Habari wakuu wa jukwaa hili la JamiiForums. Ni miezi kadhaa sasa tangu mradi wetu wa kimkakati wa Treni ya Kisasa (SGR) uanze kutoa huduma kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma. Wakati Watanzania wengi wakifurahia reli hii mpya, kuna changamoto kubwa sana inayoumiza kichwa na inayozua maswali mengi: Kero ya kuambiwa tiketi zimejaa kwenye mifumo, lakini treni ikiondoka mabehewa yanakuwa nusu tupu au robo tupu!
Jambo hili si la kawaida na limeanza kujenga hisia kali za dokezo la hujuma. Inasikitisha kuona mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya mtandao na hata yale madirisha ya vituoni yakionyesha "Seats Full" hata wiki moja kabla ya safari, lakini abiria wa ndani wanashuhudia viti vingi vikiwa wazi kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ruti. Hali hii inatufanya tuhoji kama kuna mchezo mchafu unaolenga kuhujumu shirika letu ili kurudisha abiria kwenye usafiri wa mabasi ya mikoani, au kama kuna mtandao wa watu wa ndani wanaotengeneza uhaba huu kwa makusudi.
Kibaya zaidi, uhaba huu wa mchongo umezidisha ugonjwa wa udalali na soko la nyuma (black market). Ukienda kihalali kwenye mifumo huwezi kupata tiketi, lakini ukiingia "chini ya kapeti" au ukitumia kujuana na baadhi ya watumishi, unapata tiketi kwa urahisi lakini kwa bei ya juu. Huu ni unyonyaji mkubwa kwa wananchi wa hali ya chini ambao walitegemea usafiri huu uwe mkombozi wao wa kiuchumi. Pia kumekuwa na malalamiko ya watu wanaotozwa faini kubwa wanapokosea majina huku wakitakiwa kutuma pesa hizo kwenye namba binafsi badala ya kupewa namba rasmi ya malipo (Control Number).
Kutokana na hali hii, tunaiomba TRC na vyombo vya uchunguzi kuingilia kati mara moja ili kuokoa mradi huu wa mabilioni ya walipa kodi. Kuna haja kubwa ya kuboresha mifumo ya TEHAMA ili viti vinavyobaki wazi vionekane kwa abiria wengine mara moja badala ya kuonekana vimejaa wakati wote. Vilevile, TRC lazima ifunge mifumo inayoruhusu watu kununua tiketi nyingi kwa mkupuo (bulk booking) bila kuunganisha tiketi hizo na Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Hii itasaidia kuzuia madalali kununua viti vyote na kuvishikilia kwa maslahi yao binafsi.
Wakuu, hili dokezo ni zito na linaleta maumivu makubwa kwa wananchi wanaokwama vituoni kila siku.
Au wamiliki wa mabasi wanahusika?
Hatuwezi kufumba macho na kuacha kuwanyooshea vidole baadhi ya wamiliki wa mabasi ya mikoani kwenye sakata hili la SGR. Tangu treni ya umeme ianze safari zake, matajiri hawa wamepata pigo kubwa la kiuchumi, huku wakilazimika kuegesha mabasi yao kwa sababu abiria wote wamekimbilia usafiri wa treni unaochukua saa 3 tu hadi Dodoma kwa nauli ileile ya basi. Je, inawezekana kuna "mchezo mchafu" uliosukwa chini ya kapeti ili kununua tiketi zote mtandaoni kupitia mawakala feki, lengo likiwa ni kutengeneza uhaba bandia ili kumlazimu mwananchi aliyekwama stesheni arudi Ubungo au Magufuli kutafuta basi?
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, aliwahi kukiri kuwa kuna fikra potofu kuwa reli inashindana na mabasi au malori, jambo linalopelekea watu wengine kuwa na nia ovu ya kuhujumu miundombinu au uendeshaji.
Wahusika chukueni hatua za haraka.