Thread ya kuomba ushauri nasaha kuhusu tatizo la kiafya linalonisibu kwa muda mrefu sasa

Mpamila

Member
Joined
Oct 4, 2026
Posts
50
Reaction score
46
Habarini za wakati huu wanajamii forum.

Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 23.Nimekuja hapa kuomba ushauri nasaha juu la tatizo la kiafya linalosumbua kwa muda wa miaka mitano sasa .

HISTORIA YA TATIZO (Nahisi ndiyo chanzo lakini madaktari huwa wanakataa wakidai havina uhusiano)

Mwaka 2020 mwezi december tarehe 25 nilifanyiwa operation ya kuondolewa kidole tumbo (Appendicitis) baada ya kuhangaika na maumivu ya tumbo yaliyoanza kusambaa mwili mzima kwa siku takribani tatu (3). Vipimo vilionesha kuwa kidole tumbo kina shida (kimejaa kinakaribia kupasuka).

Operation ilienda vizuri kwa masaa takribani 6 ,nikatoka salama nikiwa na maumivu tofauti na niliyokuwa nayo mwanzo.

Tatizo la kwanza : MAFUA YASIYO ISHA/MZIO WA MAFUA (ALLERGY).
SIku moja kabla ya Operation niliwekewa mrija wa plastic uliopitishwa kuanzia kwenye tundu la pua,kooni na ukaishia tumboni sikujua ni kwa kazi ipi maana nilikuwa sijitambui ipi maana sikuwa nimefanikiwa kula au kunywa chochote kwa siku 2 mfululizo.

Tatizo ambalo nahisi ni allergy nilikuja kuligundua miezi 6 mbele baada ya kuwa kila nikiamka asubuhi napiga chafya zisizo na idadi zinazoambatana na mafua ,ikawa nikikaa kwenye sehemu ya vumbi,moshi au harufu kali ya perfume kwangu ni tatizo kubwa mno.

Tatizo la pili [KUBWA].
Kabla sijafanyiwa operation hiyo 2020 nilikuwa ni mchezaji hodari wa mpira wa kikapu (Basketball) ,mpira wa miguu ilikuwa mara moja moja na mazoezi ya kukimbia mara kwa mara huku pumzi na nguvu nikiwa nazo.

Baada ya operation niliambiwa nisifanye shughuli yoyote ngumu au nzito kwa kipindi cha miezi miatatu (3) ,hili nililitimiza kwa 100%.

Shida nikaanza kuiona miezi 6 baadae pale nilipoanza kufanya mazoezi ya kawaida ,kukimbia ,basketball na football.

Ikawa nikifanya shughulu yoyote pumzi zinabana ,kifua kinabana, miguu inakosa nguvu, misuli ya mikono, mwili mzima kukosa nguvu ,jasho jingi ,kizunguzungu ,macho kuona weusi na kupumua kwa shida sana.

Mwanzo nilihisi labda ni kwa sababu sikuwa nafanya mazoezi kwa muda mrefu ,nikawa naanza kufanga mazoezi mdogo mdogo ili kuretain hali ya kawaida ,ila nakumbuka hiyo 2021 kuna siku nilipoteza fahamu kabisa nikiwa kwenye mazoezi ya kukimbia.

Hali iliyofanya niachane kabisa na michezo ,
Miaka ikazidi kwenda mwaka jana nilienda hospital nikamuelezea dokta hali nayopitia kuhusu mafua akasema hakuna uhusiano kabisa na operation niliofanyiwa na kuhusu hali ya mwili kukosa nguvu akasema labda ni upungufu wa damu akachukua kipimo cha FULL BLOOD PICTURE (FBP) lakini akakuta kila kitu kipo kawaida sina tatizo.Nikaenda hosptali nyingine mara 3 napo wakasema shida itakuwa damu lakini walivyopima hawakukuta tatzio.

Kuhusu mafua na chafya mpaka sasa bado nasumbuliwa ila natumia cetrizen mara kwa mara pale napoona nimezidiwa ila tatizo lake inanisababishia uchovu na usingizi mzito muda wote na sijajua kama matumizi ya muda mrefu kama hayana madhara mwilini

Sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata nikitembea eneo lenye mwinuko mkali au kufanya mazoezi ya kukimbia au kuendesha baiskeli,kupanda ngazi n.k hali ya misuli ya miguu na mapaja kuchoka na kuna muda inakuwa kama imeganda kabisa yani nashindwa kwenda mbele au nyuma ,jasho jepesi hasa eneo la kichwa, mwili mzima kuishiwa nguvu ,kizunguzungu, macho kuanza kuona weusi mbele ,tumbo kuvuruga .

Kurudi hali ya kawaida ya mwili huwa inachukua takribani dk 45 mpaka saa zima na hapo natakiwa nikae eneo lenye hewa ,ninywe maji kiasi kadhaa .

Hili swala limenitesa sana nashindwa kujua tatizo ni nini maana nisipofanya shughuli yoyote nzito mwili unakuwa na hali ya kawaida tu.

Hivyo nimekuja kuomba ushauri wa either kipimo cha kufata hasa kwenye hili tatizo la mwili kuishiwa nguvu na kushindwa kupumua vizuri, au kama kuna aliewahi kupata tatizo kama langu na kupona n.k

Hata kama ni dawa asili nipo tayari.

Naamini hili jukwaa lina watu wanaoujua ,madaktari wanaoelewa matatizo kama haya n.k

Naomba kuwasilisha🙏
 
Pole sana mkuu,
I can feel mtu ambaye umezoea kuwa active daily suddenly unaambiwa usifanye tena workouts. Pole mkuu, JF ni jitu kubwaaaaaa sana ninayo imani utasaidika!
Ahsante sana mkuu ngoja nisubiri🙏
 
GEMINI anasema.....

Aaah, samahani sana kwa kuelewa tofauti! Nilichukulia kana kwamba wewe ndiye mwenye tatizo moja kwa moja.
Kama ni mdau wa JamiiForums anaomba ushauri, unaweza kumsaidia kwa kumnukuu au kumueleza kwa ufupi mambo haya makuu ili yamfaae kwenye uzi wake:
1. Kuhusu Mrija na Operesheni (NG Tube): Mrija ule unaitwa Nasogastric Tube (hutumika kusafisha tumbo au kutoa gesi/majimaji kabla au baada ya upasuaji). Wanachosema madaktari ni kweli—mrija huo hawezi kusababisha allergy ya miaka 5. Mzio wa hewa/vumbi (Allergic Rhinitis) mara nyingi huanza kujitokeza utu uzimani, na muda ulioanza ulikuwa ni sadfa tu na operesheni.
2. Dawa ya Cetirizine na Mafua: Cetirizine ndiyo inayomfanya awe na uchovu mwingi na usingizi mzito. Mshauri amuone daktari wa pua, koo na masikio (ENT) ili apewe dawa za kupuliza puani (Nasal Steroid Sprays kama Fluticasone), ambazo hazina madhara ya kuleta usingizi au uchovu.
3. Tatizo Kuu la Kukosa Nguvu na Pumzi (Exercise Intolerance / Syncope):
* Hali ya kupoteza fahamu, macho kuona weusi, na misuli kuganda anapofanya mazoezi siyo tatizo la damu (FBP).
* Anahitaji vipimo vya kina vya Moyo na Mapafu kutoka kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Physician), Cardiologist, au Pulmonologist katika hospitali kubwa ya rufaa (kama Muhimbili, KCMC, Bugando, n.k.).
* Vipimo anavyopaswa kuomba/fanyiwa ni:
* Moyo: ECG, Echocardiogram (Echo), na Cardiac Stress Test (Treadmill Test).
* Mapafu: Spirometry / PFT (ili kuangalia kama ana Exercise-Induced Asthma/Bronchospasm).
4. Ushauri wa Haraka kwake:
* Aache kabla hajapata madhara makubwa kufanya mazoezi makali, kupanda milima, au kuendesha baiskeli kwa kasi hadi hapo atakapopimwa moyo na mapafu.
* Aepuke dawa za asili zisizojulikana kwani zinaweza kuongeza presha kwenye moyo.
Unaweza kuchukua maelezo haya na kumwekea kama jibu kwenye huo uzi wake wa JamiiForums!
 
Ahsante sana mkuu nimepata mwanga kiasi flani ,🙏
 
Nitaufanyia kazi ushauri wa gemini
 
Mkuu pole sana, umefanikiwa kwenda hospital ya level ipi? . Maana kama wanakupima tu FPB sijui mara wingi wa damu maana yake ni hospital ya level ya chini. Mi niliwahi kwenda hospital fulani nikalalamika nina kizunguzungu tu, hapohapo ma vipimo ya moyo yakafanyika. Sasa nashangaa wewe ujielezee hivyo halafu upime vipimo vya kawaida tu?. Nenda hospital kubwa angalau kuanzia level ya mkoa au hata kanda kabisa. Kama uko Dar nenda Muhimbili moja kwa moja. Pole sana.
 
Ahsante sana madam ,nitaufanyia kazi ushauri wako, mwaka jana nilienda agha khan , mwaka huu ilikuwa ni Iringa referall hospital nao wakapima FBP tu ,ngoja nifanye mpango wa kwenda kubwa zaidi
 
Poa mkuu,ila kwa sasa epuka matizi wewe tembea tu, hadi utakapopata suluhisho.
 
Pole mkuu...

Upo mkoa gani? Ulienda hospital zipi? Hebu fanya ufike Bugando, Benjamini Mkapa, muhimbili au hospital kubwa za Dar es salaam...

Mi nahisi upo nyanda za juu huko na hali yako inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya matibabu yasiyo sahii pamoja na hilo baridi la huko ndio kabsa....
 
Niko Iringa mkuu ,ahsante itabidi nifanye hivyo 🙏
 
Habarini za wakati huu wanajamii forum.

Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 23.Nimekuja hapa kuomba ushauri nasaha juu la tatizo la kiafya linalosumbua kwa muda wa miaka mitano sasa .

HISTORIA YA TATIZO (Nahisi ndiyo chanzo lakini madaktari huwa wanakataa wakidai havina uhusiano)

Mwaka 2020 mwezi december tarehe 25 nilifanyiwa operation ya kuondolewa kidole tumbo (Appendicitis) baada ya kuhangaika na maumivu ya tumbo yaliyoanza kusambaa mwili mzima kwa siku takribani tatu (3). Vipimo vilionesha kuwa kidole tumbo kina shida (kimejaa kinakaribia kupasuka).

Operation ilienda vizuri kwa masaa takribani 6 ,nikatoka salama nikiwa na maumivu tofauti na niliyokuwa nayo mwanzo.

Tatizo la kwanza : MAFUA YASIYO ISHA/MZIO WA MAFUA (ALLERGY).
SIku moja kabla ya Operation niliwekewa mrija wa plastic uliopitishwa kuanzia kwenye tundu la pua,kooni na ukaishia tumboni sikujua ni kwa kazi ipi maana nilikuwa sijitambui ipi maana sikuwa nimefanikiwa kula au kunywa chochote kwa siku 2 mfululizo.

Tatizo ambalo nahisi ni allergy nilikuja kuligundua miezi 6 mbele baada ya kuwa kila nikiamka asubuhi napiga chafya zisizo na idadi zinazoambatana na mafua ,ikawa nikikaa kwenye sehemu ya vumbi,moshi au harufu kali ya perfume kwangu ni tatizo kubwa mno.

Tatizo la pili [KUBWA].
Kabla sijafanyiwa operation hiyo 2020 nilikuwa ni mchezaji hodari wa mpira wa kikapu (Basketball) ,mpira wa miguu ilikuwa mara moja moja na mazoezi ya kukimbia mara kwa mara huku pumzi na nguvu nikiwa nazo.

Baada ya operation niliambiwa nisifanye shughuli yoyote ngumu au nzito kwa kipindi cha miezi miatatu (3) ,hili nililitimiza kwa 100%.

Shida nikaanza kuiona miezi 6 baadae pale nilipoanza kufanya mazoezi ya kawaida ,kukimbia ,basketball na football.

Ikawa nikifanya shughulu yoyote pumzi zinabana ,kifua kinabana, miguu inakosa nguvu, misuli ya mikono, mwili mzima kukosa nguvu ,jasho jingi ,kizunguzungu ,macho kuona weusi na kupumua kwa shida sana.

Mwanzo nilihisi labda ni kwa sababu sikuwa nafanya mazoezi kwa muda mrefu ,nikawa naanza kufanga mazoezi mdogo mdogo ili kuretain hali ya kawaida ,ila nakumbuka hiyo 2021 kuna siku nilipoteza fahamu kabisa nikiwa kwenye mazoezi ya kukimbia.

Hali iliyofanya niachane kabisa na michezo ,
Miaka ikazidi kwenda mwaka jana nilienda hospital nikamuelezea dokta hali nayopitia kuhusu mafua akasema hakuna uhusiano kabisa na operation niliofanyiwa na kuhusu hali ya mwili kukosa nguvu akasema labda ni upungufu wa damu akachukua kipimo cha FULL BLOOD PICTURE (FBP) lakini akakuta kila kitu kipo kawaida sina tatizo.Nikaenda hosptali nyingine mara 3 napo wakasema shida itakuwa damu lakini walivyopima hawakukuta tatzio.

Kuhusu mafua na chafya mpaka sasa bado nasumbuliwa ila natumia cetrizen mara kwa mara pale napoona nimezidiwa ila tatizo lake inanisababishia uchovu na usingizi mzito muda wote na sijajua kama matumizi ya muda mrefu kama hayana madhara mwilini

Sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata nikitembea eneo lenye mwinuko mkali au kufanya mazoezi ya kukimbia au kuendesha baiskeli,kupanda ngazi n.k hali ya misuli ya miguu na mapaja kuchoka na kuna muda inakuwa kama imeganda kabisa yani nashindwa kwenda mbele au nyuma ,jasho jepesi hasa eneo la kichwa, mwili mzima kuishiwa nguvu ,kizunguzungu, macho kuanza kuona weusi mbele ,tumbo kuvuruga .

Kurudi hali ya kawaida ya mwili huwa inachukua takribani dk 45 mpaka saa zima na hapo natakiwa nikae eneo lenye hewa ,ninywe maji kiasi kadhaa .

Hili swala limenitesa sana nashindwa kujua tatizo ni nini maana nisipofanya shughuli yoyote nzito mwili unakuwa na hali ya kawaida tu.

Hivyo nimekuja kuomba ushauri wa either kipimo cha kufata hasa kwenye hili tatizo la mwili kuishiwa nguvu na kushindwa kupumua vizuri, au kama kuna aliewahi kupata tatizo kama langu na kupona n.k

Hata kama ni dawa asili nipo tayari.

Naamini hili jukwaa lina watu wanaoujua ,madaktari wanaoelewa matatizo kama haya n.k

Naomba kuwasilisha🙏
Umepima presha mkuu.
 
Ukipata muda waombe wakupime vipimo vyote vikubwa ikiwemo cha damu, figo, ini, mapafu, moyo na mishipa ya fahamu.

Pole sana kwa changamoto unayopitia.
Shukrani sana mkuu🙏
 
Back
Top Bottom