TMA mna lengo gani na Watanzania mpaka kuificha habari hii muhimu iliyotangazwa na DW ya Ujerumani?

TMA mna lengo gani na Watanzania mpaka kuificha habari hii muhimu iliyotangazwa na DW ya Ujerumani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sasa ni rasmi kuwa kuanzia sasa Dunia (hasa hasa huu Ukanda wa Afrika Mashariki Tanzania ikiwemo) inaenda kuwa na ukame mfululizo wa miaka minne (4).

Ninachojua tu GENTAMYCINE ni kwamba Mzungu huwa hakosei hasa pale akipima kitu chake kwa kutumia mitambo yake na kufanya utafiti wa kina.

Tayari athari za ukame mkubwa umeshaanza kujitokeza nchini Kenya, ambako taarifa ambazo GENTAMYCINE nimezipata muda huu naandika huu uzi ni kwamba, wanyama wao wengi sehemu mbalimbali wanaanza kufa kwa kukosa maji.

Hivyo basi kama mtu nisiyetaka unafiki, upuuzi na usiri GENTAMYCINE nawaomba watu (mamlaka) ya TMA muda wowote kuanzia sasa waje na hii taarifa kwa (kwetu) Watanzania ili kwa haraka sana tuweze kutafakari nini cha kufanya.

Kwani kama taifa langu pendwa la Tanzania halitapata mvua kubwa ndani ya miezi hii miwili ijayo hadi mitatu, upo uwezekano biashara na majeneza na uchimbaji wa makaburi ya marehemu ikawa ni nzuri kwa wenye mitaji.

Nimesikitika mno.
 
Mkuu hali ni mbaya na nawaombeni Watanzania wote tuachane Utani hebu upesi sana tuanze kuchukua Tahadhari juu ya hili na ikiwezekana tuanze Kumuomba mno Mwenyezi Mungu kwani nahisi kuna mahala tumemkosea hivyo amekasirika nasi.
Sure, kweli maovu yamezidi
 
Yaani serikali INA tabia ya kuficha ficha taarifa hadi kero.
Bashe anaambiwa ashauri wakulima wasiuze chakula nje anajimwambafy.

Wanasubiria tufe njaa waombe misaada na mikopo wanunulie magari. Failed leadership.
 
Yaani serikali INA tabia ya kuficha ficha taarifa hadi kero.
Bashe anaambiwa ashauri wakulima wasiuze chakula nje anajimwambafy.

Wanasubiria tufe njaa waombe misaada na mikopo wanunulie magari. Failed leadership.
Huna Waziri katika hiyo Wizara bali una Msanii na Mnafiki tupu kama aliyeko Wizara ya Maji anayetutambia Wake zake Wawili wakati Watanzania hawana Maji.
 
Napenda sana na mno Utani ila nakuomba katika hili tuwe serious kidogo kwani hali ni mbaya kwa huu Ukame na inaenda kuwa mbaya kuliko tunavyotegemea kama Watanzania hatutachukua hatua kuanzia sasa.
Hapo sjaleta utani mkuu ww umetupa tahadhari na ndo maana nmekuambia uagize kinywaji kwa bill yngu sabb umetupa habar ambyo wahusika waliichinjia baharini😁😁 sina utani sku hz mkuu
 
Unawazungumzia hao TMA Wanaotumia mitambo chakavu ya mitumba Waliotumia ulaya karne iliyo pita
 
Sure, kweli maovu yamezidi
Mkuu nimeogopa sana na najiuliza hali yetu itakuwaje? Halafu ni kwanini TMA hii Habari wameificha wakati DW ya Ujerumani walikuwa na Nia njema tu Kuitoa Kwetu ili tuanze Kujipanga na hata Kuchukua tahadhari?
 
Unawazungumzia hao TMA Wanaotumia mitambo chakavu ya mitumba Waliotumia ulaya karne iliyo pita
Upuuzi kama huu wa TMA ulifanyika mwaka 1996 tarehe 21 May wakati Satellite ya CNN ilipoona Meli ya Mv Bukoba ikizama na Kuwaambia Watu wa TRC ( wakati huo ) na Wao Kuipuuza mpaka pale waliposikia katika Vyombo vya Habari ( Redio na Tv ) kuwa Meli hiyo imezama na Kuua Watu wengi ndiyo wakawaamini CNN kwa Taarifa yao waliyowapa Awali kabisa Ili tahadhari ichukuliwe na Abiria Waokolewe na hata Meli yenyewe.

Inasikitisha mno.
 
Watafanya nini sasa wakat miaka yote wanacare maisha yao tu.

Nilishawai sema, kwa nchi kama za East afrika kulia lia kisa ukame na kukosa vyakula huo ni upumbavu, serikali ije mitaani kuna watu tuna akili za kuisaidia nchi isipate majanga kwa kutumia akili timamu inayopaswa kutumiwa na hawa viongozi USELESS, tatzo ni kwamba tunaongozwa na watu waliotakiwa kuongozwa.

Kwa namna viongozi wetu walivyoshiriki lile zoezi lao la kubariki mkutano wa mabadiriko ya kimazingira basi tegemeeni majanga mengi na makubwa ya kutisha.

Kwa namna kiongoz wenu mzurulaji anapojiweka karibu na hiyo mikutano na hao washirika wa mabadiriko, na ndivyo hata nchi itayapitia hayo hayo aliyoyashiriki ili kuwaaminisha wananchi wake juu ya yale maushetani yao wanayoyafanya huko Jumuiyani(UN).

hakuna wa kutuokoa na hili zaid yetu wa Tz kuamka na kuanza kujitegemea,

Magonjwa, matishio ya ugaidi na vita, ukame, umasikini, njaa kali na ongezeko la wageni kwa mwamvuli wa wawekezaji haya yote tutarajie kuongezeka sana nchini kwa kipindi chote cha uraisi mpaka pale Mabadiriko yatakapotokea.
 
Wajasiriamali wenzangu ni kwa namna gani tunaweza kugeuza ukame huo kuwa fursa tukapiga hela??
Anza Kutengeneza sana Majeneza kwani ni lazima tu huu Ukame utaondoka mazima na Watanzania 30,000,000 kati ya wale 61,741,120 aliowataja Rais Samia hivi Karibuni. Utapiga mno Hela hivyo Kazi Kwako sasa nimeshakupa idea Kuntu kabisa hiyo.
 
Back
Top Bottom