Thread ya kuomba ushauri nasaha kuhusu tatizo la kiafya linalonisibu kwa muda mrefu sasa

Anza kufanya vipimo vya moyo na mapafu yako +mfumo wa upumuaji(mapafu,bronch) utakuja na mrejesho hapa. ila usiwe na shaka hakuna kinachoshindikana chini ya jua
Ahsante sana mkuu🙏
 
Pole sana mkuu sasa kuna hili kabla hatujaingia kwenye issues za kisaikolojia hebu fanya hivi dalili zako haziwezi kuhitimishwa kuwa za kisaikolojia bado. Kama kupoteza fahamu wakati wa mazoezi, kifua kubana, kizunguzungu, macho kuona giza na miguu kuishiwa nguvu ni hizi ni dalili zinazohitaji uchunguzi wa moyo na mapafu. Kipimo cha damu (FBP) hakitoshi. Mimi kwa nafasi yangu ya kisaikolojia nilipaswa nikupe rufaa kwa daktari kwa vipimo hivi:

"ECG" na "Echocardiogram" (ultrasound ya moyo)
Exercise stress test na Holter monitor (kufuatilia mapigo ya moyo)
Spirometry, kupima pumu ya mazoezi "exercise induced asthma", kwani una shida ya mzio na kifua kubana na
Sukari ya damu na tezi ya shingo "thyroid"

Unapaswa pia kuomba kuonana na daktari bingwa wa moyo (cardiologist) na asifanye mazoezi mazito hadi apimwe. Kuhusu Cetirizine, unaweza kuuliza daktari au mfamasia dawa mbadala isiyoleta usingizi sana na badala ya kuitumia kila mara bila ushauri.

Baada ya hapo sasa ndio tutaanza changamoto ya kisaikolojia (kwa muhtasari)

1.Kutokuwa na uhakika kwa muda mrefu. Wa miaka mitano bila jibu na madaktari wanne wanasema "huna tatizo" hilo pia huleta huzuni, hasira na hisia kwamba hasikilizwi (medical invalidation).
2. Kupoteza utambulisho ulikuwa mchezaji hodari na sasa hawezi hili julieta huzuni ya kupoteza (grief) ambayo mara nyingi haitambuliki sana kwenye jamii yetu ya kitanzania.
3. Kupata hofu baada ya kupoteza fahamu mwaka 2021, inaweza kuwa ni hofu ya mazoezi inayokufanya aepuke juhudi zako jambo ambalo linaloidumisha tatizo.
4. Kutafuta chanzo kimoja kinachohusisha kila kitu ikiwemo na operesheni jambo linalosukuma kutafuta majibu kwa msongo mkubwa.

Nadharia za kisaikolojia zinazokufaa ni pamoja na "CBT" ikwa mawazo ya kuogopa au "nitazimia tena" ni tabia ya kuepuka.
"ACT" (Acceptance and Commitment Therapy) kukubali hali usiokunayo na uhakika huku ukijenga maisha yasiokuwa na maana na kujiona ushapoteza na ustahili kwa kupoteza utambulisho wako wa mchezaji wa kiapo or mpira wa miguu.
Narrative Therapy: uatakiwa kupata msaada wa kuandika upya hadithi yako zaidi ya "mchezaji aliyepotea au kustaafu kwa lazima"
-Self-efficacy (Bandura): kurejesha imani ya mwili wako kwa hatua ndogo ndogo, baada ya kupata idhini ya kitabibu.

Muhimu sana: usianze na saikolojia

Kwa mawasiliano yangu +255748951191, Facebook,Instagram, Thread, LinkedIn Robert James pia utagusa hi Link Figma
 
Ushauri mzuri sana , ingawa pia kuna mambo ambayo yanahitaki kutiliwa maanani:

A: Mzio/Allergy:
Allergy hutokea katika umri wowote pale unapopata kianzilishi. Inawezekana ukawa na allergy na material ya plastiki/kemikali zilizotengenezewa plastiki ambayo baada ya kutumia/NGT ukawa umeanzisha tatizo. Ingawa unayo nafasi ya kumwona daktari bingwa wa magonjwa ya masikio, pua na koo/ENT kwa uchunguzi, tiba na ushauri pia dawa zilizo salama zaidi.

B: Mwenendo wa mwili
1: Operation ya kuondoa apendeksi ilichukua saa 6, hii inaonyesha kuna kazi iliyochukua muda zaidi ya ule wa kawaida.
2: Mapumziko aliyoambiwa na daktari ni ya miezi mitatu, ambao ni muda mrefu pia baada ya operation ya apendeksi.

Hoja ni: Je aliweza kurejea kwa daktari aliyefanya oparation na kumweleza maendeleo yake na jinsi anavyo jisikia? Hapa daktari anaweza kueleza pia kama kipindi cha operation kuna walichokiona au kifanya ambacho kinaweza kuwa jibu au majibu kwenye maendeleo yake ya afya.
 
Anha sawa mkuu shukrani sana 🙏
 
Oh sasa mkuu ,sikuwahi kurejea kufatilia ,itabidi nifanye hivyo
 
Pole sana mkuu,

Mwili wa binadamu ni moja ya maajabu kuu ya ulimwengu, una uwezo wa kujitibu wenyewe na kurudia katika hali yake ya awali.

Binadamu ameumbwa na vitu vitatu: Mwili (Body), Akili (Mind), na Ruhu/Nfsi (Spirit). Kila tatizo linalotokea katika ngazi ya mwili au akili, mara nyingi huwa lilianzia au lina mizizi yake katika ngazi ya kiroho na mfumo wa nguvu za uzima za mwili wako.

Siri kubwa ambayo wengi hawaijui ni kwamba sehemu hizi tatu zimeungana kama nyuzi za nguo moja—huwezi kuivuta moja bila nyingine kucheza.

Changamoto ya Tiba za Kisasa (Modern Medicine):
Tiba za kisasa mara nyingi zimegawa binadamu katika vipande vipande. Ukienda hospitali ya kawaida:

Wakiona shida kwenye Mwili, wanakupa dawa za kupunguza maumivu au kushikilia dalili (kama kupima damu au kukupa dawa za allergy).

Wakiona shida iko kwenye Akili, wanakutuma kwa wataalamu wa saikolojia.
Tatizo la mbinu hii ni kwamba inatibu dalili za nje (symptoms) na kuacha mizizi ya tatizo (root cause). Ndio maana vipimo vyako vya damu vinarudi vikiwa vizuri (normal), lakini bado unajisikia vibaya sana na mwili hauna nguvu.

Nini Kilichotokea Kwako?

Pamoja na kwamba upasuaji (operation) wa kidole tumbo uliokoa maisha yako kimwili, ulileta mshtuko mkubwa (trauma) katika pande zote tatu:

Kwenye Mwili (Body):
Mrija uliowekwa puani ulisisimua na kuumiza mfumo wako wa hewa na neva za puani, jambo lililofanya mwili wako kuwa na hypersensitivity (allergy) isiyoisha.
Mshono au chale ya upasuaji tumboni uliponya ngozi ya nje, lakini ndani kabisa uliacha kovu lililokata njia kuu za nguvu na stamina za mwili wako.

Kwenye Akili (Mind):
Siku ile uliyozimia wakati unafanya mazoezi, akili yako ya ndani (subconscious mind) ilipata hofu kubwa sana. Sasa hivi, kila unapojaribu kufanya mazoezi, kupanda ngazi, au kukimbia, akili yako inachukulia kama unataka kufa—hivyo inazima mifumo ya mwili (miguu kukosa nguvu, kizunguzungu, macho kuona weusi) ili kukulazimisha usimame na ujilinde.

Kwenye Roho na Nguvu ya Uzima (Spirit & Energy):
Upasuaji wa ghafla na maumivu makali uliotenganisha mshikamano wa nguvu zako za uzima (vital force). Ndio maana mwili unakosa msisimko wa asili wa nguvu pale unapoupa kazi nzito.

Hatua ya Kuchukua kabla ya Tiba:
Kupona kwako hakutokani na kumeza vidonge vya kuzuia mafua pekee au kupima damu tena. Kupona kwako kunahitaji Tiba Mchanganyiko (Holistic/Alchemical Approach) inayounganisha upya Mwili, Akili, na Roho.
Tutalazimika kufanya mambo matatu kwa pamoja:

Kimwili: Kutumia tiba za asili na mazoezi maalum ya mfumo wa neva ili kusaidia koo, pua, na eneo la tumbo kupona kabisa kuanzia ndani.

Kiakili: Kuifundisha upya akili yako kuwa mazoezi na kupumua kwa nguvu sio hatari, ili kuondoa ile hofu iliyojificha kwenye mfumo wa neva.

Kiroho/Kinguvu: Kurudisha uwiano na mshikamano wa nguvu za uzima (energy flow) zilizokatika wakati wa upasuaji, ili miguu na mwili upate stamina ya asili.
Usiogope, mwili wako haujaharibika—unahitaji tu kuelekezwa njia ya kujirudisha kwenye uumbaji wake wa awali."
 
Comment yako imenifungua upande mwingine mkuu 🙏 shukrani sana kwa elimu nzuri
 
Pole sana Mkuu. Nenda hata Hospitali ya Consolata Ikonda kwa ajili ya vipimo zaidi.
 
Ni kweli appendix huusika na kuboresha kinga ya mwili hasatumboni ila sioni uhusiano wa moja kwa moja na matatizo ya sasa, hasa kama surgery ilifanika kwa usahihi. Kwa uwelewa wangu naona tatizo liko kwenye upumuaji na kiasi cha oxygen kwenye damu hebu chunguza kwa kina kiwango cha red blood cells ambazo huusika na ubebaji wa oxygen mwilini hasa kipimo cha hemoglobin (Hb), oxygen saturation (SpO2) na upime mapafu na moyo haya ndio naona ni possible threats.
Kama unadalili nyingine kama maumivu nyuma ya mgongo hasa upande wa kulia usawa wa tumbo uweke wazi.
Ugua pole Young brother.
 

Kwenye upande wa maumivu kwenye mgongo ,hapana sina mkuu .

Shukrani sana kaka🙏
 
mafua hayo ndio kama mm nimezaliwa nayo kwetu mm na mshua tunasumbuliwa sana na hii hali ila mshua yeye ana pumu kabisa ila mm ni allegy tu vumbi kidogo tayari kitu kimeibuka kwa upande wangu niliamua situmii kabisa dawa zaidi ya kutafuna na kumumunya kipande cha tangawizi nakimumunya na kukaa nacho mdomoni huku nakitafuna kwa mbali kidogo kidogo na kumez mate yake nakaa nacho hata lisaa lizima mafua yanakoma pia jitahidi sana kuwa mtu wa kula machungwa inasaidia sana kupambana na mafua. kingine ukishajua hali hii jitahidi sana kukwepa vumbi hata geto ukiamua kufanya usafi funika pua mashuka tumia usizidishe siku 3-5 kulalia itakupunguzia sana kero za mafua.
 
Ahsante sana mkuu kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…