Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli. Mbaya zaidi hapa ni sheria iliyotumika kutoa hukumu.Ni sawa, ila hili ni kati ya jambo la kipumbavu kuliko yote, Ametumia sheria halali ya Tanzania kumfunga, swali: baada ya kumsaidia, Je hakuna sababu ya kuangaliwa sheria iliyomfunga?
Mbona kaeleza kabisa nyama kaitoa kwa nani.......fuatilia vizuri hiyo kesi mkuu, kuna shida sehemu.we tuambie hiyo nyama ameitoa wapi km siyo wamemwua huyo mnyama? Hao watu mnaowaita wanyonge ni kwamba hawajakufikia tu, ni makatili yenye roho ngumu. Acheni sheria ichukue mkondo wake, huyo jaji aliyemhukumu naye ana roho na moyo km sisi tuache unafiki
Pumbavu sana majitu yanashindilia twiga wazima kwenye ndege halafu yanapewa na bandari kwa shangwe halafu mama ambaye hana hata manati ya kuua panya anafungwa 22 yrs kwa vipande vya nyama! Mahakimu mlaaniwe kwa hili.Dege la kupeleka nyama nje
Huyu jamaa ni msengeee, nataman nipate orodha za Hukumu zake .
Wakishapewa rushwa wanakuwa wanyama.Kweli. Mbaya zaidi hapa ni sheria iliyotumika kutoa hukumu.
Lakini hakimu/judge wamepewa nafasi ya kutizama vigezo vingi kabla ya kutoa hukumu. Hapa inaonekana hiyo nafasi haikutumika kabisa.
CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa wameanzisha kampeni ya kumsaidia kisheria mjane Maria Emirio Ngoda aliyehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Iringa kifungo cha miaka 22 kwa kosa la kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.![]()
Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa, Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.
![]()
Kwa kupitia taarifa yao waliyoitoa mapema leo, Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile pamoja na Wakili Cosmas Kishamawe wamesema kwa kushirikiana na mawakili wengine wa mkoani Iringa tayari wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane huyo.
Mawakili hao wamesema tayari mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa umeanza rasmi leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kutoa msaada wa ushauri na utetezi wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii yasio na uwezo.
Ambindwile alisema tangu waanzishe mpango wa kutoa msaada wa ushauri wa kisheria mkoani Iringa, wameendelea kupokea maombi kutoka kwa makundi ya watu wasio na uwezo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.
“Tuishukuru sana kampuni ya Asas kwa ahadi yake iliyotolewa na mmoja wa wakurugenzi wake, Ahmed Asas kwa kujitokeza kushirikiana nasi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wasio na uwezo hususani wale waishio vijijini,” alisema.
Kama sijaelewa, ndoo moja ya nyama ya swala inathamani ya 900,000/= Mbona hiyo nyama ni agali Sanaa? au wamepiga bei ya kumuua Swala sio bei halisi ya nyama? Nijuavyo laki 9 Ni Ngombe mzima na usheeCHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa wameanzisha kampeni ya kumsaidia kisheria mjane Maria Emirio Ngoda aliyehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Iringa kifungo cha miaka 22 kwa kosa la kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.![]()
Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa, Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.
![]()
Kwa kupitia taarifa yao waliyoitoa mapema leo, Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile pamoja na Wakili Cosmas Kishamawe wamesema kwa kushirikiana na mawakili wengine wa mkoani Iringa tayari wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane huyo.
Mawakili hao wamesema tayari mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa umeanza rasmi leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kutoa msaada wa ushauri na utetezi wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii yasio na uwezo.
Ambindwile alisema tangu waanzishe mpango wa kutoa msaada wa ushauri wa kisheria mkoani Iringa, wameendelea kupokea maombi kutoka kwa makundi ya watu wasio na uwezo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.
“Tuishukuru sana kampuni ya Asas kwa ahadi yake iliyotolewa na mmoja wa wakurugenzi wake, Ahmed Asas kwa kujitokeza kushirikiana nasi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wasio na uwezo hususani wale waishio vijijini,” alisema.
Mbona mbu mnaua kwa kupulizia dawa kwani hao sio viumbe?acha unafiki, hata mnyama aliyeuawa ana haki ya kuishi, tii sheria bila shuruti. Watanzania ni wanafiki sana ndio maana ni ngumu kupiga hatua.
Kwa matusi tu hapa JF sidhani kama una mpinzani. Kwani ukitoa hoja yako bila kuporomosha matusi utapungukiwa na nini? Sad!we zuzu katafute nchi isiyo na sheria. Kenge tu unajifanya una huruma? Mnafiki mkubwa watu km hao wanashirikiana na majambazi, amewezaje kumwua huyo mnyama km kweli ye ni mnyonge? Acheni upuuzi hata huyo mnyama aliyeuliwa ana haki ya kuishi.
Kama ulifuatilia hii kesi ...ni kwamba alikuja MTU akamwachia ndoo na kumwambia narudi muda si mrefu ..Nyuma ya hiyo kesi naamini kuna mwenye pesa alitaka viwanja vya huyo mama akiamini atauza baada ya hukumu na hakimu alikula rushwa ili amtishe mama ila akakuta mama bora nifungwe kuliko kuuza mali zangu.
Nawaza tu
Kibatala nasikia kawatafuta ndugu zake ili awasaidie kwenye kukata rufaa lakini inasemekana wamegoma kumpa ushirikiano, waweza kukuta wameingiza siasa mwenzao kapigwa mvua 22Mwenyezi Mungu awasaidie na kuwapa wepesi, ningekua na uwezo hakika ningekua miongoni mwao watakao support lakini nawaombea.
Rosti tamu mwenyewe alisema kuwa mahakama hazina ishu Ni mapambo Mana mtu anapiga simu anasema hukumu hivi Basi kwishneiHakimu kathibitisha kua sheria ni kwa ajili ya makapuku tu. Yule mdogo wake Rosti Tamu alikamatwa na silaha kabisa za kuwindia hayo mazaga lakini kesi yake iliisha kimazabe mazabe