Tetesi: Tito Magoti kutengenezewa kesi ya Utakatishaji pesa au Uhujumu uchumi

Tetesi: Tito Magoti kutengenezewa kesi ya Utakatishaji pesa au Uhujumu uchumi

Na nyinyi mnafunzwa na nani! maana hamna tofauti yoyote ile na mashetani. Mnalazimishwa kupendwa na kuheshimiwa wakati stahili yenu pekee ni kudharauliwa, kutukanwa, kukejeliwa na kupuuzwa tu.

Mnafanya mambo ya kitoto, kishamba na kilimbukeni halafu mtegemee kuheshimiwa! Daima ataogopwa Mungu pekee na siyo mwanadamu ambaye ni udongo tu.

Hamna ubavu wa kuwanyamazisha wananchi wote, upinzani/kukosolewa ni kama mvua! Huwezi kuizuia kunyesha.
Wafuate Gerezani ukawaone walivyonyong'onyeya!
 
Yupo kwenye mikono salama na watanzania siku hizi wanavunja sheria za nchi kisa haki za binadamu. Tunatakiwa kutii katiba yetu na sheria za nchi pia uhuru una mipaka yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo wanaovunja katiba mchana kweupe lkn unafiki hauwezi ukawaacha muone, hata akina Gaddafi waiondoka, wakati ukuta.
 
Yale yale ya Kabendera yanajirudia tena , hasa baada ya misheni ya kumteka kushtukiwa na kupigiwa kelele na wadau dunia nzima , sasa anaandaliwa mashitaka ya uzushi ili kumkomoa .

Taarifa zinadokeza kwamba hapa ndipo kigugumizi cha Mambosasa kinapoanzia , pamoja na ukweli wote wa njama hizi kuvuja lakini bado wanataka kutekeleza mpango wao , wananchi endeleeni kupiga kelele maana dunia yote iko nyuma yenu.

Shetani hajawahi kumshinda Mungu

UPDATES
..................


View attachment 1302314
Nashauri waandisho wa habari wote nchini wafunguliwe mashtaka kama haya
 
Kama ametakatisha pesa sisi tunaachia wenye mamlaka

Sent using Jamii Forums mobile app

Hoja siyo kutakatisha au kutotakatisha fedha haramu. Tatizo kubwa ni kwamba mtuhumiwa huadhibiwa mara mbili; kabla na baada ya kupatikana na hatia. Hata akishinda kesi tayari ameshaadhibiwa ikizingatiwa kuwa hata upelelezi wa kesi kama hizo huwa haukamiliki. Vinginevyo mtuhumiwa anunue uhuru wake kwa kuingia makubaliano na dpp!
 
Safi sana! Sasa ni kazi yake kuithibitishia mahakama kuwa hana hatia ama la!

Hapana! Upande wa mashtaka ndiyo mwenye dhamana ya kuthibitishia mahakama kuwa mtuhumiwa anayo hatia. Mara nyingi wanashindwa kufanya hivyo ndiyo maana upelelezi wa kesi hizo haukamiliki na watuhumiwa kutakiwa kukiri kosa na kununua uhuru wao!
 
Lazima ifike pahala tukubali kuwa kumtukana aliye madarakani hata kama humpendi ni kama kuweka roho yako rehani. Kwanini utukane acha wapate kiboko chao! Povu ruksa

Wanastahili kufunguliwa mashtaka yanayoakisi kosa la kutukana; kama lipo kwenye sheria. Tatizo ni pale wanapotungiwa makosa mengine; tena makubwa yasiyokuwa na dhamana!
 
Achana na kukariri, katiba ipi inaruhusu kutukana ovyo, ulimbukeni wa kuanza kutumia smartphones kunawazuzua akina Tito, kiboko yake unaiona na bado sijui hata marinda- naishia hapo
Mbona na nyie mnawatukana wapinzani na hamkamatwi? Au ndio vile Mkuki mtamu kwa nguruwe ila mchungu kwa binadamu! Sawa bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom