Tishio la Wakenya kuitaka ardhi yetu ni zaidi ya Wachina na wazungu

James Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,206
Reaction score
1,509
Wakenya ni majirani zetu na ndio nchi pekee duniani ambayo naweza kusema tunachangia vitu vingi sana. Kwa mfano, tunaongea lugha moja, chakula chetu kinafanana na kuna makabila mengi ambayo yapo Kenya na Tanzania.

Pamoja na ujirani wetu na mila na tamaduni kufanana lakini pia kuna tofauti kubwa sana baina yetu. Tofauti hizo ni kama Wakenya kuendekeza ukabila na uchu wa mali kupita kiasi.

Hoja kubwa ninayotaka kuijadili hapa ni kuhusu ardhi yetu.

Kenya kuna uhaba wa ardhi kutokana na ardhi kubwa kumilikiwa na matajiri wachache. Hali hiyo imepelekea Wakenya kuja kwa wingi Tanzania ili kutafuta fursa za kupata ardhi. Wakenya wanafanya hivyo kupitia mahusiano ya kimapenzi na dada na kaka zetu wa Kitanzania. Wakenya wanawarubuni ndugu zetu kimapenzi ili wapate urahisi wa kutumia ardhi yetu. Kitu cha kuogopa zaidi hawa watu wana rangi za ngozi na kuongea kama sisi kwahiyo ni vigumu kujua wameenea kwa kiasi gani (bila kutumia takwimu za uhamiaji) tofauti na wazungu.

Hivi ninavyoandika ndugu yangu ambaye ni wakili anamuwakilisha dada mmoja wa Kitanzania ambaye alirubuniwa kimapenzi na jamaa wa Kikenya na kuacha ardhi yake itumiwe lakini yule dada hapati chochote ilhali wameingia ubia kwenye mkataba wa uwekezaji. Kitu kinachonipa faraja ni kwamba ndugu yangu ananiambia licha ya kuwa anamuwakilisha mteja wake lakini hii kesi ni "personal " na atapigana kufa na kupona ili ashinde kesi! Ndugu yangu anafanya hivyo kwasababu anajua Wakenya hawana utu.
 
Ila watanzania tuwe makini sana. Kuna kaugonjwa fulani kanaingia kwa kasi mno. Tunahisi umasikini wetu uneletwa na watu wengine, tunaacha kupambana na maadui wa kweli wa maisha yetu tunalazimishwa kuamini kuwa mara tunaonewa, mara watu wa nje wanatamani vitu vyetu, mara mabeberu tupo nao kwenye vita nk. Hawa si maadui zetu, adui zetu ni ujinga, uzembe, siasa za hovyo na IQ pungufu.

Mleta mada una mifano mingapi ya wakenya waliowahulumu wadada wa kitanzania? Una mifano mingapi ya wakaka wa kitanzania waliowadhulumu ndugu zao wa damu ardhi?

Ishu ni kujitambua tu mkuu. Watanzania tufike mahali tujitambue, hii ya kuwaza wakenya wanataka ardhi yetu mara mabeberu wanataka utajiri wetu haitatufikisha popote. Tusimame tupambane
 
Si bora hao wakenya waje tu ili wanunue hiyo ardhi maana haina faida yoyote kwa watu wengi wanaoimiliki. Nenda huko vijijini utakuta mtu anamiliki sio chini ya heka tano, lakini ni masikini wa kutupwa. Mtu wa hivyo si bora amuuzie huyo mkenya apate mtaji wa kufanyia biashara?
 
Watz bado mna hangover za ujamaa
Watz bado mna hangover za ujamaa
Aiseee, yaani kama sie kwa ardhi kubwa tumeshindwa kuitumia na kuleta tija na kuinua maisha yetu, ni heri waje wachukue sehemu na kuitumia kuleta maendeleo ya jamii na kiuchumi, badala ya blabla za siasa za ujamaa tulizozisikia kwa miaka 60....
 
Unaogopa nini wakati hiyo ardhi itatolewa kwa mkataba kisheria?
 
Wakenya ni majirani zetu na ndio nchi pekee duniani ambayo naweza kusema tunachangia vitu vingi sana. Kwa mfano, tunaongea lugha moja, chakula chetu kinafanana na kuna makabila mengi ambayo yapo Kenya na Tanzania.

Pamoja na ujirani wetu na mila na tamaduni kufanana lakini pia kuna tofauti kubwa sana baina yetu. Tofauti hizo ni kama Wakenya kuendekeza ukabila na uchu wa mali kupita kiasi.

Hoja kubwa ninayotaka kuijadili hapa ni kuhusu ardhi yetu.

Kenya kuna uhaba wa ardhi kutokana na ardhi kubwa kumilikiwa na matajiri wachache. Hali hiyo imepelekea Wakenya kuja kwa wingi Tanzania ili kutafuta fursa za kupata ardhi. Wakenya wanafanya hivyo kupitia mahusiano ya kimapenzi na dada na kaka zetu wa Kitanzania. Wakenya wanawarubuni ndugu zetu kimapenzi ili wapate urahisi wa kutumia ardhi yetu. Kitu cha kuogopa zaidi hawa watu wana rangi za ngozi na kuongea kama sisi kwahiyo ni vigumu kujua wameenea kwa kiasi gani (bila kutumia takwimu za uhamiaji) tofauti na wazungu.

Hivi ninavyoandika ndugu yangu ambaye ni wakili anamuwakilisha dada mmoja wa Kitanzania ambaye alirubuniwa kimapenzi na jamaa wa Kikenya na kuacha ardhi yake itumiwe lakini yule dada hapati chochote ilhali wameingia ubia kwenye mkataba wa uwekezaji. Kitu kinachonipa faraja ni kwamba ndugu yangu ananiambia licha ya kuwa anamuwakilisha mteja wake lakini hii kesi ni "personal " na atapigana kufa na kupona ili ashinde kesi! Ndugu yangu anafanya hivyo kwasababu anajua Wakenya hawana utu.
Sipingi wala silaumu haya mambo yetu na waKenya. Imekuwa kama waTanzania hatuna akili kabisa za kujisimamia, sijui kwa nini!

Hebu nami niulize swali.

Hivi huko Kenya hakuna kitu/vitu tunavyoweza hata sisi kwenda kuwatia jamba jamba navyo? Inachosha sana kusikia hizi habari za Kenya hiki, Kenya kile kila siku hapa Jukwani.

Mimi napendekeza siku moja nasi tufanye kitu ili na wao wakenya walielie angalau kidogo. Hivi itakuwaje tukienda kuwavamia ili tuwatawale kwa lengo la kuwasaidia waje kutumia ardhi na mali zetu nyingine hapa hapa kwetu?

Huenda niliyoandika hapa yasieleweke; naomba tu nisilaumiwe kwayo kwa maana hii Kenya sasa imekuwa kama ni dawa ya kulevya vichwani mwa waTanzania.

Nikitaka kuandika kwa umakini juu ya swala hili, nitaanza na lawama kwa huyo ndugu yako ambaye kazidiwa ujanja na huyo mkenya wake.

Matatizo yetu yote yanaanzia huko kwa watu kama hao. Vinginevyo, wakenya si lolote kwetu.
 
Si bora hao wakenya waje tu ili wanunue hiyo ardhi maana haina faida yoyote kwa watu wengi wanaoimiliki. Nenda huko vijijini utakuta mtu anamiliki sio chini ya heka tano, lakini ni masikini wa kutupwa. Mtu wa hivyo si bora amuuzie huyo mkenya apate mtaji wa kufanyia biashara?
Mtanzania anyetaka kuwa machinga Hana muda wa kuwaza aridhi ya kijijini
 
Kwani aanaitumia kinyume cha sheria ?au hawalipi kodi ?wew uloeshika ardh unaifanyia nin?
 
Kumbe ni Mkenya mmoja tu!, Heading yako iliniogopesha kidogo. Nilifikiri Wakenya wamevamia kama Iddi Amini alivyofanya kuteka Kijii kule Bukoba.

Halafu mbona Sheria zetu haziruhusu Mgeni kumiliki ardhi?.
Hii naiona ni kesi nyepesi.
 
Uzuri wa haya yote ni huu: Tanzania daima itabaki kuwa Tanzania, hata kama wakenya wote wakiamua kuhamia hapa na kuiacha nchi yao huko.

Waje tubanane hapa. Wakishakuwa wengi na kuanza kututawala, bado nchi itajulikana kama Tanzania, nasi wapuuzi tukiendelea kuwemo humo humo ndani ya Tanzania hiyo mpya ya watawala toka Kenya.

Lakini nadhani kuna kitu kinatusumbua sisi waTanzania. Mbona waganda, waethiopia, wasomali na wasudan wa kusini hawalii lii kama sisi kuhusu wakenya?

Kwanza hakuna mkenya anayethubutu kwenda kuvamia Ethiopia au Somalia. Ulishasikia wakitamani kwenda huko?

Walijaribu Sudan Kusini wakakuta moto, wakakimbia haraka; Tanzania ndiko wanakotingisha kila mara, na hasa sasa baada ya kufunguliwa mpaka ndipo tutajionea mengi ya ajabu.
 
Huko nchi nyingine ardhi hakuna wakachukue nini ?
 
Ardhi ya Tanzania ni mali ya Rais.

Unaweza kufanya mbwembwe zote kama mhamiaji ila siku wakiitaka wanaichukua na hata wewe wanaweza kukuchukua ukaozea mahabusu na hutakuwa na kitu cha kufanya.
👍
 
Back
Top Bottom