Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Kufuatia ajali ya vijana wawili wenye Subari Pichani wakishindana na Crown , sasa ni rasmi “bodaboda akili zao ni sawa kabisa na vijana wa Subaru/Crown”
Ajali imetokea Morogoro, wakipiga ligi na wakakutana na chuma Uso kwa uso.
Ukiangalia Barabara za TANROAD , hakuna ya kuendesha zaidi ya 100/km per h. Kuna pot holes,wanyama wanakatisha, kuna magari mabovu yanatengenezwa baranarani, kuna Barrier za mazao na polisi bila tahadhari, sasa vijana mkinunua Crown ama subaru mnaweza kwenda kwenye official rally na si hizi barabara zetu.
Mungu atusaidie na pole kwa wanafunzi wote wa CASFETA, Upanga CCC na Ardhi University