TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

1477893181933.jpg
 




Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye.
Taarifa zinaeleza ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuokotwa vichakani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.
CHANZO - SALEHE JEMBE BLOG
 
Nimesikia hii habari kupitia EFM,may his soul rest in eternal peace
 
Very sad.
R.I.P kamanda.
Wauwaji wasakwe kwa udi na uvumba😉😡🙁
 
ni habari mbaya sana, Mungu amlaze mahali pema peponi..amina
 
Nimesikiliza vizuri radio wametangaza hivi

Alikua kwenye bar moja kimara anakula masanga[emoji481][emoji481] na washikaji zake sasa pale kwenye meza akawa amepishana maneno na jamaa mmoja, ndio huyo aliyekua akijibizana nae akaita mwizi.... Na hapo ndio watu waliokua eneo hilo wakamvaa na kuanza kumpiga na mapanga, malungu mpaka bondia huyu nguli kupoteza uhai.

Ikumbukwe alitoka morogoro juzi na jana mchana alikua kwenye kongamano la mabondia na jioni alipoenda kupooza koo[emoji481] ndio mauti yakamkuta.. Pia mashali alikua anatakiwa ajiandae na pambano lake siku za karibuni.

Bwana ametoa na bwana ametwa jina lake lihimidiwe[emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom