Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Anamaanisha nini huyu nae!!?
Ana maanisha vifijo na vigeregere vya wanaccm alipokuwa anawaburudisha kwenye majukwaa Zuchu akaamini ashakuwa bonge la MC(mwanamuziki) sasa alivyoandaa tamasha la shukrani ndio akaumbuka ,wadau wanasema show utafikiri ilikuwa ya Mboso na yeye alikuwa kama anarukaruka anafanya mazoezi ya jogging.
 
Mwanamke akimkosoa mwanamke mwenzie haimaanishi anamchukia.
Unataka amsifie tu kwasababu ni mwanamke mwenzie hata kama yeye ameona aneboronga?
Bora mtu atoe constructive criticism kuliko asifie tu ilimradi.
 
Nimetoka tena kumuangalia, aisee nani alimwambia aimbe live maana sauti inakwama kwama kama gari bovu,
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwanamke akimkosoa mwanamke mwenzie haimaanishi anamchukia.
Unataka amsifie tu kwasababu ni mwanamke mwenzie hata kama yeye ameona aneboronga?
Bora mtu atoe constructive criticism kuliko asifie tu ilimradi.
Wao kukosoa ni habits...hebu soma hyo comment unaona imejaa chuki tupu...na hii yote ni team.. huyo manzi hapo juu ni team kiba hakuna asie lijua. Sasa unafkr show ya zuchu atasifia?..ukosoe panapo kosoleka..panaposifika sifia..
 
Japokuwa jana sikuiona show ila kupitia comment hizi nimegumdua wanao iponda show ya Zuchu ni walewale wanaiponda WCB na Diamond humu JF kila siku,so bila shaka show ya jana ilikuwa nzuri.

Mwanzo mzuri dogo ana miezi minne kwenye game,anafanya vizuri kwenye digital platforms,jana amefanya show yake ya kwanza kubwa ktk venue kubwa,bila shaka ni kitu kizuri na kwa kupitia hizi clip YouTube naona show ilikuwa Nzuri na hata kama kuna makosa madogo madogo ana muda mwingi wa kujifunza kwani bado mchanga.

Kwa show ya jana mimi nampa 9/10.
 
Samahani yule mwanao ulie sema ana vaa heleni kama sh0ga. ana hali gani saivi
 
Tamasha la shukrani lilikuwa la bure lile, wageni wengi ni marafiki walialikwa labda kama walitoa kama zawadi.
Kiingilio ilikuwa kwa watu baki, wasioalikwa. Na kiwango cha juu ilikuwa 500k, kwa maana ya 5M meza ya watu 10 (shared!).

Kwa vyovyote vile, acha kuteseka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…