Top 10 Best secondary schools of all time in Tanzania

Top 10 Best secondary schools of all time in Tanzania

Mhh...mbona zipo nyingi tuuu...sema zinamchuano mkubwa sana

Ngoja niongezee hapo

St. mary Goret

Canossa

Mazinde juu(st marys)

st james.......nk you name them uh!!
umenena...
 
Za government na za private hebu tofautisha hapo kuna watafutaji na waletewaji hapo.
 
hawa wanaosoma private schools wanapata elimu kwa njia rahisi bila jasho, maana wanafundishwa vizuri, na wale wanaosoma shule za gvt wanasota sana kwa sababu vitu vingi hawavipati darasani badala yake inawabidi waende tuition, na kama wazazi hawawezi kumudu gharama za kuwalipia watoto wao ada za tuition, kuna kuwa na uwezekano mkubwa kwa wanafunzi hao kufail, na wachache wanaoweza kutumia nguvu zao za ziada ndo wanaofaulu hivyo shule za serikali lazima zitaendelea kubolonga tu, SOLUTION YANGU: Serikali iwajali walimu maana walimu wanashindwa kufanya kazi zao za ualimu kwa ufanisi kutokana na maslahi duni na mazingira magumu ya kufundishia na vifaa vya kujifunzia na kufundishia nadhani kila mmoja wetu ni shahidi kwamba hawa walimu wanaofundisha hizi shule za private zinazofaulisha sana, wanapata mishahara mizuri na wana mazingira mazuri ya kazi na nyenzo tele za kikazi.
 
BelindaJacob....Labda enzi zile za kina mr. Thind ila sasa hakuna cha SRSS au AKMSS....nowadays kwishney....

Nowdays feza anawakimbiza, xul fees tu million 5 per year, shule kama hoteli inavyowaka huko bahari beach,
Sbrss na akmss zilikuwa old days but nowdays watoto wa kijanja wote wanaelekea feza boys while girls wanaelekea marian girls, sbrss inabaki na waliokosa chance hizo shule kubwa miaka ya sasa
 
MKATA KIU unaisifia feza kwa kuwainua vilaza kuwa top perfomers labda zamani hizo. Lakini tabia yao ya kununua vichwa kutoka special na kutoa offer kwa waliopiga fresh kujiunga nao. Shule za serikali hasa specia zinajitahidi sana pamoja na ugumu wa mazingira. Chukulia mfano Tabora boys kwa sasa mazingira ni magumu mno kama maji ni tatizo pamoja na mengineyo. Hao jamaa wa private ukiwaweka na jamaa wa serikalini utaona wanavyopwaya.
 
Last edited by a moderator:
lakini ilikuwa sifa kusoma, government school, maana yake ni kwamba umafaulu kuliko wengine ndio maana ukachaguliwa! Sure we were looking down to those who went to private school (kasoro seminaries na intl schools) hata kama ni kaka yako wa tumbo moja.
Enzi hizo ukifaulu darasa la saba unaonekana kama shujaa fulani kwa jinsi utakavyokuwa unapongezwa na watu.
 
acha utani huwezi fananisha hicho kijishule cha tosamaganga na mzumbe,ilboru,tbrboys,kibaha ,
Tatizo wanaobishania humu ni watoto walisoma miaka ya juzi kuanzia miaka ya elfu mbili.Sisi tuliosoma enzi hizo za Mwalimu tunazijua shule ambazo ukisoma kila mtu anakukubali na zilikuwa zinajulikana kama shule za vipaji maalumu.Nikianza kwa kuzitaja kulikuwa na shule maalumum kama;TABORA BOYS,TABORA GIRLS,MAZENGO,MOSHI TECHNICAL,TANGA TECHNICAL,IFUNDA TECHNICAL,MTWARA TECHNICAL NA RUVU BOYS. Anayebisha atakuwa ni kati ya wale waliosomo miaka ya hivi karibuni kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea,Kulikuwa hakuna cha Mzumbe wala Ilboru wakati huo.
 
lakini ilikuwa sifa kusoma, government school, maana yake ni kwamba umafaulu kuliko wengine ndio maana ukachaguliwa! Sure we were looking down to those who went to private school (kasoro seminaries na intl schools) hata kama ni kaka yako wa tumbo moja.

True kabisa, enzi hizo ukiwa unasoma Government basi wewe kipanga kweli kweli...private ilikuwa ni kwa wale ambao hawakufaulu. kiufupi ni kwamba yawezekana hukuwa mjinga, bt akili zako hazikutosha kufaulu ukaenda government.
ila mambo sasa tofauti kweli...ukimpeleka mwanao government unaonekana hauko serious na Elimu.
 
Hapa mkuu hauko analytical. Hizo shule unazodai kuwa ni Best school zinachuja wanafunzi wote vipanga (wenye uwezo wa Juu) then wanaretain kwenye shule zao. Kwa habari ya kuwa ni shule Bora sio kweli. Ubora wa Mwanafunzi ni individuals. Labda utupe data za shule ambao zimechukua wanafunzi wenye uwezo wa chini then ikawapika wakatoka na flying colour nitakuelewa.

Ukweli zinafanya vizuri kwa kuwa wanachuja watoto wote wenye uwezo wakati wa Interview, then shule zingine ubeba waliobaki. Hivyo suala ya Best school halipo.
 
Tatizo wanaobishania humu ni watoto walisoma miaka ya juzi kuanzia miaka ya elfu mbili.Sisi tuliosoma enzi hizo za Mwalimu tunazijua shule ambazo ukisoma kila mtu anakukubali na zilikuwa zinajulikana kama shule za vipaji maalumu.Nikianza kwa kuzitaja kulikuwa na shule maalumum kama;TABORA BOYS,TABORA GIRLS,MAZENGO,MOSHI TECHNICAL,TANGA TECHNICAL,IFUNDA TECHNICAL,MTWARA TECHNICAL NA RUVU BOYS. Anayebisha atakuwa ni kati ya wale waliosomo miaka ya hivi karibuni kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea,Kulikuwa hakuna cha Mzumbe wala Ilboru wakati huo.

Habari ndio hiyo. Hawa hajui shule maalumu. Shule ulizotaja ndio zenyewe. Nimesoma Warsaw (Tabora Girls) hapo kuingia ilikuwa ni mwanafunzi msichana wa kwanza kwenye wilaya na Tabora boys ni mvulana wa kwanza kwenye wilaya. Enzi hizo kweli kulikuwa na usawa kwani asilimia kubwa waliosoma shule zote ulizotaja ni vichwa maeneo mengi.
Ukilinganisha na hawa wa Best schools za sasa sijui wanaishia wapi?
 
Tatizo wanaobishania humu ni watoto walisoma miaka ya juzi kuanzia miaka ya elfu mbili.Sisi tuliosoma enzi hizo za Mwalimu tunazijua shule ambazo ukisoma kila mtu anakukubali na zilikuwa zinajulikana kama shule za vipaji maalumu.Nikianza kwa kuzitaja kulikuwa na shule maalumum kama;TABORA BOYS,TABORA GIRLS,MAZENGO,MOSHI TECHNICAL,TANGA TECHNICAL,IFUNDA TECHNICAL,MTWARA TECHNICAL NA RUVU BOYS. Anayebisha atakuwa ni kati ya wale waliosomo miaka ya hivi karibuni kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea,Kulikuwa hakuna cha Mzumbe wala Ilboru wakati huo.

tanga tech
 
True kabisa, enzi hizo ukiwa unasoma Government basi wewe kipanga kweli kweli...private ilikuwa ni kwa wale ambao hawakufaulu. kiufupi ni kwamba yawezekana hukuwa mjinga, bt akili zako hazikutosha kufaulu ukaenda government.
ila mambo sasa tofauti kweli...ukimpeleka mwanao government unaonekana hauko serious na Elimu.
Ilikuwa raha kweli kufaulu kwenda Serikalini enzi hizo.Mademu wote mtaani wanakugombea kila mmoja anaona sifa kuwa na wewe.Na kama ni msichana amefaulu wavulana wote wanamwogopa mtaani ambao hawakufaulu.
 
badoo tu mnaendelea kuaamini kuwa kuna best school!
kwa ulimwengu wa sasa kuna best candidates, ure performance will determine the best
ukiwa na akili kama zawachangiaji waliotangulia utashindwa maisha ,then bado wanaoneka mawazo yao ni ya kitoto sana
kama bado mpo shule someni kwa bidii,kama mshamaliza tafuteni hela kwa bidii zote pamoja na amani moyoni
nawasilisha

Kweli mkuu nakuunga mkono, kwa maoni yangu hizo za serikali naweza kusema sawa maana mwanafunzi akiaanza form one anendelea mpaka mwisho kikubwa awe amefaulu kidato cha pili tofauti na hizo zingine wanakuwa na kiwango chao kingine cha ufaulu tofauti na serikali na kinachofanyika kila mwaka wanachuja mtu akipata below 50 wanamwondoa wanawaacha wale wenye good pass ili mwisho wa siku walinde record ya shule wakati kazi ya shule ni kuwapa maarifa wanafunzi ili waweze kuelewa na sio kubaki na best students ambao uelewa wao siku zote upo juu kama kweli best school kwani hata yule aliepata wastani 48 kwa vigezo vyetu vya elimu amefaulu tena daraja C unapomwondoa maana yake humtendei haki, mie credit kwa hizo shule za serikali kwanza zenyewe ni zoazoa hata kama mtu atapata wastani 26 kwenye mitihani ya muhula wanaendelea nae na mwisho wa siku anajitutumua na shule inaendelea kubaki na record nzuri
 
Tatizo wanaobishania humu ni watoto walisoma miaka ya juzi kuanzia miaka ya elfu mbili.Sisi tuliosoma enzi hizo za Mwalimu tunazijua shule ambazo ukisoma kila mtu anakukubali na zilikuwa zinajulikana kama shule za vipaji maalumu.Nikianza kwa kuzitaja kulikuwa na shule maalumum kama;TABORA BOYS,TABORA GIRLS,MAZENGO,MOSHI TECHNICAL,TANGA TECHNICAL,IFUNDA TECHNICAL,MTWARA TECHNICAL NA RUVU BOYS. Anayebisha atakuwa ni kati ya wale waliosomo miaka ya hivi karibuni kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea,Kulikuwa hakuna cha Mzumbe wala Ilboru wakati huo.

Enzi hizo mtu akiingia shule za government tu tayari ana division 111 kwani shule nyingi division 0 na 4 zilikuwa ni chache sana au hakuna kabisa na ukichaguliwa lazima ufanyiwe sherehe na kusafiri ilikuwa kwa warrant, hapo kwenye list kulikuwa na KIBAHA ilikuwa ni shule ya agriculture
 
Back
Top Bottom