James Hadley Chase
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 1,984
- 3,695
Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa, Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.
Kwa kupitia taarifa yao waliyoitoa mapema leo, Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile pamoja na Wakili Cosmas Kishamawe wamesema kwa kushirikiana na mawakili wengine wa mkoani Iringa tayari wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane huyo.
Mawakili hao wamesema tayari mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa umeanza rasmi leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kutoa msaada wa ushauri na utetezi wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii yasio na uwezo.
Ambindwile alisema tangu waanzishe mpango wa kutoa msaada wa ushauri wa kisheria mkoani Iringa, wameendelea kupokea maombi kutoka kwa makundi ya watu wasio na uwezo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.
“Tuishukuru sana kampuni ya Asas kwa ahadi yake iliyotolewa na mmoja wa wakurugenzi wake, Ahmed Asas kwa kujitokeza kushirikiana nasi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wasio na uwezo hususani wale waishio vijijini,” alisema.