Zuchu hana excuse kwa show mbovu ya jana. Amezaliwa na kulelewa na nguli wa performance Khadija Kopa, hata hajifunzi kwa mama yake? Miaka yote minne aliyosema alikuwa kwenye mafunzo huko usafini ndio utopolo gani ule?
Ieleweke nampenda sana mama yake, nimejikuta nampa sapoti sababu ya mama yake ila kaniangusha sana. Anapayuka kama yuko kilabuni ati anaperfom live na bendi!
Tazama mama yake aliposhika Mic, sawa uzoefu unachangia ila roho yangu ilisuuzika, she is the best. Ndiye pekee aliyeuchezesha ukumbi mzima bila kumsahau Jide huyu ni kiboko inafahamika, Mbosso na Dullah Makabila alinishangaza, anajua sana.