HII SIO HADITHI, NI ONYO!
Ukiwa mkoa wa mara, fanya unavyoweza asee ila usimtukanie mtu mama yake. Utakufa unajiona. Kwa mkoa mara, hilo tusi ni point of no return!
Ukiwa mkoa wa Mara, usimdharau mtu kwa kuupima mwili wake. Hata ukiwa bingwa wa karate, kung fu, jiu jitsu, tai chi, mieleka na mafunzo mengine yasiyoeleweka, usimdharau mtu kisa unaona yuko na afya mgogoro. Utakufa bila kujua kilichokuua!
Ukiwa mkoa wa Mara, ni marufuku kuingilia ugomvi usiokuhusu. Ukiona wanaume wameamua kushikishana adabu, kaa pembeni asee. Ukiingia kuachanisha unakufa wewe!
Ukiwa mkoa wa Mara na ukajikuta uko kwenye mazingira yanayokulazimu kupigana, basi usochague silaha, wala usipigane kiungwana. Hakunaga vita ndogo mkoa wa Mara. VITA NI VITA!
Ukiwa mkoa wa Mara, ukampiga mtu ukamzidia akakimbia, asee toweka hilo eneo haraka iwezekanavyo. Mkurya akikimbia ugomvi haujaisha, ugomvi ndio unaanza na this time harudi kinyonge!
Ukiongelea gangs za mitaani, siku hizi zimepoa mkoa Mara. Lakini miaka kumi iliyopita, Musoma ilikua haina tofauti ni mitaa ya Sinaloa Mexico. Ni Musoma pekee ndio defender ya FFU ilishindwa kutuliza ugomvi wa gangs mbili hasimu, ikabidi warudi kujikusanya, zikaja defender nne na mabomu ya machozi ndio watu wakatawanyika!
NB: Ugomvi sio kitu chema!