TLS kumsaidia aliyefungwa Miaka 22 kisa nyama ya Swala

Nyuma ya hiyo kesi naamini kuna mwenye pesa alitaka viwanja vya huyo mama akiamini atauza baada ya hukumu na hakimu alikula rushwa ili amtishe mama ila akakuta mama bora nifungwe kuliko kuuza mali zangu.

Nawaza tu
You have a point. Kuna yaliyojificha nyuma ya pazia. Haiwezekani hakimu akatoa adhabu kali kwa mama ambaye ana watoto na kosa lenyewe siyo kubwa. Angepewa onyo tu na kuachiwa. Wewe hakimu uliyefanya haya Mungu anakuona wewe na kizazi chako. Ahsanteni TLS.
 
Maria alikua kachanganyikiwa kwa hiyo hukumu ila walioumia pia ni hao Manjagu ukiona unaona kabisa wanafikiria hukumu ya Maria uzuri naamini atatoka hata Mama mwenye nyumba ataingilia kati kwa kumpa msamaha ngoja niendelee kumuombea tu Maria atoke aendelee kulea familia yake maisha yana changamoto sana.
 
Maria alikua kachanganyikiwa kwa hiyo hukumu ila walioumia pia ni hao Manjagu ukiona unaona kabisa wanafikiria hukumu ya Maria uzuri naamini atatoka hata Mama mwenye nyumba ataingilia kati kwa kumpa msamaha ngoja niendelee kumuombea tu Maria atoke aendelee kulea familia yake maisha yana changamoto sana...
Ukiangalia picha tu hao manjagu wanamsikitikia

Sema mkuu kesi zina stress sana

Ova
 
28aeada3704aff46b4aab83218d33adc
CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa wameanzisha kampeni ya kumsaidia kisheria mjane Maria Emirio Ngoda aliyehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Iringa kifungo cha miaka 22 kwa kosa la kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa, Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.

17ab033562d668ed4cafa45cc0e59e27

Kwa kupitia taarifa yao waliyoitoa mapema leo, Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile pamoja na Wakili Cosmas Kishamawe wamesema kwa kushirikiana na mawakili wengine wa mkoani Iringa tayari wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane huyo.

Mawakili hao wamesema tayari mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa umeanza rasmi leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kutoa msaada wa ushauri na utetezi wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii yasio na uwezo.

Ambindwile alisema tangu waanzishe mpango wa kutoa msaada wa ushauri wa kisheria mkoani Iringa, wameendelea kupokea maombi kutoka kwa makundi ya watu wasio na uwezo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.

“Tuishukuru sana kampuni ya Asas kwa ahadi yake iliyotolewa na mmoja wa wakurugenzi wake, Ahmed Asas kwa kujitokeza kushirikiana nasi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wasio na uwezo hususani wale waishio vijijini,” alisema.
Katika vitu vilivyoharibu siku yangu ni siku nilipoona hii picha na kusoma eti amefungwa miaka 22 kwa kukutwa na viapnde vya nyama ya swala. Hivi huyo hakimu ni binadamu au mbwa? Hata kuna kuna sheria lakini wakati mwingine hakimu unatakiwa kutumia akili zako.
 
Nyuma ya hiyo kesi naamini kuna mwenye pesa alitaka viwanja vya huyo mama akiamini atauza baada ya hukumu na hakimu alikula rushwa ili amtishe mama ila akakuta mama bora nifungwe kuliko kuuza mali zangu.

Nawaza tu
Hivyo viwanja vina thamani gani? Mtu anatokea vijijini ndani ndani huko ambako shamba huuzwa laki moja. Na huyo mama anaonekana mchovu kabisa namna hyo
 
Ukiangalia picha tu hao manjagu wanamsikitikia

Sema mkuu kesi zina stress sana

Ova
Unaona kabisa wanahuzunika ila hawana la kufanya yule Mchina aliua Tembo wengi Tanzania yupo nje mama ana kilo za swala tena ka mboga awapelekee watoto wake wahuni wanataka afie jela...
 
we zuzu katafute nchi isiyo na sheria. Kenge tu unajifanya una huruma? Mnafiki mkubwa watu km hao wanashirikiana na majambazi, amewezaje kumwua huyo mnyama km kweli ye ni mnyonge? Acheni upuuzi hata huyo mnyama aliyeuliwa ana haki ya kuishi.
Kwa hiyo mama huyo jangili au?
 
we tuambie hiyo nyama ameitoa wapi km siyo wamemwua huyo mnyama? Hao watu mnaowaita wanyonge ni kwamba hawajakufikia tu, ni makatili yenye roho ngumu. Acheni sheria ichukue mkondo wake, huyo jaji aliyemhukumu naye ana roho na moyo km sisi tuache unafiki
Converged, tls wameingilia Kati. Tunashkuru kwa mchango wako
 
Sheria zipo kwa maskini tu. Yule Suleiman Chambis kakamatwa na nyara za serikali ila mahakamani hakukanyaga. Ila huyu maskini kapigwa miaka 22.
 
28aeada3704aff46b4aab83218d33adc
CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa wameanzisha kampeni ya kumsaidia kisheria mjane Maria Emirio Ngoda aliyehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Iringa kifungo cha miaka 22 kwa kosa la kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa, Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.

17ab033562d668ed4cafa45cc0e59e27

Kwa kupitia taarifa yao waliyoitoa mapema leo, Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile pamoja na Wakili Cosmas Kishamawe wamesema kwa kushirikiana na mawakili wengine wa mkoani Iringa tayari wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane huyo.

Mawakili hao wamesema tayari mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa umeanza rasmi leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kutoa msaada wa ushauri na utetezi wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii yasio na uwezo.

Ambindwile alisema tangu waanzishe mpango wa kutoa msaada wa ushauri wa kisheria mkoani Iringa, wameendelea kupokea maombi kutoka kwa makundi ya watu wasio na uwezo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.

“Tuishukuru sana kampuni ya Asas kwa ahadi yake iliyotolewa na mmoja wa wakurugenzi wake, Ahmed Asas kwa kujitokeza kushirikiana nasi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wasio na uwezo hususani wale waishio vijijini,” alisema.

Ni sawa, ila hili ni kati ya jambo la kipumbavu kuliko yote, Ametumia sheria halali ya Tanzania kumfunga, swali: baada ya kumsaidia, Je hakuna sababu ya kuangaliwa sheria iliyomfunga?
 
we zuzu katafute nchi isiyo na sheria. Kenge tu unajifanya una huruma? Mnafiki mkubwa watu km hao wanashirikiana na majambazi, amewezaje kumwua huyo mnyama km kweli ye ni mnyonge? Acheni upuuzi hata huyo mnyama aliyeuliwa ana haki ya kuishi.

Jitahidi sana uwe unakula na vitamins zote uzipate kwa sababu ile gas inayotengenezwa tumboni ukiwa na njaa ikiingia kwenye ubongo inasababisha ubongo kujikaanga na hatimaye fikra kuungua na kunuka.
 
Back
Top Bottom