Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Timu ya uchunguzi wa matukio makubwa toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai toka Makao Makuu imetumwa kuongeza nguvu ili kuhakikisha waliofanya mauaji ya Ali Kibao Kada wa CHADEMA wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.Jana Septemba 7, 2024 Jeshi la Polisi lilitoa taarifa juu ya Ally Mohamed Kibao kuhusishwa kutoka kwenye basi la Tashrif na kuchukuliwa na watu ambao hawakuweza kutambuliwa na kwamba uchunguzi ulianza baada ya kupokelewa taarifa hiyo.
Baada ya kutolewa taarifa za kuonekana mwili wa mtu mwanaume ambaye hakuweza kutambuliwa kwa wakati huo ni mwili wa nani huko Ununio Jijini Dar es Salaam, utambulisho umefanyika kwa mujibu wa taratibu na kubainika ni mwili wa Ally Mohamed Kibao.
Soma Pia:
- Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
- Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ally Kibao
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha na timu ya uchunguzi wa matukio makubwa toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai toka Makao Makuu imetumwa kuongeza nguvu kwenye timu ya awali ili kuhakikisha waliofanya mauaji haya wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.