Top Secret: Nyaraka Namba 12333 kutoka Whitehouse

Top Secret: Nyaraka Namba 12333 kutoka Whitehouse

Status
Not open for further replies.
The bold mkuu shukrani sana kwa makala ya maana. Kuna mtu alishaleta makala juu ya Mossad, leo umeleta ya CIA. Naomba mkuu kama inawezekana tutengenezee na ya Komityet Gasudalstiveniy Bezopostnost (KGB) Natamani niwajue na wao, mission zao afu nifanye comparison kati ya hizi agency tatu Mossad, CIA na KGB.
 
Nimeikubali aiseee!!!!
Niliisoma sana ile ya kuuawa kwa Guevara Bolivia na hata Rodriguz ninazo picha zake ndie aliongoza wale Red Barret ambao ndio walimkata Guevara msituni na ndie mtu wa mwisho kuongea na Guevara kumwambia kuwa imeamuliwa uuawe na kumwambia ampe ukumbe wwte wa kumpelekea Fidel ambapo Gievara alimwambie amwambie Fidel atunze wanangu!!!!
Ni interesting kujua hawa watu jinsi wanavyoendesha mambo yao ya kihuni na kihayawani!!!!!
Halafu Mtanzania anatatanga huko kwao kwenda kumshitaki Jecha na Magufuli. Hawa mabeberu siku zote hawafanyi vitu kwa hasara, wakikukubalia jambo ujue wana lao jambo, wakikupotezea ujue wanakula na wapinzani wako.
 
Sasa kama zamani ilikuwa hivi, je sasa hivi wapo hatua gani mbele?

Haya mataifa UK na USA ni zaidi ya sumu duniani hasa linapokuja swala la maslahi.
 
Mkuu ni SAG walienda Iran wakachagua baadhi ya vijana wa Kiiran na kuwatrain..

Lakini kiongozi wa Operations wa SAG (CIA) aliyekuwepo Iran Bw. Donald Wilber alikuwa na kiasi fulani ana asili ya kiarabu (Wilber alikuwa kiongozi wa mission za kijeshi na Kermit Roosevelt alikuwa kiongozi upande wa Utawala (Senior Officer)). Pia Wilber alikuwa na ujuzi mkubwa wa lugha ya kiarabu na tamaduni zao. Hii ilitokana na ubobezi wake katika masuala ya akiolojia na historia ya kale ya Persia kama nilivyoeleza kwenye makala.

Hata muonekano wa Wilber na uvaaji wake ulikuwa wa kiarabu kabisa. Hii ilimsaidia 'kublend' kiurahisi katika jamii ya Wairan..

Nitapandisha picha yake hapa baada ya dakika kadhaa..
Nimewasikia wa iran sio waabu na waajemi
Au sura zao wanafanana km wachina,wajapan na wakorea nk??
 
Sasa akibuni kitu hiyo itakuwa ni simulizi au fix?

...ugonjwa huu kiasili wanaugua jinsia ya kike hebu jihakiki jinsia yako kwanza wewe ni Semenya?

Unauliza itakuwa simulizi au fix? Kwani simulizi haiwezi kuwa fix?
 
Hongera mkuu wewe ni moja ya watu ampao wanafanya wengine tusiichoke JF.
 
Hizi ndio mada au makala za watu hasa sisi vijana kusoma,kujadili na kutafakari na kisha kuona mbali tuna majukumu gani katika kufikia ndoto walizowaza waasisi wa mataifa yetu ya Afrika baada ya ukombozi wa nchi zao.Ningependa kufatilia mada zako maana kichani huwa namaswali mengi juu ya migogoro ya nchi za kiafrika hususani za kasikazini kwa wale wenzetu wenye asili ya kiarabu na wenye utajiri wa mafuta.Umoja wamataifa kwasasa imebadilishwa badala ya kusimamia usalama,kulinda na kuleta amani wao wamekua watoa misaada kwenye nchi za mapigano?Swala la Syria tumlaumu nani au lipelekwe wapi Marekani au Urusi?Gadafi alikua na shida gani?Hii mikataba ya madini inayotunyonya hatuwezi kuivunja kwa malipo ya kuchukuliwa utumwa mababu zetu.
 
Kabisa Mkuu! Kwa namna fulani pia ni sehemu ya propaganda kuonyesha ulimwengu juu ya "supremacy" ya taifa la Marekani.

Ni sawa sawa na nchi nyingine inavyofanya maonyesho ya silaha nzito, makombora, na teknolojia ya kijeshi.. Ni mkakati wa kutisha maadui..

So kwa sehemu fulani nakubaliana nawe kuwa utoaji/uwekaji wazi wa siri hizi nzito huwa pia una lengo lilijificha..

Lakini pia kwa upande mwingine tufahamu kuwa si suala jepesi kwa CIA kuachia hadharani siri hizi, huwa kesi zinafunguliwa mahakama kuu kudemand hizi files na kesi huunguruma kwa miaka kadhaa mpaka CIA kufikia hatua ya kuachilia hizi files..
Hapo tunakwenda sawa, Chkua Gwara
 
Ndio maana Hayati Mwalimu Nyerere alisema kwamba "nikiona Marekani wanasifia, nitajiuliza kwamba hivi nimekosea wapi?"

Leo ndio nimelewa hayo maneno!
 
Ume claim hati miliki.

Sijui kama unaweza kubeba simulizi la mtu mwingine, James Angleton, la matukio ya zaidi ya miaka 40 iliyopita, yaliyowekwa kwenye public records za national archives na kudai ni ya kwako.

Kwa nini, kwa sababu, awali ya yote, ndani ya simulizi hukuonyesha hukutofautisha kwa citation kipi umebeba cha mwenzio na kipi cha kwako, kama kipo.

Swali: Nini hapo umekibuni wewe, umeongeza ya kwako ya kichwani, kiasi cha kukupa hati miliki ya ubunifu juu ya simulizi hili?

Tuheshimiane, acha mambo ya kipumbavu na kuongelea vitu usivyovifahamu na usilete mazoea ya kijinga mpuuzi wewe..

Hujui hata unachoongea!! Unamuongelea James Angleton?? Mpuuzi kabisa wewe, James Angleton hajawahi kuandika chochote kuhusu Mapinduzi ya Iran na najua hujawahi hata kumsikia na nisingemtaja hapo usingekuja kumsikia..

Unajua kwanini nimeweka quote yake hapo?? Nimeandika hiyo quote kwa kuwa nimeipenda na inashabihiana na nilichotaka kuandika.. Unakuja na kimbele mbele chako unaanza kuongea sijui nimebeba vitu vya Angleton?? Mpuuzi kabisa, wapi umesikia Angleton amewahi kuandika kuhusu Mapinduzi ya Iran.. Angleton mpaka anafariki mwaka 1989 hajawahi kuandika hata kitabu kimoja maisha yake yote na wala hakuwahi kutoa siri yoyote kuhusu CIA..

Nimeweka pale chini source ya makala yangu ni Nyaraka zilizo kabidhiwa George Washington University, wewe unakuja na upuuzi wako unaongea vitu usivyovijua!!

Unaongea kuhusu hati miliki! Hivi unajua hata hati miliki inazingatia nini??? Kisa ni True story ndio isiwe na hati miliki??
Kwahiyo unataka kusema kuwa mtu anaweza kwenda kudurufu kitabu cha mzee Msekwa alichoongelea maisha ya Nyerere na kwenda kuuza kisa tu msekwa kaandika true story ya Nyerere hivyo hana hati miliki??? Mpuuzi kabisa..

Wewe mtoto wa kiume acha wivu wa kipumbavu..

Tuheshimiane.!!
 
Yes Mkuu! Kuna visa vingi sana kuhusu Mugabe na wamagharibi..
Kuna kipande fulani katika series niliona kuhusu mugabe kutaka kupinduliwa lakini hawakufanikiwa! Mkuu ukipata nakala.hata sources tu please naomba unipe links nipitie huko nipate maarifa ya ki ulimwengu na mambo ya intelijensia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom