Threads 1,000 hazitoshi ku-prove ubaya wa Magufuli bali fact moja tu

Huu ujumbe unamhusu Tindo
 
Mkuu nimesema mtu au watu.... ? Au kwako hakuna tofauti ya kati ya mtu na watu...., Nimesema nchi inahitaji taasisi imara na sio kutegemea mtu...., Ofcourse inategemea watu imara na taasisi zinaendeshwa na watu na sio mtu.... ndio maana kuna separation of power kuna representatives ambao wanakutana na watu na kufanyia kazi mawazo ya watu..., ndio maana kuna wadau wa kuweza kufanya due dilligence na sio mtu kuamka tu na kuamua nini kifanyike bila kuwashirikisha watu...
 
Ni kawaida ya mtu anapopenda chongo huona kengeza
 
Mzee yule wacha apumzike kwa amani alihakiksha wale walio jilimbikizia mali kijanja janja wanakiona cha mtema kuni na kuacha wanyonge nao wapumue kidogo ndo maana machinga aliwatetea sana nao kidogo wafaidi ila sasa wale waliporudi wameanza na wanyonge zingua kila mahali ili waendeleee kujenga kijumba kwa bilioni tatu.
 
Machinga kidogo wafaidi nn?, unajua kwann wanaongezeka Kila siku. Vp kuhusu kampuni yake ya ujenzi aliyokuwa anaipa tenda za ujenzi, haikufata taratibu za rank za board ya maenguneer, napo alikuwa anabana mafisadi
 
So fact nini hapo?
 
Watu imara na taasisi imara kipi kinaanza?
 
Kwa umri wangu shida ya sukari nchini ikikwisha kati yamwaka 1985-90 na maduka ya RTC alipokuja AH Mwinyi, sijawahi kuisikia tena mpaka huyu Magufuli alipoivuruga.

Mwinyi ndiye aliyeleta trade liberalization, yaani aliruhusu Watanzania wenye uwezo kuagiza popote na kuja kuuza Tanzania.

Mwaka 1980-85 zilitawaliwa na uhaba wa kila kitu kuanzia sabuni, nguo, mchele nk. Hizi bidhaa zilikuwa zinapatikana kupitia RTC na maduka ya kaya Kwa foleni. BWM na JK hawakuvuruga mfumo wa biashara ulioanzishwana Mwinyi, instead waliuongeza nguvu.

Kwanini tulirudi kule kweusi alipokuja Magufuli?

Magufuli alikuwa MWEHU tu, never subscribe to his hate over rich people. Alikuta bei ya sukari ni Tsh 1,800 October 2015, akaivuruga hadi ikaruka Tsh 3,000-5,000 na hadi anakufa haikuwahi kuteremka. Kwanini aliwapa Manufacturers role ya trading?

Inawezekana vipi ukapata nafuu ya bei kwa kumpa Kilombero Sugar mwenye workforce ya wafanyakazi zaidi ya 5,000 na related overheads aagize Sukari?

Hiyo ndiyo jukumu la intermediaries ambao wana wafanyakazi wachache na overhead chache.

Alivyoharibu biashara ya korosho ndivyo alivyoharibu biashara ya sukari. Akiwachukia matajiri kwa UMASKINI wake lakini akatutengenezea shida hii.

Anachofanya Rais SSH ni ku "reboot" au "reset to factory settings", kama tunavyofanya simu ikisumbua au iki-jam.
 
Watu imara na taasisi imara kipi kinaanza?
Tusiamishe magoli ukiwa na watu Imara lazima Taasisi zitakuwa imara hata bila taasisi kama una watu Imara kila kitu kitakwenda ndio maana nikakuuliza unajua tofauti ya watu na mtu ? Mimi nilizungumzia hatuwezi kumtegemea mtu wewe umeleta watu katika conversation..., kuna sehemu nimesema tusitegemee watu ?
 
Hizo kanuni ndio zisubiri hadi wanyonge wafe wote kwa maumivu ya maisha magumu yasiyotabirika kesho yake?
Magufuli alikuwa kiongozi muhimu kwa wakati sahihi.
 
Hizo kanuni ndio zisubiri hadi wanyonge wafe wote kwa maumivu ya maisha magumu yasiyotabirika kesho yake?
Magufuli alikuwa kiongozi muhimu kwa wakati sahihi.
Ugumu wa maisha ulipungua wakati wa JPM ? Muendelezo wa Ugumu wa maisha umekuwa ukiendelea kabla wakati na baada ya JPM na hio ni sababu ya so called wanyonge kutegemea mtu kutatua matatizo yao (ofcourse wachache kula keki peke ya taifa peke yao haisaidii) lakini hakuna binadamu mmoja anayeweza kuwavusha watu peke yake...

Kiongozi anachofanya ni kuunganisha nguvu kuhamashisha na kuleta umoja ili watu wasonge mbele (jambo ambalo pia sidhani kama JPM alifanya ) Kuunganisha watu..., ingawa ofcourse kuna mambo alifanya kama mtendaji (lakini kama nilivyosema hapo mwanzo mtendaji sio necessarily kiongozi) Kiongozi anaongeza kwa kuwapa watu nguvu watende...
 
Shida mnakuwa general sana.
Umoja kwa maana ipi?
Tupe mikakati yako ungekuwa raisi hiyo ambayo ingetuvusha inayoeleweka bila kutumia ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…