cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
- Thread starter
- #41
Hivi niwaulize ndugu zangu USA wanapata wapi haya mabilioni ambayo wanatapanya Dunia nzima kwa style hii??? Imagine Kanisa linapewa Bil 4 dola unadhani PAPA atasema jambo akisikia USA wanaua watu????
Mkuu hiyo ni mada nyingine kabisa! Nakumbuka tu hii pesa ya USAID Inayopewa na serikali ni 1% katika budget yao! Ndio maana wengine wanamlaumu Trump huku Marekani kuwa 1% unayoiingilia na kuumiza watu ulimwenguni itakusaidia nini! Wanaona ana lake jambo! Unajua budget ya Pentagon?
Ndugu yangu Somoche, Marekani inapata wapi pesa, ni mada kubwa kabisa, labda kukupa mwanga tu ungeazia kusoma kazi ya huyu bwana, W.W Rostow- The Model of Economic Growth, Japo theory yake ni ya muda, lakini huwa nakubaliana naye, Marekani iko katika stage ya tano ya maendeleo duniani,( Age of Mass Consumption) nchi nyingi sana haziwezi kufika Marekani alipofika, mpaka marekani yenyewe ianguke, kwa vita au majanga! Si kwamba haitanguka! Wakati nchi nyingi duniani, hasa za Kiafrica tuko stage ya pili kiuchumu ( Precondition for take off)
Kwangu mimi siamini kabisa sisi tunaweza kutoka kwa misaada kama ya USAID, ni upuuzi na ujinga tu! Nimefanya mashirika haya, nikaona tunachezewa akili, lakini hatuna jinsi!