Today I Learned (TIL): Adam alikuwa na Wake Wawili

Today I Learned (TIL): Adam alikuwa na Wake Wawili

Hadithi ya Lilith ni moja ya hadithi za zamani ambazo zimekuwa sehemu ya mapokeo ya baadhi ya jamii. Katika baadhi ya mafundisho ya Kiyahudi ya kale, Lilith anatajwa kama mke wa kwanza wa Adamu kabla ya Hawa. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba hadithi hii haipo katika maandiko rasmi ya Kiyahudi au ya Kikristo, kama vile Biblia au Talmudi.

Kulingana na hadithi hizo, Lilith alidai usawa na haki sawa na Adamu, na alipokataa kutii amri za Mungu za kuwa chini ya Adamu, aliondoka kutoka kwa Adamu na Paradiso. Baadaye, Hawa aliundwa kutokana na ubavu wa Adamu, kama ilivyoelezwa katika Biblia.

Hadithi hizi za kiasili za maandishi ya zamani mara nyingi hutumika kuelezea masuala ya kijamii, kiutamaduni, au ya kisaikolojia, na hazipaswi kuchukuliwa kama ukweli wa kihistoria. Ni hadithi za kuburudisha au kufundisha, na haziingiliani na mafundisho rasmi ya dini.
Kwani hadithi ya Adamu na Hawa nayo ni ya kweli?. Mimi nadhani zote ni hekaya tu regardles imeandikwa wapi na nani.
 
Unasemaje Adam hakuumbwa tena?
Soma 1Wakorintho 15:45-50..
Pia ulimaliza soma #126
Mkuu, mbona hapa hawaongelewi watu wawili tofauti, anaongelewa mtu mmoja katika roho na katika mwili. Si unajua kuna mwili na roho ambayo ni pumzi toka mbinguni?

IMEANDIKWA,

Mtu wa kwanza,Adam akawa nafsi iliyo hai, Adam wa mwisho ni roho yenye kuhuisha, lakini haitangulii ule wa roho bali ule wa asili baadae uja ule wa roho, mtu wa kwanza atoka katika ardhi ni wa udongo mtu wa pili atoka mbinguni, na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

Sasa mbona ipo wazi mkuu kuwa anaongelea binadamu baada ya kuachana na mwili na kubaki roho? Tena akasema wa kwanza umetoka ardhini, wa pili umetoka mbinguni akimaanisha roho.

OK. Twende na assumption yako,

Ukirudi mwanzo 1 & 2 inasema kuwa uumbaji wa pili binadamu hakuumbwa na mavumbi ila alitoka mbinguni?

Huoni hiyo assumption yako tayari inaibua swali jingine, kuwa binadamu wa kwanza ndo aliumbwa kwa mavumbi au binadamu wa pili ndo aliumbwa kwa mavumbi?

YAANI TUKISHAASSUME KUWA PALIKUWA NA UUMBAJI MWINGINE WA PILI, BASI MASWALI NI MENGI MNO AMBAYO MAJIBU YAKE LAZIMA YANABATILISHA KABISA UUMBAJI WA KWANZA.

MAMBO SI MAGUMU HIVYO MKUU.
 
Mkuu, nilisoma hoja zako zote na ndo nikakueleza hapo ulitumia akili ya ziada isiyohitajika ikakutengenezea mambo ya kufikirika na ukayatengenezea logic ukayahalalisha.

Lakini ni kweli mwanzo 1 na 2 inamaanisha ule uchambuzi wako wa post namba 126?

Binafsi nasema hapana. Mwanzo 1 & 2 ni hadithi moja katika angle 2 tofauti.

Sababu, tukisema hoja zako ni sahihi na ndicho biblia ilichomaanisha basi tunasema biblia imedanganya kuhusu uumbaji kutumia siku 6.

Tukiishia hapa kwanza, tunakubaliana kwamba kwa uchambuzi wako biblia imesema uongo kuhusu siku za uumbaji kuwa 6 na ya saba MUNGU akapumzika?
Mkuu Hauoni wewe ndo unayejifungia kutokana na ulichoamini au ulichofundishwa kuona hakiwezi kuwa uongo wakati tafsiri yako ndyo Ambayo haiko sahihi?

Mkuu Hata mimi Nilikuwa Mbishi kama wewe kipindi nasoma Theology Especially nilipokuwa mwaka wa Kwanza na wa Pili..

NA baadae Tulipoanza kusoma bible Textual Analysis nilikutana na kitu kimoja kinaitwa
nilchokutajia mwanzoni,"Doccumentary Hypothesis" ambayo inasadikiwa imeanza kutumika Tangu miaka ya 1600s..

Kuwa Vitabu vya Pentateuch Vinafuata Sheria ya JEPD (Yaani vimetoka Katika Vyanzo tifauti na haadithi zake zote zimekamilika kwa vyanzo hvyo tatizo lilikuja walipokuwa wanaarrange vitabu vya biblia hawakufanya Analysis ya Text wakakusanya Tu manuscript na kuziweka pamoja na ndo maana utakuta kuna baadho ya Visa vinafanana kimtazamo na kila kitu ila kimerudiwa..

Na hiyo ishu ungeiomgelea kwa upande wa utetezi wa Dizaini hiyo kama wanatheolojia wengi wanavyiconclude ningekuelewa zaidi ila kukazania kuwa ni Account moja hapo nakiri unakosea sana..

JIpe muda Fanya analysis, chunguza Fanya Research sehemu mbalimbali ..

Utapata Jibu..Watetezi baadhi wa Kitheolojia wanasema hiyo mwanzo 1 ni Jehova sources , Na mwanzo 2 ni Elohim Sources...
 
Mkuu Hauoni wewe ndo unayejifungia kutokana na ulichoamini au ulichofundishwa kuona hakiwezi kuwa uongo wakati tafsiri yako ndyo Ambayo haiko sahihi?
Mkuu, mm wala mambo ya mafundisho ya kanisani huko sipo. Yaani ukisema hoja yako, mm nachukua biblia naisoma kama ulichosema ndicho kweli kilichopo. Wala sitaki complications, nipo na biblia ya kiswahili na kingereza hapa. Hakuna kukariri wala kukubali tu, ni kuchukua kile kile ulichoniambia na mimi kukisoma na kuchanganya na za kwangu.
Mkuu Hata mimi Nilikuwa Mbishi kama wewe kipindi nasoma Theology Especially nilipokuwa mwaka wa Kwanza na wa Pili..
Mimi sijasoma theology wala sijui mambo ya uchambuzi wa biblia kwa level hizo za kisomi cha viwango vya juu. Naangalia unachosema nakisoma na mimi nakitafsiri kwa akili yangu ndo nahoji.
NA baadae Tulipoanza kusoma bible Textual Analysis nilikutana na kitu kimoja kinaitwa
nilchokutajia mwanzoni,"Doccumentary Hypothesis" ambayo inasadikiwa imeanza kutumika Tangu miaka ya 1600s..
Ndo maana nikasema pengine jambo jepesi unatumia akili kubwa mno kulichambua ila je, ni kweli linahitaji akili kubwa? Walengwa wa haya maandiko walikuwa ni wenye akili kubwa waliosoma sana?
Kuwa Vitabu vya Pentateuch Vinafuata Sheria ya JEPD (Yaani vimetoka Katika Vyanzo tifauti na haadithi zake zote zimekamilika kwa vyanzo hvyo tatizo lilikuja walipokuwa wanaarrange vitabu vya biblia hawakufanya Analysis ya Text wakakusanya Tu manuscript na kuziweka pamoja na ndo maana utakuta kuna baadho ya Visa vinafanana kimtazamo na kila kitu ila kimerudiwa..
Ok mkuu, hapa siwezi kuhoji maana hata hiyo JEPD sijui maana yake ila ukinipa fungu as long as limeandikwa kwa kiswahili au kingereza naweza soma nikachanganya na za kwangu.
Na hiyo ishu ungeiomgelea kwa upande wa utetezi wa Dizaini hiyo kama wanatheolojia wengi wanavyiconclude ningekuelewa zaidi ila kukazania kuwa ni Account moja hapo nakiri unakosea sana..
Za kuambiwa nimechanganya na zangu mkuu ndo nikafika hapo. Tunaweza kukubaliana kutokukubaliana si mbaya pia.
JIpe muda Fanya analysis, chunguza Fanya Research sehemu mbalimbali ..
Hapana, why should i do this? Reference ya biblia kuhusu uumbaji ndo uliitumia kujadili hoja na mm ndo nikasoma nikaona hapana si sahihi kwa mtazamo wangu, sasa kujadili nje ya hapo labda kama nataka kufungua kanisa.
Mimi si muhubiri ila muhubiri ukiniletea jambo naweza soma vifungu ulivyonipa kisha nikajiongeza mwenyewe kuwa upo sahihi kwa reference uliyotumia au la.
Utapata Jibu..Watetezi baadhi wa Kitheolojia wanasema hiyo mwanzo 1 ni Jehova sources , Na mwanzo 2 ni Elohim Sources...
NOPE. BINAFSI HILI LINAISHIA HAPA HAPA KWENYE REF ULIYOLETA YA BIBLIA. SITAENDA KUPEKUA MAVITU MENGINE.

ACCORDING TO YOU MWANZO 1&2 NI HADITHI ZA UUMBAJI WA BINADAMU MBILI TOFAUTI NA MM NINAVYOONA MWANZO 1&2 NI HADITHI MOJA ANGLE TOFAUTI.
 
Acheni simulizi za kale, sumulizi ya Adam na Eve ni allegory, hakuna mtu existential aliyewahi kuwepo na kuitwa Adam au Eva
Kwanini? Kwani kuna ubaya tukizichambua hizo simulizi hata kama hawakuwepo kweli? Si wapo kwenye hizo simulizi ndo maana kunapatikana hoja za kujibizana?
 
Katika pita pita nimesoma hivo leo. Sio kwenye biblia.

Kwamba Adam alikua na mke wa kwanza anaitwa Lilith ambae nae aliumbwa na Mungu kwa udongo. Sio kutolewa mbavuni kwa Adam.

Ila Adam alivotaka kumdominate Lilith, uyu sista akawa kiburi akakataa kutawaliwa. Wakagombana.

Pia pengine walisema chanzo cha ugomvi ni Lilith kutaka kua on top wakati wa sex, na anasema kabisa ni haki yake. Mambo ya 50/50 hayajaanza leo na mwisho wake wakashindwana.

Hapo ndio Eve akatokea.

Mwenye nyama ataongezea. Elimu haina mwisho.
Nani kakuambia?
 
Mimi sijawahi kukutana na story kama hii kwenye Biblia.
Japo kuna kitu kinanitatiza pia kwenye Biblia na imeandikwa kuwa Cain baada ya kumuua ndugu yake Abeli.. alitembea umbali mrefu hadi akafika nchi fulani, cha kushangaza hiyo nchi ilikuwa na watu wengi tu.. Kwenye biblia wameitwa "Watu wa watu"

Hawa watu walitoka wapi? Na wakati wakati huo wazazi walikuwa ni Adam na Hawa tu. Mimi chimbuko la hawa watu hadi leo silijui.

Na cain baada ya kumuua Abeli, walikuja kumpata tena mdogo wao wala siyo wa kike ni wa kiume. Hii kuendelea kuzaliana hadi kuijaza dunia ilitokea wapi?
 
ACCORDING TO YOU MWANZO 1&2 NI HADITHI ZA UUMBAJI WA BINADAMU MBILI TOFAUTI NA MM NINAVYOONA MWANZO 1&2 NI HADITHI MOJA ANGLE TOFAUTI.
Bhasi naomba uniambie kitu Kipi kilianza kuumbwa kati ya Miti,Wanyama na Adamu..
Adamu na Hawa waliumbwa pamoja au Waliumbwa tofauti..
Nataka Uchambue according to Mwanzo 1 na according to mwanzo 2 kivyake na unipe moral ya kila hadithi hizp
 
Katika pita pita nimesoma hivo leo. Sio kwenye biblia.

Kwamba Adam alikua na mke wa kwanza anaitwa Lilith ambae nae aliumbwa na Mungu kwa udongo. Sio kutolewa mbavuni kwa Adam.

Ila Adam alivotaka kumdominate Lilith, uyu sista akawa kiburi akakataa kutawaliwa. Wakagombana.

Pia pengine walisema chanzo cha ugomvi ni Lilith kutaka kua on top wakati wa sex, na anasema kabisa ni haki yake. Mambo ya 50/50 hayajaanza leo na mwisho wake wakashindwana.

Hapo ndio Eve akatokea.

Mwenye nyama ataongezea. Elimu haina mwisho.
Hii hadithi umeitoa wapi maana haipo kwenye Biblia??
 
Bhasi naomba uniambie kitu Kipi kilianza kuumbwa kati ya Miti,Wanyama na Adamu..
Adamu na Hawa waliumbwa pamoja au Waliumbwa tofauti..
Nataka Uchambue according to Mwanzo 1 na according to mwanzo 2 kivyake na unipe moral ya kila hadithi hizp
Mwanzo moja.
DAY 1. ANGA
DAY 2. MAJI , ARDHI, MIMEA
DAY 3. MIANGA. KUTENGA MCHANA NA USIKU
DAY 4. NDEGE NA SAMAKI
DAY 5. WANYAMA
DAY 6. BINADAMU

Mwanzo mbili. 1-3 inahitimisha ukamilifu wa uumbaji wa mwanzo 1 kwa kusema:

Basi mbingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote, na siku ya saba MUNGU alimalimaliza kazi yote aliyoifanya akastarehe na kupumzika. SAVEN DAYS MWISHO.

Halafu Mwanzo 2:4 akahitimisha tena kwa kusema: Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.

Halafu, rejea ikaanza, Siku ile BWANA MUNGU alipoziumba mbingu na nchi, hapakuwa na miche ya kondeni bado,....... n.k n.k
(HAPA ANAONGELEA KIPINDI KABLA YA KUUMBA MICHE NA BINADAMU HAYUPO BADO)

HAPO MBONA IPO WAZI KABISA MKUU DR MAMBO JAMBO? YAANI KWA AKILI YANGU NAONA KABISA HIYO NI MAELEZO ZAIDI YA UUMBAJI ULIOFANYIKA KWENYE MWANZO 1 NA SI UUMBAJI MPYA. VERY CLEAR.

NA NIKISEMA NIWEKE ASSUMPTION KUWA NI UUMBAJI MPYA MASWALI YAFUATAYO YANAIBUKA.

1. Uumbaji si wa siku 7? Biblia imeanza kwa kudanganya hadithi yake yenyewe?
2. Mwanzo mbili inasema hapakuwa na mtu wa kulima. Kwanini aliyeumbwa wa kwanza hajawekwa kwenye list ya mtu? Hakuwa mtu?
 
Nakusoma mkuu.

Haya tuendelee
 
Kuna kitu kimoja kinakuchanganya Nimekiona..

na pia nimegundua Unataka pia kwenye mwanzo mbili wakwambia siku ya 1 ilikuwa hivi siku ya pili ilikuwa hivi..
Na hiyo ndiyo shida ilipo..

Sasa ngoja tuangazia Vitu hapa chini ili unielewale

Haya Twende na Mimi sasa!

Beresh'it 2:4...
(Mwanzo 2:4)..

Hebrew (Kiebrania)..

וְאֵ֗לֶּה תּוֹלְדֹ֧ת הַשָּׁמַ֛יִם וְהָאָ֖רֶץ בְּהִבָּֽרְאָ֑ם בְּי֗וֹם עֲשׂ֛וֹת יְהוָ֥ה אֱלֹהִ֖ים אֶ֥רֶץ וְשָׁמָֽיִם׃..
Inatamkwa Hivi..

"Ve’eleh toldot hashamayim veha’ardhi behibare’am beyom asot Adonai Elohim erdhi veshamayim."

sasa Neno Ve linamaanisha "Na" na neno "Eleh" linamaanisha Hiki....

Kwa hyo tafsiri sahihi itakuwa kama ifuatavyo..
  • ! (Ve) - And
  • אֵ֗לֶּה (eleh) - these
  • תּוֹלְדֹ֧ת (toldot) - generations
  • הַ (ha) - of
  • שָּׁמַ֛יִם (shamayim) - heavens
  • וְ (ve) - and
  • הָ (ha) - the
  • אָ֖רֶץ (ardhi) - earth
  • בְּ (be) - in
  • הִבָּֽרְאָ֑ם (hibare’am) - their being created
  • בְּ (be) - in
  • י֗וֹם (yom) - day
  • עֲשׂ֛וֹת (asot) - to make
  • יְהוָ֥ה (Adonai) - the Lord
  • אֱלֹהִ֖ים (Elohim) - God
  • אֶ֥רֶץ (erdhi) - earth
  • וְ (ve) - and
  • שָׁמָֽיִם (shamayim) - heavens
Sasa neno eleh likiwa na maana ya These "Hivi" ndo lililobadilisha maana halisi ikaonekana Habari hiyo haizungumzii habari iliyopita sijui kama unajua Tamathali za Semi?

Kuna tofauti sana kama ingetumiwa neno.."And those Was the Generation of...." na "ilivotumiwa neno And these was the generation"

Sentensi ikianza na those humaanisha ni rejea ya yaliyo Nyuma..

Ila sentensi ikianza na These sio rejea bali ni Mada mpya..

Ni sawa na kusema "hicho kilikuwa" na kusema "hiki ni"
Nafikiri sasa umeelewa kuwa Those are the Different account..
Ila ukitaka niendelee kuchambua its ok
 
Hujamaliza kumalizia hii hadithi vijana wa kiume/kike wanapofikia balehe lilth huwatokea katika ndoto

Vijana wa kiume huwaonyesha wakifanya tendo la jimai na Mwanamke mzuri sana (Succubuss) na kufyonza manii zao

Vijana wa kike huona wakifanya tendo la jimai na Mwanaume mzuri sana (Incubus) mpaka wanaingiziwa manii na huyo Mwanaume Shababi mwenye bonge la ndonga linalojua kusugua tupu yake vilivyo wakiwa usingizini

Na hivyo ndivyo lilth anavyojipatia watoto katika upande wake,
View attachment 2936875
Documents zozote ku support hii wazo lako..au ni stories za kwenye gahawa
 
Kuna kitu kimoja kinakuchanganya Nimekiona..

na pia nimegundua Unataka pia kwenye mwanzo mbili wakwambia siku ya 1 ilikuwa hivi siku ya pili ilikuwa hivi..
Na hiyo ndiyo shida ilipo..

Sasa ngoja tuangazia Vitu hapa chini ili unielewale

Haya Twende na Mimi sasa!

Beresh'it 2:4...
(Mwanzo 2:4)..

Hebrew (Kiebrania)..

וְאֵ֗לֶּה תּוֹלְדֹ֧ת הַשָּׁמַ֛יִם וְהָאָ֖רֶץ בְּהִבָּֽרְאָ֑ם בְּי֗וֹם עֲשׂ֛וֹת יְהוָ֥ה אֱלֹהִ֖ים אֶ֥רֶץ וְשָׁמָֽיִם׃..
Inatamkwa Hivi..

"Ve’eleh toldot hashamayim veha’ardhi behibare’am beyom asot Adonai Elohim erdhi veshamayim."

sasa Neno Ve linamaanisha "Na" na neno "Eleh" linamaanisha Hiki....

Kwa hyo tafsiri sahihi itakuwa kama ifuatavyo..
  • ! (Ve) - And
  • אֵ֗לֶּה (eleh) - these
  • תּוֹלְדֹ֧ת (toldot) - generations
  • הַ (ha) - of
  • שָּׁמַ֛יִם (shamayim) - heavens
  • וְ (ve) - and
  • הָ (ha) - the
  • אָ֖רֶץ (ardhi) - earth
  • בְּ (be) - in
  • הִבָּֽרְאָ֑ם (hibare’am) - their being created
  • בְּ (be) - in
  • י֗וֹם (yom) - day
  • עֲשׂ֛וֹת (asot) - to make
  • יְהוָ֥ה (Adonai) - the Lord
  • אֱלֹהִ֖ים (Elohim) - God
  • אֶ֥רֶץ (erdhi) - earth
  • וְ (ve) - and
  • שָׁמָֽיִם (shamayim) - heavens
Sasa neno eleh likiwa na maana ya These "Hivi" ndo lililobadilisha maana halisi ikaonekana Habari hiyo haizungumzii habari iliyopita sijui kama unajua Tamathali za Semi?

Kuna tofauti sana kama ingetumiwa neno.."And those Was the Generation of...." na "ilivotumiwa neno And these was the generation"

Sentensi ikianza na those humaanisha ni rejea ya yaliyo Nyuma..

Ila sentensi ikianza na These sio rejea bali ni Mada mpya..

Ni sawa na kusema "hicho kilikuwa" na kusema "hiki ni"
Nafikiri sasa umeelewa kuwa Those are the Different account..
Ila ukitaka niendelee kuchambua its ok
Hivi ni kweli kuyaelewa hayo mafungu inahitaji kuyabadili kwa lugha hizo ndo mtu aelewe? Kwamba walengwa wa biblia inabidi waelewe hayo ma Ve na ma Na sijui na kilatini?

EMBU TUSICHOSHANE MKUU, HAPO HATA UKINIDANGANYA MM NAHOJI VIPI SASA NA KIARABU HICHO?

Mimi naona tuishie tu kukubaliana kuwa according to you, mwanzo 1&2 ni uumbaji wa binadamu wa4, na reference ndo hayo manamba namba.

na mimi kwa uelewa wangu mwanzo 1&2 ni hadithi moja iliyosimuliwa kwa angle mbili tofauti na uumbaji ni binadamu wa2, Adam na Hawa sijui Eva na reference ni mtiririko wa hiyo hadithi tu ilivyosimuliwa.

ASANTE.
 
Kabla sijakuaga mkuu naomba niweke Record sawa..

Bible imeandikwa kwa Lugha ya Kihebrania/Kiebrania....

Ili kupata maana halisi ya neno ni Vyema kuiangalia Lugha yake halisia iliyoandikiwa..
Bible unayosoma sasa hivi ni tafsiri ya Biblia kwa lugha ya kingereza na kiswahili na iko labeled kabisa tafsiri hiyo ni ya mwaka gani..

Ni vema Ili kuujua Ukweli Lazma uangalie Manuscript ilkuwa inasemaje..

Huenda mtafasiri alichanganya maana na akapotosha jamii nzima..

Na ndo maana nawapenda hawa waislam kwa sababu Huweka lugha asili na Lugha tafsiri ili ukisoma uone kabisa kuwa Walichoandika na walixhotafsiri ni sawa?

Kuna vitu viwili kama ungebahatika Kusoma Theolohy hufanya kazi sana katika kuchunguza Maandiko..

Kuna Translation na Interpretation..
Inaweza kuwa mwandishi aliInterprete badala.ya kutranslate lazima uangalie Neno halisia lilikuwa lipi ili ujue kama ilikuwa ni interpretation au ilikuwa ni translation...

Asante sana
 
  • Thanks
Reactions: Tsh

Asante, Mm nafahamu kiswahili na kingereza, naamini ukichukua biblia za lugha nyingine bado hadithi inaweza kuwa ile ile.

Sasa kama lugha zote hizi zimetafsiriwa kutoka lugha mama na watafsiri wote wakapotosha basi huo upotoshaji utapokelewa kama uhalisia na walengwa ambao ni wasomaji.

Naamini kutafsiri lugha kuna mchakato unaohusisha wasomi wa lugha kama wewe na ni wengi na pengine wasomi kukuzidi.

Hizi ni hadithi za kale za kiimani, iwapo kama wamekaa wakapindisha tafsiri kwa kiswahili, kingereza, kifaransa, kijerumani, kiitaliano na lugha nyingine na pasiwe na conflict ya tafsiri kwa lugha zote hizo isipokuwa lugha mama basi walengwa wataipokea na kuelewa hivyo.
 
Back
Top Bottom