Top Ten ya majiji tajiri zaidi Afrika 2022, Nairobi namba 5, Dar es Salaam haimo

Top Ten ya majiji tajiri zaidi Afrika 2022, Nairobi namba 5, Dar es Salaam haimo

Hapa kuna vitu vinachanganywa ndio maana kuna jaama kasema wabongo wanachonga sana lakini uelewa wao ni sifuri. List ilioletwa hapo ambayo Dar haipo kwenye top 10 ni ya majiji tajiri barani Africa. Wachangiaji wanashangaa ni vipi Nairobi imeipita Dar.
Kweli kwa majiji tajiri kwa africa lazima tukubali Nairobi ni zaidi ya Dar kwa sababu wameangalia ukwasi wa matajiri wanaoishi kwenye hio miji. Matajiri wengi wa Nairobi ni wasomi na wanaofanya biashara zinazoeleweka na ni kweli wako wengi zaidi kuliko Dar Es Salaam. Matajiri wengi wa bongo ni wa janja janja hivyo hawako kwenye hesabu kama wa miji mingine hio iliopo kwenye top 10. Inshort, Dar ina vitajiri uchwara.
Kwa ukubwa na ukuaji wa jiji kimajengo na idadi ya watu Dar ni zaidi ya Nairobi na imo kwenye top 5 barani Africa. Watu wasichanganye vitu hapa.
Naongezea bongo wengi ni scammer na wanatumia ujanja kutapeli watu wachache Wana biashara zinazoeleweka ..hao wakenya watu wana biashara kubwa na wahudhuria international exhibitions na mikutano ya kibiashara ,hapa bongo mtu akishaleta mzigo kutoka china basi yeye no billionaire karidhika
 
Kwa Mujibu wa Africa Facts zone,Dar inashika namba 11 na haimo kwenye List ya Majiji 10 Tajiri zaidi Afrika..

Source-Africa Wealth Report 2022.

List kamili hii hapa [emoji116]
...Utajiri katika Nini, labda wafanye Hapo kwanza...!!
 
Taratibu Dar inaanza kufufua kwenye real estate 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220923-141709.png
    Screenshot_20220923-141709.png
    134.9 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220923-141738.png
    Screenshot_20220923-141738.png
    42.1 KB · Views: 7
Kwa mtu ambaye hajawahi kufika Nairobi anaweza kubabaishwa sana na hii taarifa. Kiukweli Nairobi ni jiji lililojaa maskini wengi huku idadi kubwa ya wakazi wake wengu wanaishi maisha duni mnoo.

Wakenya ni mafundi wakubwa wa kutengeneza au kukuza taarifa zenye mwelekeo chanya kwao. Na kwa kuwa watanzania wengi ni 'washamba wa taarifa' (hawana exposure tofauti tofauti wala hawataki kupanua wigo wa kuchambua taarifa zinazoletwa machoni pao) ni rahisi mnoo kubebwa na taarifa yoyote.

Kwangu mimi katika ukanda huu wa Afrika mashariki na nchi zote zinazoizunguka Tanzania, hakuna jiji bora kama Dar ikiwa tutapima kwa vigezo vya:
-Miundo mbinu
-huduma muhimu za kijamii.
-muingiliano wa kimaisha
-Ubora wa Makazi na majengo.
-Usafiri wa umma
-Mandhari.

Aliyewahi kusema Bongo sihami ng'o huenda alikuwa sahihi sana. Bongo tamu kwa kila mtu. Sio maskini wala sio tajiri wote wanakula raha.
 
Nairobi ilionekana jiji bora sana kuliko Dar hapo zamani sana. Kuanzia miaka ya tisini kuja sasa Dar imekuwa kwa kasi maradufu ya Nairobi. Mambo ya soko huria (ubepari) yalipoingia Tz yalibadilisha kila kitu katika jiji la Dar. Kuanzia kwenye biashara, usafirishaji, ujenzi na huduma muhimu ghafla mnoo zilibadilika Dar na kuwa bora, rahisi, kisasa na mvuto.
 
Back
Top Bottom