Toka Bongo Fleva ianzishwe hakuna mwanamziki wa kike mwenye sauti ya kuvutia, kipaji cha kutunga na kuimba kwa hisia kama Lady Jaydee

Toka Bongo Fleva ianzishwe hakuna mwanamziki wa kike mwenye sauti ya kuvutia, kipaji cha kutunga na kuimba kwa hisia kama Lady Jaydee

Kabisa, JiDe yuko njema mno, anaimba high pitched notes vizuri, haami key . Big up kwake
 
Binafsi nimekuwa mfuatiliaji wa nyimbo za bongo fleva haswa kwa upande wa R&B, na nimejiridhisha kwamba toka uanzishwaji wake ulipoanzia miaka zaidi ya 25 iliyopita, hadi leo hii hakuna msanii wa kike mwenye kipaji cha uimbaji, utungaji na ufikishaji ujumbe maridhawa wa nyimbo zake kama Lady Jaydee.

Msanii huyu ukiachilia mbali ubora wa album zake, na nyimbo zake ambazo kwa uchache nitaziandika hapo chini. Pia alikuwa ni mmoja wa wasanii ambao walishirikishwa katika nyimbo nyingi za wasanii mbali mbali wakubwa na wadogo na akafanya vizuri.

Itoshe tu kusema kwamba uwezo wake, ujuzi wake na utaalam wake wa kutunga na kuimba uliwasaidia vijana wengi (underground) kutoka kimziki mara tu baada ya kumshirikisha Lady Jaydee katika nyimbo moja au mbili.

Je kwa wale wafuatiliaji wenzangu wa bongo fleva, mnaona ni msanii gani mungine wa kike ambae anamsogelea japo kwa mbali mwanadada huyu anaejulikana kwa jina lingine la Komandoo wa R&B.

Baadhi ya album zake ni:
1. Machozi - aliyoitoa mwaka 2000

2. Binti - aliyoitoa mwaka 2003

3. Shukran - aliyoitoa mwaka 2007

Baadhi nyimbo zake ni:
1. Siku hazigandi
2. Siwema
3. Siri yangu
4. Yahaya
5. Ndindindi
6. Basimama
7. Understanding alioimba na T.I Dee
Baadhi ya nyimbo alizoshirikishwa ni:
1. Mr II Proud aka "Sugu" ft Jaydee - Mambo ya fedha.
2. Prof Jay ft Jaydee - Bongo Dar es Salaam.
3. Mwana FA ft Jaydee - Sitoamka
5. Mwana FA ft Jaydee - Alikufa kwa ngoma
6. AY ft Jaydee - Machoni kama watu
7. Ngwea & FA ft Jaydee - Sikiliza
8. East Coast ft Jaydee - Ama zangu ama zao
9. Mandojo & Domokaya ft Jaydee - Wanoko

Kifupi ameimba na kushirikishwa katika nyimbo nyingi kuliko msanii mungine yoyote wa kike. So ili nisiwachoshe wasomaji nimeandika hizo, ila kama kuna mtu anaweza kuongeza zingine hapo chini ni ruhusa.

Moderators naomba muifungue hiyo picha ionekane vizuri ili wale wasiomjua (vizazi vya leo) vimuone msanii tunaemzungumzia.
Hapana mkuu.
Kiuno bila mfupa ndo yupo juu.
 
Anaimba lakini sauti nzuri hapana
Huwa akiimba na yule jamaa Rama dee inakuwa bomba sana
 
kuna ngoma ali shirikishwa na mwana fa inaitwa #hawajui_tulipotoka_watajuaje_tunapokwenda, inanikumbushaga mbali aisee mitaa ya mwilavya kasulu kigoma
 
Unamjua Vumilia wewe!!!!!
Chanzo ni umaskini au ni nini??
Niambie nijue..[emoji445]
Kinachofanya wazazi wako wanikatae...
Niambie nijue..

Au mimi sina hadhi ya kuwa na wewe eeh
Kama mimi sikufai oa mwingine eeeh...oh baby.....[emoji444]
 
niliwahi kuwakubali jide, banana, banza stone, papii kocha pamoja na tid. hao walikuwa wanaweza kucheza na sauti zao mpaka ukaufurahia muziki wao.
 
Alikuwa anachukua manyimbo ya kijita anaweka maneno
 
Lady Jay Dee Enzi zake alisumbua Sana kwenye nyimbo zinazoigusa jamii hasa akizingatia zaidi maadili na mashairi mazuri na mpangilio mzuri wa kuimba.

Kuna Ile Ngoma anaanza " Nakupenda, nakutaka nakuhitajiii..." Ngoma kali humo kuna lugha kama nne hivi ni balaa Sana kuna kingereza, Kiswahili, kifaransa na kiganda ni shida Sana aisee... Lakini tukija upande wa sauti hapo ni Big No...

Kwangu mdada aliyenipagawishaga Kwa sauti Tamu ni mwanadada Ray C....

Kuna mdada niliwahi kudate nae one day akanitumia voice note ya ray c uko wapi.... Sijui aliitoa wapi lakini Nilihisi nywele zimesimama [emoji16][emoji28]
 
Sauti hapana labda stara Thomas na Ruby..

Ila kuimba yupo vizuri ila sauti hapana ni kawaida sana anashindwa hata na Ally kiba.
 
Utoto unawasumbua nyinyi ..

Hana sauti acha ku-overrate ,labd besi nishwahi kumuona akiongea live hata hizo nyimbo sauti hana ni uongo.

Nyimbo muangalie ile singleboy akiwa studia mishipa inavyomtoka kwa kubana sauti.

Usimfananishe na Ruby kwa sauti utaonekeana kichaa
 
Back
Top Bottom