Tottenham Hotspurs Thread

Tottenham Hotspurs Thread

Kabisaaaa, sisi tunachotaka ni furaha buana.
Kale kakocha ka Man U hata hakaongei utadhani kila saa kako msibani[emoji847][emoji847][emoji847]
Kweki dunia inakimbia. Kwa mara ya kwanza mashabiki wa United tunajikuta tunaanza shabikia timu nyingine epl. Acha wabaki na timu yao wapuuzi akina Woodwork. Now tuko na fundi Jowzey.
 
Nenda mkuu utupunguzie mashabiki mandazi kwenye timu yetu.
United inaweza shinda au kutoa sare pe OT ila haitamaliza ligi juu ya Spurs. Naipenda sana United ila siwezi shabikia kitu kisichoshindana. Now that Jowzey is back acha niende Spurs kwa mkopo.
 
Nenda mkuu utupunguzie mashabiki mandazi kwenye timu yetu
Shabiki kindakindaki wa Jose Mourinho..alipo naweka kambi, man u hawakua na passion... ni shabiki wa Man u ila Tot ninakua shabiki pia.
 
Nendeni mtupunguzie gundu
Kweki dunia inakimbia. Kwa mara ya kwanza mashabiki wa United tunajikuta tunaanza shabikia timu nyingine epl. Acha wabaki na timu yao wapuuzi akina Woodwork. Now tuko na fundi Jowzey.
 
Taratibu tunajikongoja 3 points away.....
Naona future nzuri japo sikufurahishwa na matokeo ya mchezo haiwezekani jamaa wanapata goli kirahisi vile mpaka nikahisi zingekuwa dakika zimeongezwa 10 wangepata sare
 
Eneo analocheza lucas moura kadri siku zinavyozid kwenda ata-improve kuliko kawaida, majeruh yapite mbali!
 
#COYS

Mko wapi wakuu. Naona kimya sana hapa janvini. Amkeni basi.
 
Hebu tuanze kuimulika hii project ya sasa ya Spurs chini ya mtaalam mwenyewe the special one. Naona re-build inafanyika kimyakimya bila kelele.

Tulianza kwa kusajili creative DM kwa Gedson Fernandes kwa long term loan (kudos). Hapa tumeimarisha idara ya kiungo ukabaji kwa kuleta new version ya Harry Winks. Kwa mnaowafahamu vizuri Rakitic, Veratti, Rabiot, Modric na KDB mnaelewa naongelea nini. Timu imepata pass master ambaye mbali na kuwa DM mzuri pia anaweza cheza kama Kiungo mshambuliaji anapotakiwa. Tuliona kwenye debut yake.

Kisha tukaufanya mkopo wa Giovani Le Celso kuwa biashara ya kudumu. Huyu bwana ni direct replacement ya fundi Eriksen. Ukitazama game mbili zilizopita utakubaliana nami kuwa Jowzey atakuwa na kibarua kigumu cha kumuanzishia benchi Dele Alli kwenye CAM endapo tutapata replacement ya Harry Kane.

Hatukuishia hapo, tumemsajili Steven Bergwijn (tamka Berg-Wine). Huyu bwana kama ilivyo kwa Le Celso na Fernandes ana versatility ya hali ya juu. Yaani anaweza cheza nafasi nyingi tofauti uwanjani. Naturally jamaa ni Left Winger. Ila anaweza cheza nafasi nyingine yoyote ile kwenye final third, yaani RW, CAM na ST.

Hii inafanya timu ikamilike kwenye eneo la ushambuliaji kama ifuatavyo;

LW _ Son/Bergwijn

RW _ Moura/Lamela/Fernandes

CAM _ Le Celso/Dele Alli/ Fernandes/Bergwijn




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maeneo yenye udhaifu kikosi cha Spurs

Kiungo cha ukabaji. Idara hii ili ikamilike yaani iwe na balance, huitaji viungo wakabaji wa aina mbili kwa ratio ya 2:1;

Kwanza, Creative/More Offensive DM. Hapa nazungumzia wachezaji kama Kroos, Modric, Pogba, Rakitic, KDB, Fred, nk. Sisi tayari tunao Ndombele, Fernandes, Sissoko na Winks. Hawa huwa na majukumu ya kutoa/kupokea mipira kwenye eneo la ulinzi na kuhakikisha inawafikia washambuliaji. Ukiacha inconsistency ya Ndombele nadhani tuko vizuri.

Pili, More Defensive DM. Hapa nazungumzia wale viungo wakabaji wanaokaba zaidi ya kushambulia. Watu kama Matic, Kasemiro, Fernandinyo, na sisi tunao Eric Dier na kaka yetu Wanyama. Hapa pana shida. Wanyama ni expendable na ni dhahiri yuko out of form. Dier naye yuko out of form na haeleweki lini ata-step up. Akicheza vizuri game moja, mbili au tatu anaharibu.

Kocha amekuwa akilazimika kuwatumia Winks na Sissoko kitu ambacho hupelekea DM kufa kabisa. Hapa natarajia dirisha lijalo asajiliwe mtu kama Matic/McTominy ili pengo lizibwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom