Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Kufa kwa sekta binafsi, utegemezi wa raia kwa serikali kuu kwa karibia kila kitu, siasa za mfumo wa chama kimoja kisichowajibika ipasavyo kuleta maendeleo.
Fafanua raia anategemea serikali kwa lipi?
 
Fafanua raia anategemea serikali kwa lipi?
Hujawahi kusikia watu wanalalamika kwa waziri au hata Rais shule ya kijijini kwao haina madawati au matundu ya choo?? Halafu shule yenyewe unakuta iko sehemu wanazalisha mbao!
 
Ukiona unalaumu waliokutangulia jua wewe ni sehemu ya tatizo na unachotanya ni kuongelea kile kile kilichofeli kwa sauti nyingine ila hakuna utakachobadili.

Kimsingi,ukiwa na uwezo wa kuchambua wapi alipatia then ukabaini alipopungua ukasema sisi tutadeal na haya matatizo kuanzia hapa kuendelea mbele.

Kwani kuna mtu anahoji leo kwamba ujamaa au ubepari ni issue? Kwani hii inchi kwasasa mifumo ya kiserikali ni ya kijamaa kweli au ndio basi imekuwa miyeyusho tu?
 
Hujawahi kusikia watu wanalalamika kwa waziri au hata Rais shule ya kijijini kwao haina madawati au matundu ya choo?? Halafu shule yenyewe unakuta iko sehemu wanazalisha mbao!
Na akitokea mtu akataka kujenga hiyo shule,kununua madawati na kujenga vyoo kwa gharama zake na kwa kutumia michango ya wanainchi wazalendo, basi mkurugezi na watendaji wa halimashauri,diwani,mbunge na serikali lazima watamtangazia vita na kumuona ni mhaini na mhujumu uchumi. Mixer kumharibia biashara zake na kumbambikia kesi za kumchafua na kumshusha kiuchumi.

Wanataka raia wawe katika hii hali ya utegemezi ili wao waigize kuwa ni wakombozi kila mwaka wa uchaguzi kuja na ahadi mpya za kitapeli.
 
Wanataka Nyerere afufuke akawafanyie yote hayo ili wazidi kuneemeka.

📌📌📌Uafrika ni laaaaannnnaaaaaa😭😭😭😭
 
Una tofauti gani na ujamaa wa Magufuli?
 
Bila wakoloni mngekuwa mshapotea kwa kuugua UKIMWI,vipindupindu na Malaria.Bila mkoloni mpaka kesho mngekuwa mnakunya machakani.Mkoloni mpaka kesho anaendelea kutujengea mashimo ya choo😂😂😂upendo ulioje huo.Kula ule wewe ila karaha ya mavi yako anaona mtu yupo huko maelfu ya maili Ulaya😣😣😣

Ashukuriwe mkoloni kwa kututoa tongotongo na kutustaarabisha maana mpaka kesho bila mkoloni Waafrica wangekuwa kundi moja na punda,nyani na sokwe.

Ashukuriwe mkoloni maana bila yeye magari,ndege na treni ingekuwa ni maajabu walau saivi tunaenda nao bampa tu bampa ukitoa ukiritimba wa kodi ya TRA leo tungekuwa tunamenya maganda na kuendesha gari mpya zerooo KM🤗

Mkoloni hana tunachomdai kwakua hatuna kitu tumewaprove wrong tangu wametuachia nchi zaidi ya kutaka na kupenda kujifananisha nao.

Ikiwapendeza wakoloni warudi AFRICA.Wajitwalie tena hili bara maana muafrika ameonyesha hawezi ishi bila mzungu.


📌📌MKOLONI AACHWE APUMZIKE AMILIFANYIE MENGI MAZURI HILI BARA LA GIZA.
 
Ukimsoma Deng Xiaoping vizuri ukamsoma na Mao Zedong vizuri ukasoma kipindi ilichopitia China wakati wa Mao hasa miaka kumi ya mwisho wa utawala wake na ukasoma kipindi ilicho pitia China chini ya Deng hasa miaka ya mwanzo ya utawala wake ukarudi kusoma tena ulicho andika utaona umeandika ujinga.
 
Kuna watu ambao sio wanafiki Ulimwengu.lissu na Mohamed said utajua sana mapungufu ya Julius K Nyerere.

Huwa napenda kuwasikiliza na kuelewa wanachokiongea ili kujua palipopungua
 
Nyerere alikuwa mjinga mwenye confidence kubwa hana tofauti na Magufuli.
 
Malengo yalikuwa mazuri ila matokeo yakaja ndivyo sivyo
Ingawa maendeleo aliyokua anayapigania Mzee Nyerere na Hali ilivyo kwa nchi zilizoiga ubepari toka mwanzo hata hatutofautiani sana, South Africa hiyo hapo mbona nao wamefeli tu
Mwl. Dr Julius Kambarage Nyerere aliyemuingiza chaka la Ujamaa ni Wazanzibari waliokuwa wamesomea uhanaharakati Cuba,East Germany, Soviet, Yugoslavia n.k
Mmoja wao ni Profesa Abdullah Babu waziri wa Uchumi na mipango.

Pili muungano na Zanzibar,wao walifungua ubalonzi wa Ujerumani Mashariki wakati Tanganyika tulikuwa na Ujerumani Magharibi.
Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru the mighty West Germany ilikuja kwa nia mmoja kuijenga Tanganyika kiuchumi,viwanda,Elimu iwe mfano wa kuigwa duniani.Mjerumani alikuuja kwa mbwembwe tena akitaka kumuonyesha Mwingereza kuwa hawakufanya lolote kwa miaka 70.
Mara huko Zanzibar nayo ikafungua ubalozi na East Germany.mbaya wa West Germany.
Mbabe West Germany akamtaka Raisi Nyerere afunge ubalozi wa East Germany mara mmoja. Nyerere akawajibu wasimchagulie rafiki.
West Germany ikafuga ubalozi Dar ndio hivyo Mjerumani akatutosa mmoja kwa mmoja.

Karata ya pili Nyerere aliwakimbilia Israel wahimarishe vyama vya Ushirika,kilimo cha kisasa kwa peasants. Kuanzisha Jeshi la kujenga Taifa .
Cooperative Unions zikashahimili,Mashamba darasa ya kilimo yakafunguliwa,ukakamavu wa kujenga utaifa kwa wasomi kupitia JKT ukatamalaki.
Lakini 1967 six days war kati ya Israel na Nchi za Misri, Jordan na Syria,Tanzania ikavunja uhusiano na Israel.

Nyerere karata ya tatu akiambatana na Abdullah Babu kwenda China ya Mao kutafuta ufadhili wa kujenga reli ya Tazara na mengine yakafuata ndio ikazaliwa Azimio la Arusha ambalo ndio siasa ya ujamaa na kujitegemea.
 
Historia za nchi za Afrika zinasikitisha na kuaibisha
 
Historia za nchi za Afrika zinasikitisha na kuaibisha
Kuna makala ya Profesa Babu anasema Western trained Nyerere hakujua kabisa propaganda za nchi za Kikominist katika safari yao ya kwanza kutembelea China anasema alionyeshwa vijiji vya ujamaa viko na nyumba,maji umeme,shule,hospitali, barabara nzuri,maduka.Kumbe ni vya kuigiza tu.
Anasema Nyerere alienda amevaa western suit lakini kurudi Tanzania akaja amebatizwa na ki Mao,hakuvaa tena western suit.
Kwa lugha nyepesi Nyerere was Compromised by Chinese.Alifuata njia nyingine ya siasa za kijamaa alizokuwa hazielewi vizuri.
 
Kwa lugha nyepesi Nyerere was Compromised by Chinese.Alifuata njia nyingine ya siasa za kijamaa alizokuwa hazielewi vizuri.
Mao mwenyewe alikuwa kashaingia chaka , mamilioni waliokufa kutokana na sera zake tushukuru hatukupitia hayo
 
Ni kweli, Ujamaa wa Nyerere ulikuwa na matokeo mabaya sana kwa Tanzania japo lengo lilikuwa zuri. Hata hivyo umekuwa na faida pia katika suala la umiliki ardhi.

Fair to say that...kuna mengine yalikuwa mabaya. Na mengine mengi mazuri.
Kosa letu kubwa ni kutohakikisha mazuri yanalindwa na mabaya yanaondolewa.
Mfano, uadilifu kwenye nafasi za umma ulikuwa una kasoro gani?
 

Kati ya Prof Babu na Mwalimu Nyerere, nani alikuwa mkomunisti kindakindaki?
 
Uelewe Jambo moja unapojadili haya mambo.
Ujamaa na ukomunisti Ni vitu viwili tofauti.
Kiingereza Socialism na Communism.
Tanzania haijawahi kuwa nchi ya ukomunisti bali Ujamaa.
Kuna nchi nyingi tu duniani hata Ulaya zenye Ujamaa na wajamaa zilizo endelea. Ndani ya Marekani, Germany na kwingineko wapo watu wanachama wa chama cha kijamaa.
 
Ni kweli, Ujamaa wa Nyerere ulikuwa na matokeo mabaya sana kwa Tanzania japo lengo lilikuwa zuri. Hata hivyo umekuwa na faida pia katika suala la umiliki ardhi.
tafadhali tupatie mfano wa hizo faida zilizopatikana kwenye umiliki wa ardhi, ambao kwa sasa ni utapeli na dhuluma kwa asilimia kubwa
 
Kati ya Prof Babu na Mwalimu Nyerere, nani alikuwa mkomunisti kindakindaki?
Profesa Babu alikuwa mjamaa haswa akiamini katika Ujamaa wa Kisayansi Mwanaharakati mahili wa Pan Africanism,
Alikuwa ni rafiki wa Mwenyekiti Mao alimtembelea 1959 huko China.
Mimi namkumbuka alipokuwa Waziri wa Uchumi na Mipango akitoka nyumbani kwake kwa mguu hadi ofisini kwake wakati mwingine anapekuwa hana viatu.
Na siku nyingine anakuja na baiskeli yake.
 
Misingi mikuu ya Ujamaa na Ukomunisti inafanana kwa kiasi kikubwa Sana, almost kama Ujamaa na Ukomunisti ni Kitu kimoja. There is a very slight difference between them.

Aidha, Tanzania ni nchi ya UKOMUNISTI, labda wewe hauna uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala haya ya Ukomunisti/Ujamaa.
Sera ya Mwl.Nyerere ya Azimio la Arusha ni Copy and paste from USSR, China, Cuba and North Korea.

Nakupa Homework: Fanya Utafiti wako wa kina kuhusu Sera ya Itikadi ya Juche kwenye Ukomunisti na Kisha linganisha na Sera za Mwl. Nyerere juu ya Siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea (misingi 3 ya Ukomunisti: Jaju, Jiraw na Jurip)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…