Top Ten ya majiji tajiri zaidi Afrika 2022, Nairobi namba 5, Dar es Salaam haimo

Naongezea bongo wengi ni scammer na wanatumia ujanja kutapeli watu wachache Wana biashara zinazoeleweka ..hao wakenya watu wana biashara kubwa na wahudhuria international exhibitions na mikutano ya kibiashara ,hapa bongo mtu akishaleta mzigo kutoka china basi yeye no billionaire karidhika
 
Kwa Mujibu wa Africa Facts zone,Dar inashika namba 11 na haimo kwenye List ya Majiji 10 Tajiri zaidi Afrika..

Source-Africa Wealth Report 2022.

List kamili hii hapa [emoji116]
...Utajiri katika Nini, labda wafanye Hapo kwanza...!!
 
Taratibu Dar inaanza kufufua kwenye real estate 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220923-141709.png
    134.9 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220923-141738.png
    42.1 KB · Views: 7
Kwa mtu ambaye hajawahi kufika Nairobi anaweza kubabaishwa sana na hii taarifa. Kiukweli Nairobi ni jiji lililojaa maskini wengi huku idadi kubwa ya wakazi wake wengu wanaishi maisha duni mnoo.

Wakenya ni mafundi wakubwa wa kutengeneza au kukuza taarifa zenye mwelekeo chanya kwao. Na kwa kuwa watanzania wengi ni 'washamba wa taarifa' (hawana exposure tofauti tofauti wala hawataki kupanua wigo wa kuchambua taarifa zinazoletwa machoni pao) ni rahisi mnoo kubebwa na taarifa yoyote.

Kwangu mimi katika ukanda huu wa Afrika mashariki na nchi zote zinazoizunguka Tanzania, hakuna jiji bora kama Dar ikiwa tutapima kwa vigezo vya:
-Miundo mbinu
-huduma muhimu za kijamii.
-muingiliano wa kimaisha
-Ubora wa Makazi na majengo.
-Usafiri wa umma
-Mandhari.

Aliyewahi kusema Bongo sihami ng'o huenda alikuwa sahihi sana. Bongo tamu kwa kila mtu. Sio maskini wala sio tajiri wote wanakula raha.
 
Nairobi ilionekana jiji bora sana kuliko Dar hapo zamani sana. Kuanzia miaka ya tisini kuja sasa Dar imekuwa kwa kasi maradufu ya Nairobi. Mambo ya soko huria (ubepari) yalipoingia Tz yalibadilisha kila kitu katika jiji la Dar. Kuanzia kwenye biashara, usafirishaji, ujenzi na huduma muhimu ghafla mnoo zilibadilika Dar na kuwa bora, rahisi, kisasa na mvuto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…