TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Ipo imani mara tunapofariki uhai huutenga mwili ambao kiimani huuita "udongo",
Nafsi hai hii huondoka zake baada ya kuuacha mwili,na ipo imani huenda kuingia ndani ya kiumbe hai kingine kwa maisha mapya.
"Why don't we uses" REST IN PEACE AND BORN AGAIN IN ......../
Imani hiyo ya re-incarnation imeenea sana India ila huku kwetu haijaenea kiasi hicho!
 
Kimara ipi?Mbona huyo jamaa alikuwa anafahamika sana Kimara,ina maana hakukutokea mtu anayemfahamu hadi watu wakamuua?
Duh!
 
View attachment 426997 View attachment 426990
Thomas Mashali,bondia mashahuri wa Tanzania amefariki usiku wa leo baada ya kupigwa mapanga maeneo ya Kimara.Inasemwa kuwa Mashali alikuwa kambini akijiandaa na pambano,lkn alitoka kambini na jamaa zake na kwenda kunywa moja moto na moja baridi.

Baada ya kupata kilaji,Mashali alihama Bar moja na kwenda nyingine,ambapo wanasema akilewa huwa anakuwa na fujo.Sasa aliingia Bar nyingine akaanza kuleta ubabe wa kupiga watu.Raia wakamuitia mwizi,watu wakaja na mapanga na marungu wakampiga mpaka kufa.Walipokuja kugundua ni Mashali,ilikuwa ameshauwawa na kupoteza damu nyingi.

Madereva wa bodaboda wakamchukua na kumpeleka Muhimbili.Mpaka sasa mabondia wanakusanyika Muhimbili kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.

Kwa Heri Bondia Thomas Mashali.

RIP
 
Mkuu Tembo wapo kabisa na ni halisi, wanagawana maeneo.

Mimi hawa niliwafahamu baada ya Tembo wa Ubungo kwenda kuvamia kituo kipya cha Mbezi Mwisho, kukatokea vita kali sana na wale wa Ubungo wakatimshwa, sasa baadae tena kukatokea mtafaruku wa Tembo wa pale Mbezi mwisho mpaka ikafikia kugawana stendi, mwingine alichukua stendi ya Malamba Mawili.

Mashali alikuwa ni Tembo wa Manzese, sina uhakika utawala wake ulikuwa unaishia wapi lakini jamaa alikuwa na eneo kubwa analomiliki kwa muda mrefu tu.

Hebu nieleweshe kuhusu hawa Tembo, Ni wakala wa Serikali kukusanya pesa vituoni?
Wanatoa huduma gani kwa madereva wa daladala?
Je! hizo pesa zinaishia mikononi mwao au zinaingia pia serikalini?
Kama si shughuli halali kwanini bado wapo na vyombo vya usalama hawiwashughulikii?
 
Watu wanashift kwenda mars kwa sasa...kwanini tusiombee roho yake ikawe reborn Mars maana wazungu washaanza safari sasa.
 
Sijui raia walioshiriki kuutoa uhai wake wamefaidika na nin mpaka wakati huu.
 
Huyo jamaa alikuwa anajihusisha na wizi wa chini chini kwa kutumia nguvu zake
 
Hebu nieleweshe kuhusu hawa Tembo, Ni wakala wa Serikali kukusanya pesa vituoni?
Wanatoa huduma gani kwa madereva wa daladala?
Je! hizo pesa zinaishia mikononi mwao au zinaingia pia serikalini?
Kama si shughuli halali kwanini bado wapo na vyombo vya usalama hawiwashughulikii?

Kifupi ni kwamba hawahusiani na serikali, ila tu wanakuwa na ulinzi wa mapolisi wa maeneo husika kwa sababu kuna mgao unaokwenda kwao.

Unaweza ku-google 'Underground boss" au "Underworld boss" kujua mifumo yao inavyofanya kazi, ni copy cat za ki-Mafia.

Ila kwa hawa Tembo ni at very low scale, siyo kwa level za hao Mafioso, uchukulie tu kama mfumo.
 
Alikuwa ni jamaa fulani anayeishi maisha ya uswahili japo jina lake ni kubwa sana.
images

MASHALI2.jpg
 
Israeli mtoa roho jana alitembelea kimara basi na lori kuungua bondia kuuawa lakini hii tabia wananchi kujichukulia sheria mkononi mbaya sana na yakukemea na kuwekawa matamko yenye uzito sikuiz mtu hata ukiwa na bifu na mtu tu ukiitiwa mwizi unauawa kwann hii tabia inaachwa iendelee ee Mungu tusaidie[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hebu toa Taarifa inayoeleweka, kama alikuwa mwizi au mbakaji tusitoe pole wala RIP
LICHA YA KUWA MAARUFU KTK NGUMI ILA ALIKUWA MWIZI,MKABAJI....NA SHUGULI YAKE YA TOKEA ZAMANI ALIKUWA HAJAIACHA
ALIZOEA KUWAIBIA TEMEKE,TANDALE,MANZESE HUKO MAANA SI NDIYO WANAMJUA SASA KAENDA KIMARA KAYAKANYAGA HUKO...SASA SJUI ALIJARIBU KUWAIBIA AU MAANA INASEMEKANA ALIITIWA MWIZI....NDIYO KACHEZEA KICHAPO.

OVA
 
Huu mchezo unaweza kumkuta yeyote, muda wowote, inabidi ukomeshwe haraka. Upiversity unatoka na manzi anayemtaka, anakuitia tu mob wanakutanguliza mbele ya enzi.

R.I.P Mashari/Mashali.
 
Back
Top Bottom