Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Dah ..kwel adui wa wanawake ni wanawake wenyew [emoji16]

Hivi lini mtaanza kupendana ? Ile show we unaona ni yakiwaki? Tena mtu hana experience...Hebu madem mjifunze ku appreciate...Ile show zuchu kafanya poa sana...Mtu kafanya gestures zote, dancing..moves hadi kwa audience , comfortable still unasema hajatawala jukwa....? Uzur show ipo YouTube wala haiitaji hype..
Tofautisha kati ya ukweli na uadui kcamp . Sababu kitu kimefanywa na mwanamke sio lazima wanawake wote wakikubali haswa kinapokua na mapungufu.
Victoire ametoa maoni yake kama mwanamke anayejua MAANA na TOFAUTI kati ya USAWA na UWEZO kwenye mambo yahusuyo jinsia
 
Maelezo niliyoyaona kua wameuA tiketi za elfu 50 kwa watu elfu 2 ukipiga heaabu ni milioni 100 si haba.
 
Nakiri kukwambia HONGERA Sana kwa uchambuzi wako huo....daaah yaani ww dada sijui nikusifu vipi.....ur superpub and exquisite 👍👍👏👏

Much congrats to WCB...Zuchu is talented and amazing,wish her prosperity aaamen aaamen🤲🤲🤲

Ngojea niendelee kuinjoi show humu ndani same niliyoinjoi Jana...
 
Kwanza niwape pongezi Sana Wasafi namna walivyopamba ukumbi ulikuwa very nice na pia setting up ya jukwaa ilikuwa zuri Sana ikiwemo graphics zilizotumika on scene wakati msanii anaperfomance ilikuwa Ni fire Sana.WCB wanajua how to brand msanii na hii ndio tofauti yao na wasanii wengine I believe after hiyo show itapandisha value ya Zuchu Mara dufu.

Perfomance

Performance ya mboso dah was amazing kwa kweli amefanya wonders performance na ana deserve zile hela nyingi alizotuzwa.I think mbosso ndio msanii aliyetunzwa hela nyingi Sana.

Combination performance ya mboso & Zuchu

Moja Kati ya performance iliyonikosha kweli kweli nilipenda chemistry walionayo.

Combination ya Zuchu & Jide commando

Kumekuwa namsemo kwamba wanawake wanachukiana Sana lakini ushirikiano wa Jide na zuchu unaweza kutengeneza kitu kwenye Huu mziki.Walifanya something special as if Kama walikuwa na ngoma ya pamoja hapo kabla.Honestly nimependa Sana performance yao ya pamoja kiasi ambacho mashabiki wakataka warudie kuperform Mara 3.

Performance ya Zuchu

Kwanza kabisa ana confidence yake kaperform as if ana muda mrefu kwenye game I did like dress code yake ila nimependa zaidi performance ya wimbo wake wa "Nisamehe" nimependa alivyo calm na hisia kubwa aliyotumia Kama wimbo ulivyo, ukichanganya na voice yake ilivyo mzuri you get something good.Pia ametuonesha uwezo wake pia wa kudance huku aliimba kwa baadhi ya wimbo zake was amazing.

Combination ya mama yake na Zuchu

Waliua Sana aisee mama na mtoto.

performance ya Lavalava

Katika show zake zote za Lavalava hii ndio best show kuliko zote nilizowahi kuona kutoka kwake mzee aliua.


Ushauri wangu kwa baadhi ya udhaifu

Kuna watu wengi walibaki nje ambao walikosa tickets Wasafi wangejitahidi kuweka scene kubwa nje ya Ukumbi walau waone Nini kinajili ndani kuliko walivyowaacha.

La pili hili Ni moja Kati ya tatizo kubwa la watanzania wengi na nilichoona Jana watu kutokuja kwenye tukio kwenye muda uliopangwa watu hawapendi kuzingatia muda wasafi walipanga tukio nzima lianze saa 1 usiku Cha ajabu hata Diamond mwenyewe na Zuchu walikuja saa 2 usiku badala ya saa 1 usiku.
👏👏👏👏👏
 
Back
Top Bottom