TISS, PSU Jifunzeni kwa walioendelea

TISS, PSU Jifunzeni kwa walioendelea

Jana kaja Kamala wote tumeshuhudia Ulinzi imara usio na maonesho. Maonesho yenu ya kubeba mibunduki hadharani hayajaonekana jana. Siku zingine mnazingira Rais kama ni gaidi...
Daima ukosoaji ni kazi rahisi sana ambayo hata mtu dhaifu anaweza kuifanya.pia ww kutokuona kazi/umuhimu wa wale unaowaita "Vidada" haimaanishi huo umuhimu haupo ni vile tu either hujui ila unataka kuonekana mjuaji au ni vile tu hujui alafu hujui kama hujui. ACHENI UJUVI MWINGI MNAHISI MNA AKILI NYINGI KULIKO TAASISI AMBAZO ZIMEWEZA KUSIMAMA KUANZIA WW HAUJAJUA KUANDIKA MPAKA LEO UMEKUA KEYBOARD WORRIOR.

Sent from my SM-G960N using JamiiForums mobile app
 
Heshimu Taasisi na Utaratibu wa Taasisi sawa? Siyo lazima kila lifanywalo na CIA / NSA (Marekani ) basi na TISS ( Tanzania ) nao walifanye au waliige.

Binafsi ( GENTAMYCINE ) nimebahatika Kukaa ( kuwa karibu ) na Walinzi wa baadhi ya Marais wa Ukanda wetu huu ( Kale Kayihura aliyekuwa CIG: wa Uganda ila kabla alikuwa Mlmoja wa Walinzi PPU wa Rais Museveni na Marehemu Noble Mayombo aliyekuwa CMI wa Uganda na aliyewahi pia kuwa ADC wa Rais Museveni ) achilia mbali wa Rais Kagame na wa Hayati Mzee Kabila ( Laureant Kabila ) na Sifa pekee niliyoisikia kutoka Kwao kuhusu TISS na hasa hasa PSU ni kwamba wako vizuri na Wameiva mno Kimedani.

PSU ndiyo blueprint ya Vikosi vingi vya Ulinzi wa Marais katika nchi nyingi za Ukanda huu ikiwemo na Msumbiji na nyinginezo.

Acheni Kudharau vya Kwenu TZ Oky?
Kumbe maneno ya kuambiwa. Hakuna lolote. Wapo busy kwenye inbox za wadada wanatuma picha zao wakiwa safarini na suti. Ndio maana hawaaminiki. Nchi unazotaja ni utopolo tupu.
 
Jana kaja Kamala wote tumeshuhudia Ulinzi imara usio na maonesho. Maonesho yenu ya kubeba mibunduki hadharani hayajaonekana jana. Siku zingine mnazingira Rais kama ni gaidi.

Hata yule mpambe anayevaa magwanda sioni umuhimu wake zaidi ya matumizimabaya ya kodi. Vile vidada vinavyokaa pembeni ya Rais akiwa anahutubia jana havijaonekana popote pale.

Jifunzeni bana
Mmekariri sana

Nendeni pale Hyatt Regency muone gari zinavyosachiwa haijalishi ni ya wapi, hawana cha yule ni mwenzetu, ukifika pale unasachiwa na MBWA afu waruhusiwa pita.

TISS ivunjwe maana imeshindwa msaidia Rais kazi
Hawawezi jifunza baba, hawataki, kisa Ulaji, kuna mtu anapiga hela kutokana na hayo, misafara mikubwa, kuzingirwa na upuuzi gani sijuwi...wanajifanya wana BLANK CHQ kumbe UFUSADI TU
 
Ivi kumbe kamala alilala hyatt nilikuwa najiuliz leo baada ya kupita pale hyatt kwamba mwanama MMA Kamala atakuwa amelala wapi jana ikulu mmmh nikasema hapana maaana hata mama mwenyewe halalagi kule
Unapoona hotel ina vyumba Presidential suite ndio kazi yake hiyo.
 
Kuwepo kwa ulinzi imara sehemu hakuhitaji bango getini la " Hatari mbwa mkali" .... Wajifunze ndio!!. 👍
 
Wote ni mashahidi wale mabaka mabaka, wale wadada wanaokaa pande mbili za Rais hawakuwepo jana nyuma ya Rais

Tujaribu kujifunza wao wanawezaje kumlinda Rais wao bila kukera watu, sasa TV inakuwa unaangalia hata watu wasiohusika wakati anayetakiwa onekana ni Rais pekee.
Mswahili fahari yake ni kumtisha mwezake. Mswahili anafarijika sana akiona mswahili mwenzake anapata hofu na kukosa amani kwa ajili yake
 
Msafara mrefu inamaanisha watu wengi zaidi wanapata ulaji wa posho humo, marafiki na washikaji zao.
Kingine PSU iweje wakubali Rais kutembea na msafara mrefu?
Rais wa Marekani msafara wake sio mrefu kama wa Rais wa nchi omba omba
 
Sijawahi kuelewa sababu za Marais au viongozi wakuuu wa Africa kuwa na mwanajeshi/mlinzi anayesimama nyuma yao kila mahali. Hata ndani ya Ikulu mahali ambapo pangetegemewa kuwa mahali salama zaidi unakuta huyo mwanajeshi anasimama nyuma ya Rais wakati anahutubia au kusalimiana na watu!
White House huwa namuona Biden amejiachia tu ana mingle na raia bila watu wa usalama kumfuatafuata!
Wote ni mashahidi wale mabaka mabaka, wale wadada wanaokaa pande mbili za Rais hawakuwepo jana nyuma ya Rais

Tujaribu kujifunza wao wanawezaje kumlinda Rais wao bila kukera watu, sasa TV inakuwa unaangalia hata watu wasiohusika wakati anayetakiwa onekana ni Rais pekee.
 
Kumbe maneno ya kuambiwa. Hakuna lolote. Wapo busy kwenye inbox za wadada wanatuma picha zao wakiwa safarini na suti. Ndio maana hawaaminiki. Nchi unazotaja ni utopolo tupu.
Yaani wale PSU wakishaonekana kwenye TV, wakipewa off wanasumbua sana watu, wanatapeli watu kuwa tuko karibu na Rais tunaweza fikisha shida yako
 
Sijawahi kuelewa sababu za Marais au viongozi wakuuu wa Africa kuwa na mwanajeshi/mlinzi anayesimama nyuma yao kila mahali. Hata ndani ya Ikulu mahali ambapo pangetegemewa kuwa mahali salama zaidi unakuta huyo mwanajeshi anasimama nyuma ya Rais wakati anahutubia au kusalimiana na watu!
White House huwa namuona Biden amejiachia tu ana mingle na raia bila watu wa usalama kumfuatafuata!
Hicho ndo nakishangaa kama wanachagua marais wagonjwa waseme.

Napenda sana nchi yetu iende mbele zaidi, ila ili iende mbele inabidi kwanza hawa TISS washughulikiwe, walioingia bila merits wapelekwe kwingine kulingana na elimu zao
 
Back
Top Bottom