Thread maalum ya wapenda Pikipiki kubwa

Vyuma mbali mbali ulimwenguni.
 
Imetulia sana halafu imeuzwa bei ya kuku [emoji16]
 
Sele mapikipiki anabei za kawaida sijui kwa kua yupo zanzibar au niaje
 
Kwenye kupeana maelezo tutambue kwenye hizi pikipiki zipo kama magari kuna ya sports,za mjini na biashara,safari ndefu na off road kwenye kufanya maamuzi bora utambue ilo
 
Kuna kesi ilikuwahi kumkumba jamaa mmoja jirani, wanaishi nyumba ya kupanga na wapo wapangaji kama saba hivi wenye pikipiki na zote zinalala sebuleni.
Katika pikipiki hizo zote zilikuwa ndogo (fekon, Huoniao na Boxer) kasoro jamaa alikuwa na chuma kama hicho pichani.

Usiku mmoja wakaingia wezi wakapuliza madawa yao ya usingizi na kuchukua pikipiki zote ndogo ila XR wakaiacha!

Walioibiwa hawakuelewa wakajua ni mchongo wa jamaa hivyo akawekwa ndani, aliulizwa kwa nini pikipiki yake ilikuwa ndiyo ya kwanza kabisa karibu na mlangoni lakini imesogezwa vema kabisa na kuwekwa pembeni na zikachukuliwa nyingine?
Jamaa akajibu, itakuwa wezi walijua hizi nyingine kuziuza ni fasta na hata wakisema wauze spare ni mara moja, lakini wakiichukua hii machine itabidi mpaka ipate watu wake hivyo biashara itachelewa, lakini pia hizi ziko chache hivyo ni rahisi kuonekana hata ukiiuza wapi.

Jamaa akashinda akaachiwa [emoji2]
 
"itabidi mpaka ipate watu wake"[emoji3]
 
Hawa ni Honda na KTM, ni jamii ya sports na zinazumbua duniani kote katika michezo na mashindano.
 
Hawa ni wazee wa 'nzito' na ni kwa ajili ya safari ndefu.
 
Barabara korofi haipitiki? Hawa ndio nyumbani kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…