Tofauti ya “Vijana wa Subaru & Crown” na “bodaboda” haipo!

Tofauti ya “Vijana wa Subaru & Crown” na “bodaboda” haipo!

Bara zetu nyembamba bila kutegemea utakumbana na shimo katikati cha kushangaza speed 100 inaonekana mwendo mkaliiii kwa ufinyu wa barabara.
Hio ndio chanzo kikuu, pili uzembe. Highway driving watu wanachukulia simple ila inataka akili yenye maamuzi ya haraka na hesabu kali. Unaanza ligi hujui risks, Blindspot Overtaking (Corners and Hills) kisha Tailing. Mwenzio anaanza toka nitoke na wewe unafata nyuma tu bila mahesabu lazma uchakae.

Hio Case ya hio Subaru SJ5 sababu naitumia mara kwa mara ni nzito kupokea maagizo. Kwa style ya toka nitoke inakubidi uwe na nafasi ya kutosha. Crown ni nyepesi na inatii maagizo chap kukata gari na kurudi kushoto ni sekunde tu. Makosa ya dereva hakuwa na uzoefu bila shaka. Walazwe pema peponi.
 
Juzi nimetoka safari, Dar Tanga Lushoto na kurudi, data zangu izi hapa:

View attachment 3570608Pamoja na kwamba nimetembea jumla ya kilometa 860, tena 70% usiku, average speed yangu ni 32 km/h.

Hakuna sehemu nimeendesha above 70 km/h kwasababu nazijua barabara zetu, dakika 2 nyingi tuta, au shimo, au mnyama/mtu kavuka.

Better late than never.
Hongera sana mkuu, naona unasukuma Honda Vezel kagari katamu sana hako ila kwa huo wastani sio kweli bana.
 
Hakuna barabara ya kuendesha zaidi ya 100km/h Tanzania. Unakuta mtu ana gari yenye maximum speed 360km/h lakini nusu hajawahi kugusa. Sababu kubwa ni matuta na vibao 50
Hio nakubali, sema serikali imeridhika kununua magari ya billion 700 kila mwaka badala ya kupanua barabara zote zifate mfano kama wa Kimara to Kibaha Mile 1.
 
Barabarani huwezi kukubali upigwe overtake hivihivi. Unanyoosha goti mpka asalimu amri mwenyewe, madereva wanaelewa hii kitu. Ligi barabarani Ina raha sana ila ndio hivyo viwango vya barabara zetu ni duni sana. Tunaweka maisha yetu hatarini
Wapumzike kwa amani wapendwa wetu
Kwenye hatari lazma upunguze kidogo kisha unaanza kumtafuta upya mbaya wako😅 ndio udereva, sio unaunga kama treni tu.
 
Kwa kweli changamoto yetu kubwa ni ubovu wa miundombinu yetu ya barabara

Kwa Nchi nilizoendelea, kuna barabara wanakwambia kabisa minimum speed ni 120km/hr

Sisi huku vibao vya 50 ni vingi mno, na hii wamefanya kutokana na uduni wa miundombinu

Barabara ya DSM - Morogoro haina tofauti na barabara ya Morogoro - Dodoma ni finyu mno

Ukija kipande cha Mbeya hadi Igawa, ndiyo disaster

Mashimo kama yote alafu ndiyo barabara ya kwenda Nchi za Zambia/Malawi/Zimbabwe/DRC hadi South Africa 🙌

Ukiambiwa hii Nchi watu wanalipishwa Kodi utashangaa 🙌
Dah mkuu ile Mbeya-Igawa ni majanga, pale pona yako bora upite mchana tu! Hivi kilichofanya ile barabara mpya iishie igawa toka Makambako ni kipi?
 
Hakuna barabara ya kuendesha zaidi ya 100km/h Tanzania. Unakuta mtu ana gari yenye maximum speed 360km/h lakini nusu hajawahi kugusa. Sababu kubwa ni matuta na vibao 50
Unatania au? Weekend iliopita nimeendesha Dar-Moshi-Dar nimejaribu kujizuia nimetembea sehemu nyingi 120-130kph. Ajali nyingi tatizo sio mwendo ni uzembe na barabarani kumejaa waendesha magari sio madereva mtu anakutupuka tu kisa Subaru au Crown inakimbia.
 
Ina mashimo kama barabara za mtaani na ilivyo nyembamba usipotulia unajikuta kwenye shamba la mtu.
Aisee basi ni hatari sana huko, ile barabara ishakufa inatakiwa ipanuliwe sijui kwanini hawajiongezi hawa viongozi wetu wa Elimu mbalimbali😂
 
Unatania au? Weekend iliopita nimeendesha Dar-Moshi-Dar nimejaribu kujizuia nimetembea sehemu nyingi 120-130kph. Ajali nyingi tatizo sio mwendo ni uzembe na barabarani kumejaa waendesha magari sio madereva mtu anakutupuka tu kisa Subaru au Crown inakimbia.
Same - Mwanga unapata sehemu za kunyoosha goti vizuri tu
 
Juzi nimetoka safari, Dar Tanga Lushoto na kurudi, data zangu izi hapa:

View attachment 3570608Pamoja na kwamba nimetembea jumla ya kilometa 860, tena 70% usiku, average speed yangu ni 32 km/h.

Hakuna sehemu nimeendesha above 70 km/h kwasababu nazijua barabara zetu, dakika 2 nyingi tuta, au shimo, au mnyama/mtu kavuka.

Better late than never.
Hiki kipaji. 70kph njia kuu inaweza kuwa hatari kwako.
 
Back
Top Bottom