Tofauti ya “Vijana wa Subaru & Crown” na “bodaboda” haipo!

Bara zetu nyembamba bila kutegemea utakumbana na shimo katikati cha kushangaza speed 100 inaonekana mwendo mkaliiii kwa ufinyu wa barabara.
Hio ndio chanzo kikuu, pili uzembe. Highway driving watu wanachukulia simple ila inataka akili yenye maamuzi ya haraka na hesabu kali. Unaanza ligi hujui risks, Blindspot Overtaking (Corners and Hills) kisha Tailing. Mwenzio anaanza toka nitoke na wewe unafata nyuma tu bila mahesabu lazma uchakae.

Hio Case ya hio Subaru SJ5 sababu naitumia mara kwa mara ni nzito kupokea maagizo. Kwa style ya toka nitoke inakubidi uwe na nafasi ya kutosha. Crown ni nyepesi na inatii maagizo chap kukata gari na kurudi kushoto ni sekunde tu. Makosa ya dereva hakuwa na uzoefu bila shaka. Walazwe pema peponi.
 
Hongera sana mkuu, naona unasukuma Honda Vezel kagari katamu sana hako ila kwa huo wastani sio kweli bana.
 
Hakuna barabara ya kuendesha zaidi ya 100km/h Tanzania. Unakuta mtu ana gari yenye maximum speed 360km/h lakini nusu hajawahi kugusa. Sababu kubwa ni matuta na vibao 50
Hio nakubali, sema serikali imeridhika kununua magari ya billion 700 kila mwaka badala ya kupanua barabara zote zifate mfano kama wa Kimara to Kibaha Mile 1.
 
Kwenye hatari lazma upunguze kidogo kisha unaanza kumtafuta upya mbaya wako😅 ndio udereva, sio unaunga kama treni tu.
 
Dah mkuu ile Mbeya-Igawa ni majanga, pale pona yako bora upite mchana tu! Hivi kilichofanya ile barabara mpya iishie igawa toka Makambako ni kipi?
 
Hakuna barabara ya kuendesha zaidi ya 100km/h Tanzania. Unakuta mtu ana gari yenye maximum speed 360km/h lakini nusu hajawahi kugusa. Sababu kubwa ni matuta na vibao 50
Unatania au? Weekend iliopita nimeendesha Dar-Moshi-Dar nimejaribu kujizuia nimetembea sehemu nyingi 120-130kph. Ajali nyingi tatizo sio mwendo ni uzembe na barabarani kumejaa waendesha magari sio madereva mtu anakutupuka tu kisa Subaru au Crown inakimbia.
 
Ina mashimo kama barabara za mtaani na ilivyo nyembamba usipotulia unajikuta kwenye shamba la mtu.
Aisee basi ni hatari sana huko, ile barabara ishakufa inatakiwa ipanuliwe sijui kwanini hawajiongezi hawa viongozi wetu wa Elimu mbalimbali😂
 
Same - Mwanga unapata sehemu za kunyoosha goti vizuri tu
 
Hiki kipaji. 70kph njia kuu inaweza kuwa hatari kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…