Lipwebwete
Member
- Apr 14, 2021
- 41
- 73
Habari wana jamvi wa JF...
Leo tumeanza maadhimisho ya jubilei ya miaka 100 (1926 - 2026) ya Shule ya Sekondari ya Tosamaganga. Maadhimisho haya yameanza leo tarehe 08/10/2026 na kilele chake ni keshokutwa tarehe 10/10/2026. Aidha mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Mh. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Nchi, Bunge, Sera, Uratibu....
Kama ilivyo kwa shule nyingi kongwe hapa nchini, ambapo viongozi wengi wamekuzwa katika shule hizo, basi, Kabudi naye ni mwanafunzi aliyekuzwa na Tosamaganga Sekondari, yaani ni mwana Alumni wa Tosamaganga.
Naam, ni karne moja ya uhai, ufanisi na ujenzi wa vizazi tofauti vya watanzania.
Kila la heri Tosamaganga, Mungu akulinde na akupe maisha marefu, ili uendelee kuwanufaisha Watanzania wa kizazi hiki na vizazi vingi vijavyo.
Je, wewe ni mwana Tosa? Tia neno moja la kumbukumbu yako ukiwa katika Ardhi ya Tosamaganga wakati wako.
MUHIMU LA KUKUMBUKA
Kuanzia Julai mwaka huu 2026, Shule ya Sekondari ya Tosamaganga imepandishwa hadhi kuwa "SPECIAL SCHOOL" Level moja na kina Mzumbe, Kibaha, Ilboru, na Tabora boys.