Tofauti ya “Vijana wa Subaru & Crown” na “bodaboda” haipo!

Tofauti ya “Vijana wa Subaru & Crown” na “bodaboda” haipo!

Hapana. Same Mwanga njia mbovu sana. Mombo Same ndio njia nzuri imenyooka,pana haina kona kali. Ila siku hizi najitahidi kutembea under 130kph.
Ooh yes, Mombo kwenda same pana kaumbali. Sijaipita hio njia almost 5 years now. Umri wetu ukiwa na majukumu lazma kumitigate risks tu. Mwendo wastani
 
Sasa mtu akifa anapata hasara gani kwani? Pengine labda mtu apate ulemavu, inaweza ikawa hasara ila sio kufa!
Ukiwa huna mchango wowote katika jamii inayokuzunguka utaacha skendo wenzako wanaacha pengo!!
 
Naona mmekuja kujitetea 😀😀😀
Unakuta mtu ana Subaru anaenda taratibu unataka kumpita mara anakurupuka kama mashindano 😊😊
Madereva wa Subaru sijui huwa tunawahi wapi aisee ,Mimi siwezi kufanya ligi na crown hata sikumoja najua hapo ni kutafuta kifo Tu
 
View attachment 3570524
Kufuatia ajali ya vijana wawili wenye Subari Pichani wakishindana na Crown , sasa ni rasmi “bodaboda akili zao ni sawa kabisa na vijana wa Subaru/Crown”

Ajali imetokea Morogoro, wakipiga ligi na wakakutana na chuma Uso kwa uso.

Ukiangalia Barabara za TANROAD , hakuna ya kuendesha zaidi ya 100/km per h. Kuna pot holes,wanyama wanakatisha, kuna magari mabovu yanatengenezwa baranarani, kuna Barrier za mazao na polisi bila tahadhari, sasa vijana mkinunua Crown ama subaru mnaweza kwenda kwenye official rally na si hizi barabara zetu.

Mungu atusaidie na pole kwa wanafunzi wote wa CASFETA, Upanga CCC na Ardhi University
Tunakamua Ile Ile 120 babaake
(Kwenye Kona ufunge mkanda)
Yeah ndio manake
R.I.P GWEA
 
Unatania au? Weekend iliopita nimeendesha Dar-Moshi-Dar nimejaribu kujizuia nimetembea sehemu nyingi 120-130kph. Ajali nyingi tatizo sio mwendo ni uzembe na barabarani kumejaa waendesha magari sio madereva mtu anakutupuka tu kisa Subaru au Crown inakimbia.
Sahv hakuna madereva
Wao wanachojuwa ni kukanyaga tu...
Mtu unakimbia speed unakwenda wapi,tatizo watoto sahv ujuaji mwingi

Ova
 
Shida sio Subaru wala si Crown.

Tabia chafu chafu za madereva na ujuaji ulipitiliza

Leo hii usiku huu..Basi la Mbazi Dsm to Arusha ametoa basi zima zima kidogo atuue..mbele ya Msata hapo.
Leo hii bas la BM na hizi mvua naye akatoa nzima nzima kidogo azame ndani ya tanki ya mafuta.

Watu wengi tumekuwa wapuuzi huku njiani.

Njoo na hawa washamba wanawasha full kuanzia mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari.
 
Dah mkuu ile Mbeya-Igawa ni majanga, pale pona yako bora upite mchana tu! Hivi kilichofanya ile barabara mpya iishie igawa toka Makambako ni kipi?
Ile barabara ni hatari sana, huenda kulikuwa na shortage of funds kuweza kujenga hadi Mbeya, hivyo ujenzi kuishia Igawa
 
Sijapita hivi karibuni Mkuu

Kama nayo ina mashimo, basi Nchi nzima almost asilimia 85 ya barabara zetu zitakuwa tia maji tia maji 🙌

Na hivi wao saivi wanatumia ATCL pamoja na sgr sisi tuonatumia barabara ndiyo basi tena 🙌
Ina mashimo na viraka vingi sana. Ni kama unendesha barabara ya vumbi. Kama sio mzoefu hii njia ni hatari.
 
Back
Top Bottom