wowote na Wizara ya Elimu. Mwenyeketi wa Baraza la mitihani alikuwa ni Vice Chancellor wa Chuo kikuuu cha Dar es Salaam, na kuna wakati alikuwa ni Ibrahim Kaduma (huyo hakuwa Galatia wala Kafiri kama unavyowaita watanzania wengine wasiokuwa dini yako)

(3) Ninaweza kuwa siyo msomi wa kiwango chako au kiwango cha Malima lakini nina uwezo wa kuchambua uwongo na ukweli. Umekuwa unaandika uwongo mwingi sana kuhusu Malima kama vile wote tunaosoma hapa JF ni mbumbumbu kama. ... sijui nani.
 


Na wewe unafikiri kwa mapovu: hapa tunamuongelea Malima halafu wewe unakuja na mambo ya Kikwete na kiongozi anayetaka kwenda Magogoni, sijui unamuongelea Lowasa, Januari au Zitto kwani hao ndio tunaojua kuwa wamekwisha tangaza nia zao kutaka kwenda Magogoni. Kwa vyovyote uwezo wako wa kuona mambo na kuyajengea hoja ni duni sana, labda kwa sababu unayona kwa kutumia mwanga wa dini tu.
 
Du kweli ww hamnazo.......naona namna gani unaokota okota....Hebu niambie nchi gani afrika ambayo muislamu aliongoza kutafuta uhuru.
 
Hizo tungo zako za uongo sijui zinakusaidia nini. Sehemu zote ukombozi haupiganiwi na mtu mmoja lakini kunakuwa na mtu mmoja mwenye akili kubwa ya kuongoza akili zingine na nyerere alikuwa kiongozi. Unashangaa kwamba inawezekana sijawahi kusikia mtu anaitwa faiza mafongo! Yaani nisikie MKWAWA, KINJEKITILE NGWALE (Hawo ndo watu wa maana) halafu nisikie na hao waliokuwa wananyatia kwa nyuma na pengine walikuwa maarufu tu kwa kupiga soga vijiweni. Tunawasikia mashujaa
HEBU JIPANGE VIZURI
 

Duh! Leo imekuwa humjui hata kiongozi anaetaka kuhalalisha gongo? Amma kweli, wajinga ndio waliwao.
 

Nketi,
Umerejea lakini naona umekuja na kejeli.

Mie kujibu kejeli kwangu ni muhali.
Ila kwa faida ya ukumbi nitakuwekea kwa muhtasari habari za Idd Faiz Mafongo.

Mafongo alikuwa mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na wakati
huo huo alikuwa mwekahazina wa TANU.

Mafongo alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnatougo Hall Agosti 1954.

Mafongo ndiye likabidhiwa jukumu la fedha kwa ajili ya safari ya Nyerere ya kwanza
UNO 1955.

Mafongo ndiye liyemjulisha Nyerere kwa Sheikh Mohamed Ramiya wa Bagamoyo.
Yapo mengi.

Labda Nketi nikukumbushe kitu kidogo.

Mkwawa, Kinjiketile, Selemani Mamba, Ali Songea Mbano, Abdallah Mchiama, Abushiiri bin
Salim
na mashujaa wengine walionyanyua silaha dhidi ya Wajerumani wote hao walikuwa
Waislam kama unavyoona hao hapo chini waliokuwa na Nyerere katika kupigania uhuru wa
Tanganyika.

Na huu si uzushi.




Kushoto Kwenda Kulia: Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro
na Haruna Taratibu. Picha imepigwa Dodoma Railway Station wakiwa katika harakati za kufikisha ujumbe
wa TANU kwa wananchi.
 
Ni wajib wangu kuieleza dhulma. How can we move.on while all opportunities are blocked?

usichoke ndugu huo ndo wako wajiiib
tuko pamoja nawe kila utakapo kwenda wameifungia TV Iman kisa waeleza ukweli
 
Asante sana mkuu Kichuguu sisi tunafyonza elimu unayotoa..
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…