Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Premature entrance to socialism was one of the worst failure of Nyerere regime
 
ali waweka rumande baadhi ya matajiri, babu yetu akiwemo๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ
 
Alijua watamsumbua..

Alikuwa mjamaa kweli kweli, lakini kuendesha nchi changa kama hii yenye watu milion karibu kumi kipindi hicho na wasomi hawafiki 200.. haikuwa rahisi
Shida historia ime wekwa kijamaa, Kuna watu hawaja pewa heshima walio stahili.

kina Sykes wame saidia Sana, Kuna watu wa tabora pia.
 
Tanzania ni kubwa karibia mara mbili ya Kenya, ina rasilimali nyingi zaidi ya Kenya na ardhi kubwa ya kilimo kuliko Kenya.
 
Malengo yalikuwa mazuri ila matokeo yakaja ndivyo sivyo
Ingawa maendeleo aliyokua anayapigania Mzee Nyerere na Hali ilivyo kwa nchi zilizoiga ubepari toka mwanzo hata hatutofautiani sana, South Africa hiyo hapo mbona nao wamefeli tu
 
Bado hujasema
 
Nchi zina sababu zao za kufeli kulingana na muktadha mbalimbali na matatizo waliyokuwa nayo.
 
Tanzania ni kubwa karibia mara mbili ya Kenya, ina rasilimali nyingi zaidi ya Kenya na ardhi kubwa ya kilimo kuliko Kenya.
Upo Sawa mkuu,

Lakini ukubwa wa nchi na resources sio hoja, Mindset za viongoz wake ndio kila kitu...

Kama mindset hazipo sawasawa kuendelea ni ndoto ..

Miaka 40 baada ya Nyerere kutoka madarakani kuendelea kumlaumu sio kumtendea haki ..

Mambo mengine tunakosea wenyewe .

Wapo watu hawastahili kabisa kupewa uongozi, lakini tujiulize nani anawafanyia vetting?

Wananchi wanawapigia tu kura bila kujali...

Huko Upinzani ndio balaa tupu.
 
Shida historia ime wekwa kijamaa, Kuna watu hawaja pewa heshima walio stahili.

kina Sykes wame saidia Sana, Kuna watu wa tabora pia.
Mkuu wanasiasa wa Tanzania Nyerere aliwajua kitambo sana...

Angalia kina Msigwa, Dr. Slaa, Lema, Covid?

Unadhani anaeandika historia ya Upinzani asipowataja atakuwa kakosea mahali?
 
Wazungu wa west siku zote wamekuwa wakidemonize socialism na communism. There is no way watasifia ujamaa au kumsifia kiongozi wa kijamaa. Chuki za kiitikadi zipo deeply ingrained ni kama ambayo hamas hawezi kusifia chochote cha yahud au shabiki mnazi wa simba asivyoweza kuisifia Yanga.
Ni wazungu hao ndio ambao wamekuwa wakitoa skolaship kwa baadhi yetu kwenda kusoma kwenye vitabu vyao, vyuo vyao, kufundishwa na hao wazungu, na tunakuwa indoctrinated kuwa ujamaa ni mbaya na Nyerere was bad.

Kuna nchi jirani kadhaa, ambazo hazikufuata ujamaa wala hazikuwa na mtu kama Nyerere, ZIKO WAPI KIUCHUMI?

Na toka Nyerere kaondoka, tuko wapi kiuchumi?
 
Malengo yalikuwa mazuri ila matokeo yakaja ndivyo sivyo
Ingawa maendeleo aliyokua anayapigania Mzee Nyerere na Hali ilivyo kwa nchi zilizoiga ubepari toka mwanzo hata hatutofautiani sana, South Africa hiyo hapo mbona nao wamefeli tu
South Africa hakuna Siasa za Ujamaa wala Ukomunisti. South Africa ni full Ubepari.
Je, hao South Africa wamefeli nini?
 
Kqa
Hyo successor wa nyerere ni mkapa na na magufuli ambae hata kujua kama atakua raisi hakushuhudia hv unaupofu au unamalengo yako jee nyerere alipokelewa uraisi na mkapa than akampasia magufuli hii ni historia au maharage ya wapi au ni sucseer wa kigangoni hebu weka wazi
 
Zao la ujamaa, unadhani nyumba inaanza kujengwa roof kabla ya foundation?
Miaka 40 yote bado unalalamikia msingi? Mipango miji mibovu analalamikiwa Nyerere wakati yeye mini yake ameacha imepangiliwa, barabara mbovu analaumiwa Nyerere, rais kua na msafara wa magari 120 kwenye ziara yake lawama ni kwa Nyerere, ufisadi mkubwa lawama ni Nyerere, elimu mbovu lawama ni Nyerere, huduma mbovu za afya lawa ni Nyerere, mtu akishindwa kumpa mkewe mimba lawama ni Nyerere, mwanaume akishindwa kusimamisha lawama ni Nyerere, uchawa lawama ni Nyerere.

Tunakoelekea hata mtu akila chakula kichafu akaharisha lawama zitaenda kwa Nyerere, mtu akikosa choo lawama zitaenda kwa Nyerere, mtu akinywa sumu akaua figo zake na maini lawama zitaenda kwa Nyerere, mtu akigongwa na gari barabarani lawama zitaenda kwa Nyerere. Hii nchi imejaa watu wa hovyo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ