Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kwa namna nikienda kwenye maduka ninavyoona Wafanyabiashara wanafanya mauzo bila kutoa risiti na Wananchi wananunua bidhaa bila kudai risiti napenda kusisitiza, Mama yangu Samia kazia hapo hapo.
Nchi inahitaji kodi ili huduma za maendeleo ziweze kutolewa na kama wananchi hawako tayari kushiriki kwenye njia za kawaida kabisa katika kuhakikisha wanalipa kodi stahiki ili nchi ipate mapato basi njia hizi zingine kama kuweka kodi kwenye miamala ya kibenki hazina budi kutumika ili tupate mapato
Niliandika uzi humu kwa namna gani Watanzania hawajali suala la kuhakikisha wanalipa kodi ili kuhakikisha nchi yao inapata mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Leo hii mfano mdogo tu mtu kwenye duka ana bidhaa zenye thamani ya milioni zaidi ya 5 au 10 ila hana mashine ya efd, kama anayo mashine basi kaiweka uvunguni imejaa vumbi anauza bidhaa za mamilioni mwezi mzima ila hakuna hata risiti anayotoa.
Kwa wananchi pia, pamoja na matangazo kibao ya TRA kwenye radio na television kuwa wanaponunua wadai risiti ila unamkuta mtu anafanya manunuzi na hajali kama anatakiwa kudai risiti ili nchi ipate mapato kwa shughuli za maendeleo.
Siku ya mwisho wanaishia kuumizwa wafanyakazi kwa kukatwa kwenye mishahara yao kwa sababu wananchi hawataki kutimiza wajibu wao kwenye kulipa kodi
With wangu, Rais wangu Mama Samia usicheke na nyani utavuna mabua, wanataka bima ya afya kwa wote, elimu bure hadi form six, madaraja yajengwe, barabara zijengwe sasa wasipolipa kodi utapata wapi hela za kufanya yote hayo?
Kazia hapo hapo Mama yangu!