Top 3 GOAT Tanzania Rappers, Serikali itambue mchango wao ikibidi watunukiwe Phd

Top 3 GOAT Tanzania Rappers, Serikali itambue mchango wao ikibidi watunukiwe Phd

Songa ndio nani? Hawa watoto wa 2000 bwana! Hamuwajui kina Solo, Mox, Mo na wengine kibao
 
Mkuu ukimsikiliza Kendrick Lamar unaona amepoa au hajapoa? Hao kina BIG na Jay z wanafanya hiphop zaidi, ila kwenye rap hapana
Hiivi mkuu kwako uelewa wa Rap and Hip Hop ni nini?.

Unajua kuwa Hip Hop ni broader concept?, unafahamu kuwa hip hop ni culture and way of living?.

Unafahamu kuwa Hip Hop haiwakilishwi tu na maneno yatokayo katika mdomo wa anayeimbia, ila inaenda mpaka kwenye vitu kama graffiti, MCing, DJing and breakdancing?
 
nawaheshimu wote kwa mchango wao lakini... sioni goat apo..
 
post yako imenistua ikabidi kwanza nipite Youtube kujiridhisha.

Sijaona ulicho Kiona..

Yaan ata kama hapa Tz nzima wangekua rapper hao watatu tu ulio wataja huwez mweka fid q namba Tatu jamaa angu

fid kawapita mbali Sana kwa Kila kitu na hasa uandishi, hao labda Kwenye free style
 
Mwana FA huyuhuyu aliyeimba bado niponipo, mwanaume suruali, mabinti? Nitajie punchline moja tu kwenye hizo nyimbo! Prof jay nineshazungumza hapo juu, Afande sele hao ni bongo fleva
Punch line inapaswa iweje?..rap ni nini na hip-hop ni nini!?.. usiniambie hip hop ni pana na rap imo ndani yake,define rap from hip hop
 
Hii list bila mfalme Hashim Dogo ambae hata huyo Songa mwenyewe anakiri hilo hapo siwezi kukuelewa kabisa mkuu. Fanya research yako vizuri.
 
Juma Nature? Seriously? Huyo mnamuita rapper? Afande sele a.k.a selemani msindi anaimba lakini sio rapper mwandishi IQ ya kutisha, Sugu ni hiphop lifestyle zaidi,Joseph Haule anaimba Hiphop Lifestyle + promo sio pure rapper, angalau One incredible,na Young killer
Babuu na LANGA nao ni kundi gani?
 
Dizasta huwa namuona kama anatumia nguvu nyingi,ni kama vile mtu yupo chooni anakata gogo ngumu
 
Ngoja nikamsikilize Imam Abbasi mwokozi wa mitaa ya kati
 
Disaster ni hatari mkuu
Huyo Dizasta vina ni mchumba na vimistar vya kuunga unga.... Hapo mkali Fid... Walau huyo Songa yupo vizuri kwenye story telling
. Hebu sikiliza kitu inaitwa kikao na nyingine inaitwa mwanajua
 
Afande sele ndo msanii wangu bora wa muda wote kwenye swala la tungo akifuatiwa na Prof. Jay ....kwa wasanii wa sasa nikiwa na hamu ya kupata chakula cha ubongo namsikiliza Dizasta Vina na nimesikiliza nyimbo zake nyingi mno ila nimejikuta naupenda zaidi wimbo wake unaoitwa MBUZI ,jamaa anajua kuandika na anafikilisha sana kuna baadhi ya nyimbo zake kumuelewa ni mpaka utulize akili.
 
Back
Top Bottom