TLS kumsaidia aliyefungwa Miaka 22 kisa nyama ya Swala

Nyuma ya hiyo kesi naamini kuna mwenye pesa alitaka viwanja vya huyo mama akiamini atauza baada ya hukumu na hakimu alikula rushwa ili amtishe mama ila akakuta mama bora nifungwe kuliko kuuza mali zangu.

Nawaza tu
You have a point. Kuna yaliyojificha nyuma ya pazia. Haiwezekani hakimu akatoa adhabu kali kwa mama ambaye ana watoto na kosa lenyewe siyo kubwa. Angepewa onyo tu na kuachiwa. Wewe hakimu uliyefanya haya Mungu anakuona wewe na kizazi chako. Ahsanteni TLS.
 
Maria alikua kachanganyikiwa kwa hiyo hukumu ila walioumia pia ni hao Manjagu ukiona unaona kabisa wanafikiria hukumu ya Maria uzuri naamini atatoka hata Mama mwenye nyumba ataingilia kati kwa kumpa msamaha ngoja niendelee kumuombea tu Maria atoke aendelee kulea familia yake maisha yana changamoto sana.
 
Ukiangalia picha tu hao manjagu wanamsikitikia

Sema mkuu kesi zina stress sana

Ova
 
Katika vitu vilivyoharibu siku yangu ni siku nilipoona hii picha na kusoma eti amefungwa miaka 22 kwa kukutwa na viapnde vya nyama ya swala. Hivi huyo hakimu ni binadamu au mbwa? Hata kuna kuna sheria lakini wakati mwingine hakimu unatakiwa kutumia akili zako.
 
Nyuma ya hiyo kesi naamini kuna mwenye pesa alitaka viwanja vya huyo mama akiamini atauza baada ya hukumu na hakimu alikula rushwa ili amtishe mama ila akakuta mama bora nifungwe kuliko kuuza mali zangu.

Nawaza tu
Hivyo viwanja vina thamani gani? Mtu anatokea vijijini ndani ndani huko ambako shamba huuzwa laki moja. Na huyo mama anaonekana mchovu kabisa namna hyo
 
Ukiangalia picha tu hao manjagu wanamsikitikia

Sema mkuu kesi zina stress sana

Ova
Unaona kabisa wanahuzunika ila hawana la kufanya yule Mchina aliua Tembo wengi Tanzania yupo nje mama ana kilo za swala tena ka mboga awapelekee watoto wake wahuni wanataka afie jela...
 
we zuzu katafute nchi isiyo na sheria. Kenge tu unajifanya una huruma? Mnafiki mkubwa watu km hao wanashirikiana na majambazi, amewezaje kumwua huyo mnyama km kweli ye ni mnyonge? Acheni upuuzi hata huyo mnyama aliyeuliwa ana haki ya kuishi.
Kwa hiyo mama huyo jangili au?
 
Converged, tls wameingilia Kati. Tunashkuru kwa mchango wako
 
Sheria zipo kwa maskini tu. Yule Suleiman Chambis kakamatwa na nyara za serikali ila mahakamani hakukanyaga. Ila huyu maskini kapigwa miaka 22.
 
Ni sawa, ila hili ni kati ya jambo la kipumbavu kuliko yote, Ametumia sheria halali ya Tanzania kumfunga, swali: baada ya kumsaidia, Je hakuna sababu ya kuangaliwa sheria iliyomfunga?
 
we zuzu katafute nchi isiyo na sheria. Kenge tu unajifanya una huruma? Mnafiki mkubwa watu km hao wanashirikiana na majambazi, amewezaje kumwua huyo mnyama km kweli ye ni mnyonge? Acheni upuuzi hata huyo mnyama aliyeuliwa ana haki ya kuishi.

Jitahidi sana uwe unakula na vitamins zote uzipate kwa sababu ile gas inayotengenezwa tumboni ukiwa na njaa ikiingia kwenye ubongo inasababisha ubongo kujikaanga na hatimaye fikra kuungua na kunuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…