Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Chuki au katoa mtazamo wake mkuu??

Bro nimeshangaa sana kuonekana ni mwenye chuki ilhali nimeshasema namsapoti dogo.
Kuna watu bado wapo kwenye ule upuuzi wa uteam sijui nini ambao kwangu hivi sasa ni ushamba tu, mambo kama haya ndiyo yanayosababisha wengine tuwe watazamaji tu wa JF siku hizi.
You are missed
 
Wazee wa kuongeza zero nyuma wakiugua tu matangazo kila kona kuomba msaada maisha ya sanaa ya bongo yamejaa ulimbukeni na stress kibao ,ukimsikia v money alijiita v money akisema anazo leo analialia ndio utajua hizo billion 2 za huyo dogo
Ukitaka kupiga Hela za wabongo waandalie show tu
Utawatafuna mpaka basi

Ova
 
Chuchu kasainiwa kulipa fadhila kwa mama ake. Ukikaa karibubna domo lazima akulipe kwa namna fulani mfano gigy kuropoka kootee ni kujiweka karibu na wao wamemkubali,lokole etc

Ruby tatizo lake kiburi hata angekua muislam wasingemuweza
 
πŸ‘πŸ‘
 
Madam hakuna point ya kumwambia yote hayo. Kila mtu ana haki ya kutoa mtazamo juu ya chochote kile as long as havunji Sheria. Ni kitu Cha ajabu Sana mtu anapotoa post kisha anataka sote tukubaliane na mtazamo wake....huku ni kukosaa ufahamu sahihi.

Jana nilikuwepo kwenye show ya zuchu, binti Bado Sana ana hitaji kukuzwa zaidi. Huwezi kumlinganisha na wakina Nandi au Ruby kwa sauti Bado Sana.

Katika kutumbuiza naamini ni ugeni wa show kubwa Kama Ile na kwa kuwa yupo na lebel kubwa kibongo bongo ataendelea kujifunza na atakuwa mtumbuizaji mzuri ana jiamini Sana binti.
 

Asante
 
 
Hahaha wengi wanaoshabikia Huyo zuchu humu sijui hata Kama walienda ukumbini mlimani city. Wengine walikuwa kwao mikoani au wamekaa makwao wanasubiri clip za YouTube na Wasafi TV.


Narudia Tena kusema Tanzania haijawahi kupata msanii overrated kama zuchu. Zuchu ni msanii wa kawaida Sana Tena Sana Ila kwasababu ukiongea unaonekana hater ngoja tuone mwisho wake.

Ni sawa na harmonize alivyokuwa Wasafi tulisema humu kuwa ukimuondoa diamond Hakuna msanii mwingine pale wcb mwenye uwezo Kama Harmonize. Leo linaanza kuonekana hata diamond tungo zake za siku hizi zinaanza kuyumba maana moja ya watunzi wake wakubwa alikuwa harmonize.


Huyo zuchu mtu anaemuandikia nyimbo ni Mboso , Sasa fikiria angekuwa anaandika kila kitu yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…