These Are The Top USAID Recipients—From Religious Groups To Major U.S. Companies—As Trump Targets Agency

These Are The Top USAID Recipients—From Religious Groups To Major U.S. Companies—As Trump Targets Agency

Hivi niwaulize ndugu zangu USA wanapata wapi haya mabilioni ambayo wanatapanya Dunia nzima kwa style hii??? Imagine Kanisa linapewa Bil 4 dola unadhani PAPA atasema jambo akisikia USA wanaua watu????

Mkuu hiyo ni mada nyingine kabisa! Nakumbuka tu hii pesa ya USAID Inayopewa na serikali ni 1% katika budget yao! Ndio maana wengine wanamlaumu Trump huku Marekani kuwa 1% unayoiingilia na kuumiza watu ulimwenguni itakusaidia nini! Wanaona ana lake jambo! Unajua budget ya Pentagon?

Ndugu yangu Somoche, Marekani inapata wapi pesa, ni mada kubwa kabisa, labda kukupa mwanga tu ungeazia kusoma kazi ya huyu bwana, W.W Rostow- The Model of Economic Growth, Japo theory yake ni ya muda, lakini huwa nakubaliana naye, Marekani iko katika stage ya tano ya maendeleo duniani,( Age of Mass Consumption) nchi nyingi sana haziwezi kufika Marekani alipofika, mpaka marekani yenyewe ianguke, kwa vita au majanga! Si kwamba haitanguka! Wakati nchi nyingi duniani, hasa za Kiafrica tuko stage ya pili kiuchumu ( Precondition for take off)

Kwangu mimi siamini kabisa sisi tunaweza kutoka kwa misaada kama ya USAID, ni upuuzi na ujinga tu! Nimefanya mashirika haya, nikaona tunachezewa akili, lakini hatuna jinsi!

1739089884785.png
 
Hizi forms ni kwa ajili ya US NGO. Wewe NGO yako ya Tanzania unajazaje hizo form? Kwani wewe ni US taxpayer? Hapo kwenye form inabidi uingize EIN number ambayo ni sawa na TIN number huku kwetu. Utaipata wapi?
Wanadai kwamba non-U.S can apply maana yake unakuwa registered kama international NGO kwa uelewa wangu hata huku Tz ili uwe na sifa ya Internationational NGO utaratibu ni kama founders ni wanne watatu lazima wawe wenyeji na moja awe foreigner 1:3.
 
Sasa kama unataka kuwa International NGO na ufanye kazi US, it is your choice and not a requirement to any NGO. Unapofanya SAM registration huambiwi ujaze hizi forms.
 
Makombo tu mkuu.
Mkuu Doctor G, temea mate chini mkuu! Hayo makombo wengine yamebadili maisha yetu! Professional yangu ya kwanza ni Mwalimu wa Sekondari! Ningebakia huko leo, nisingeona dunia! Nakubali ni makombo kabisa! Lakini yamebadili maisha yangu binafsi! ingawa najua wazi hayawezi kubadili Taifa zima!
 
Mkuu cassavaleaves kwenye Black budget ya taasisi za ujasusi CIA pekee wanatumia takriban $14.7bn ndani ya $52.6bn zilitengewa taasisi 16 za ujasusi.
 
Kwanza siku hizi hakuna DUNS number kuna UEI, na hata wakati ilipokuwepo ilikuwa inatolewa bure tu ila kwa watu wasiojua walikuwa wanapigwa na makampuni binafsi online. Ni kama DV kama hujui waweza lipishwa wakati ni bure.
Kujisajili SAM ni requirement kwa kila organization (US and non US alike) as long as utapata US government funds, whether through a contract or grant.
Thanks mkuu, umempa jamaa shule bila kulipia ada, akushukuru kwa maarifa hayo uliyomongezea
 
Makombo tu mkuu.
Kuwa na Shukrani wewe! Sema kama hukubahatika kupata ufadhili wa USAID! Jamaa walikuwa anamwaga hela mpaka watu wanachanganyikiwa! Kuna vi local vingi tu vilinufaika na miradi ya USAID kupitia RTI (hawa walikuwa na mradi sijui wanauita HESHIMU BAHARI au maliasili? Na mambo ya utafiti kwenye afya); fhi360 mambo ya ukimwi na tohara. Huku kote local NGOs zimefaudu sana! Hapo hakuna cha makombo wala ukoko!
 
Hivi niwaulize ndugu zangu USA wanapata wapi haya mabilioni ambayo wanatapanya Dunia nzima kwa style hii??? Imagine Kanisa linapewa Bil 4 dola unadhani PAPA atasema jambo akisikia USA wanaua watu????
Ni michango ya wananchi
 
Kuna watu huku walikuwa wanashangaa mabilion ya dola kutengwa na USAID kwa nchi za Africa wao wanajua kwamba pesa inaingia direct kwa nchi husika.
Kuna pesa za USAID huwa zinaingia direct cash kabisa serikalini kupitia miradi mbalimbali ya serikali na wizara zake.
 
Sasa kama unataka kuwa International NGO na ufanye kazi US, it is your choice and not a requirement to any NGO. Unapofanya SAM registration huambiwi ujaze hizi forms.
Ni vizuri sio lazima kwasababu priority ya grants inakuwa kwa mashirika yaliyosajiliwa kwao ndio maana kwetu local NGOs nyingi tunaishia kuwa partners,na pia tovuti ya www.iris.gov wanatoa ITIN (Individual tax identification number wanachohitaji ni passport kwa wageni.
 
Kuwa na Shukrani wewe! Sema kama hukubahatika kupata ufadhili wa USAID! Jamaa walikuwa anamwaga hela mpaka watu wanachanganyikiwa! Kuna vi local vingi tu vilinufaika na miradi ya USAID kupitia RTI (hawa walikuwa na mradi sijui wanauita HESHIMU BAHARI au maliasili? Na mambo ya utafiti kwenye afya); fhi360 mambo ya ukimwi na tohara. Huku kote local NGOs zimefaudu sana! Hapo hakuna cha makombo wala ukoko!
Nimefanya na ifakara health institute chini ya THPS,wakubwa ndio walifaidi.
 
Nimefanya na ifakara health institute chini ya THPS,wakubwa ndio walifaidi.
Sasa hapo nyie mlikuwa third party, tofauti lazima uione kwa hiyo usiseme USAID ilikuwa inatoa makombo. Hapo nyie mlikuwa partner wa waswahili hamkusaini mkataba na USAID. THPS ndio walifaudu!
 
Back
Top Bottom