Wakenya ni majirani zetu na ndio nchi pekee duniani ambayo naweza kusema tunachangia vitu vingi sana. Kwa mfano, tunaongea lugha moja, chakula chetu kinafanana na kuna makabila mengi ambayo yapo Kenya na Tanzania.
Pamoja na ujirani wetu na mila na tamaduni kufanana lakini pia kuna tofauti kubwa sana baina yetu. Tofauti hizo ni kama Wakenya kuendekeza ukabila na uchu wa mali kupita kiasi.
Hoja kubwa ninayotaka kuijadili hapa ni kuhusu ardhi yetu.
Kenya kuna uhaba wa ardhi kutokana na ardhi kubwa kumilikiwa na matajiri wachache. Hali hiyo imepelekea Wakenya kuja kwa wingi Tanzania ili kutafuta fursa za kupata ardhi. Wakenya wanafanya hivyo kupitia mahusiano ya kimapenzi na dada na kaka zetu wa Kitanzania. Wakenya wanawarubuni ndugu zetu kimapenzi ili wapate urahisi wa kutumia ardhi yetu. Kitu cha kuogopa zaidi hawa watu wana rangi za ngozi na kuongea kama sisi kwahiyo ni vigumu kujua wameenea kwa kiasi gani (bila kutumia takwimu za uhamiaji) tofauti na wazungu.
Hivi ninavyoandika ndugu yangu ambaye ni wakili anamuwakilisha dada mmoja wa Kitanzania ambaye alirubuniwa kimapenzi na jamaa wa Kikenya na kuacha ardhi yake itumiwe lakini yule dada hapati chochote ilhali wameingia ubia kwenye mkataba wa uwekezaji. Kitu kinachonipa faraja ni kwamba ndugu yangu ananiambia licha ya kuwa anamuwakilisha mteja wake lakini hii kesi ni "personal " na atapigana kufa na kupona ili ashinde kesi! Ndugu yangu anafanya hivyo kwasababu anajua Wakenya hawana utu.
Tuwe wakweli tunahitaji nguvu kazi ya kutosha kujenga Tanzania yetu nikimaanisha nguvu za watu kujidanganya eti tuzaane ndipo tupate nguvu kazi ya kutosha ni ujima,ubaguzi wa hata na majirani zetu ,ni wa kiwango Cha juu.lengo la jumuia ya afrika mashariki ni kujenga nchi kubwa ya uchumi mkubwa .lengo hilo liliasisiwa mwishoni mwa miaka ya 1950 ,Leo hii mtu anajitokeza na kuogopa wakenya pole yake. ubaguzi hujawahi kuleta maendeleo, afrika ya kusini ilishamiri kwa ubaguzi iakatengwa pamoja na maendeleo waliyo kua nayo walikwama wakasalimu amri,wakakubali kuwathamini watu wote taifa lisilo lakibaguzi likaunuka na kua taifa la uchumi imara.kwa kua ilikubaliwa kushirikiana na nchi nyingine
Taifa linalo ongoza kwa uchumi duniani ni Marekani , taifa la mchanganyiko wa mataifa karibu yote duniani
Sisi tuna rasilimali za kutosha, lakini uchumi wetu ni wa kipato Cha Kati Cha nchini wakenya uchumi wao ni wa Kati wa juu, ni kwa kua Wana maarifa na mbayo tunayahitati mbinu wanazo tatua changamoto huenda zikatusaidia
Hebu fanya utafiti mdogo mijini Kuna maendeleo unajua ni kwa Nini,ni kwakua Kuna mchanganyiko wa makabila . na mikoa yenye makabila mengi Toka sehemu tofauti zinapiga hatua.
Hivi Sasa Canada inabembeleza wahamiaji imegundua Siri ya urembo na sisi wakijilengesha Kuna kosa gani .
kwanza wameoa au kuolewa unadhani watarudi kwao labda Sio Tanzania nakutabiria siku wakikubali uraia pacha mitaji italetwa na wageni kutafuta ulowezi
Pia tujifunze historia sisi tunaojiita watanzania ni miaka ya 1844 ndipo afrika ikagawanyika haijafika hata miaka 200
sisi wasukuma historia Ina sema tulitokea Uganda kwenye Dora la buchwezi ndio maana utakuta tamaduni za kichwezi tukiwatuhumu waganda ni kutokujua chimbuko letu wadigo wasambaa wamasai wamburu wachaga nk ni makabila yaliyotokea Kenya wayao wamakua wamwela nk walitokea msumbiji Vivyo hivyo wamanda wanyakyusa baadhi Yao walitokea Malawi na Zambia Kuna watanzania asiri Yao ,na Kongo Burundi Rwanda Uganda Hadi sudani (wajaluo)
Najalibu kuonesha jinsi tulivyo kua tunatoka sehemu mbali mbali na hata Sasa Kama watu wanakuja na kuoleana huo ni mpango wa MUNGU
Mbona hujahoji watu waliokuja na kugoma kuoleana nasi vipi hao wao unawachukuliaje poa tu,na inawezekana ndo wenye ukwasi mkubwa
Kubali falsafa ya marasta afrika moja isiyo na mipaka ndiyo ita kayo kua na maendereo