Tozo Mpya: Kwa tabia za Watanzania, Rais Samia kazia hapohapo

Kwanza kodi imeanza kulipwa kernel hii? Au mpagani wewe?
Hata enzi za Mkoloni, Wazee wetu hawakulipa kizembe tu yale makodi kandamizi! Na hata Serikali ya Mkoloni ilipotumia nguvu, bado haikufanikiwa kivile.

Sasa kama Mababu na Mabibi zangu walikwepa kodi kutoka kwa Mkoloni mweupe, mimi ni nani mpaka niache kukwepa kodi za aina ile ile kutoka kwa Mkoloni Mweusi?
 
Mr
Kwa namna nikienda kwenye maduka ninavyoona Wafanyabiashara wanafanya mauzo bila kutoa risiti na Wananchi wananunua bidhaa bila kudai risiti napenda kusisitiza, Mama yangu Samia kazia hapo hapo.

Nchi inahitaji kodi ili huduma za maendeleo ziweze kutolewa na kama wananchi hawako tayari kushiriki kwenye njia za kawaida kabisa katika kuhakikisha wanalipa kodi stahiki ili nchi ipate mapato basi njia hizi zingine kama kuweka kodi kwenye miamala ya kibenki hazina budi kutumika ili tupate mapato

Niliandika uzi humu kwa namna gani Watanzania hawajali suala la kuhakikisha wanalipa kodi ili kuhakikisha nchi yao inapata mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Leo hii mfano mdogo tu mtu kwenye duka ana bidhaa zenye thamani ya milioni zaidi ya 5 au 10 ila hana mashine ya efd, kama anayo mashine basi kaiweka uvunguni imejaa vumbi anauza bidhaa za mamilioni mwezi mzima ila hakuna hata risiti anayotoa.

Kwa wananchi pia, pamoja na matangazo kibao ya TRA kwenye radio na television kuwa wanaponunua wadai risiti ila unamkuta mtu anafanya manunuzi na hajali kama anatakiwa kudai risiti ili nchi ipate mapato kwa shughuli za maendeleo.

Siku ya mwisho wanaishia kuumizwa wafanyakazi kwa kukatwa kwenye mishahara yao kwa sababu wananchi hawataki kutimiza wajibu wao kwenye kulipa kodi

With wangu, Rais wangu Mama Samia usicheke na nyani utavuna mabua, wanataka bima ya afya kwa wote, elimu bure hadi form six, madaraja yajengwe, barabara zijengwe sasa wasipolipa kodi utapata wapi hela za kufanya yote hayo?

Kazia hapo hapo Mama yangu!
Wewe utakuwa Mrundi siyo Mtanzania.Tulipe Kodi wanunulie Magari ya kifahari ambayo kila mwaka wanatumia zaidi ya bilioni 500!
Hizo shule za Serikali zenyewe madawati na vitabu mtihani na ukienda hospitalini dawa mtihani alafu anahamasisha watu walipe Kodi kwa lipi!!
 
Kama barabara hazijengwi na kama wanafunzi wanasoma kwa kulipa ada hadi form six basi kweli kodi zinachezewa
Hebu nipe takwimu ni wanafunzi wangapi walishindwa kuendelea na kidato cha 5 kwa sababu ya ada.
 
Huoni zikitumika ipasavyo barabara zinajengwa kwa hela yako? Gharama za ada form five na Six zinafidiwa kwa hela yako? Madeni ya mikopo yanalipwa kwa pesa yako?
Ongea vingine lkn form 5 na 6, kisiwe kichaka cha tozo kama wako serious na elimu watoe mikopo 100% kwa wabafunzi wa vyuo vikuu hapo kweli tutaona tozo zetu zinafanya kazi.Badala yake wanaenda kujilipa maposho makubwa.
 
kwa hiyo kwako form 5 na 6 kusoma bure sio big deal?
 
Hata enzi za Mkoloni, Wazee wetu hawakulipa kizembe tu yale makodi kandamizi! Na hata Serikali ya Mkoloni ilipotumia nguvu, bado haikufanikiwa kivile.

Sasa kama Mababu na Mabibi zangu walikwepa kodi kutoka kwa Mkoloni mweupe, mimi ni nani mpaka niache kukwepa kodi za aina ile ile kutoka kwa Mkoloni Mweusi?
Basi tulia! Utalipa tu
 
Kwa namna nikienda kwenye maduka ninavyoona Wafanyabiashara wanafanya mauzo bila kutoa risiti na Wananchi wananunua bidhaa bila kudai risiti napenda kusisitiza, Mama yangu Samia kazia hapo hapo.

Nchi inahitaji kodi ili huduma za maendeleo ziweze kutolewa na kama wananchi hawako tayari kushiriki kwenye njia za kawaida kabisa katika kuhakikisha wanalipa kodi stahiki ili nchi ipate mapato basi njia hizi zingine kama kuweka kodi kwenye miamala ya kibenki hazina budi kutumika ili tupate mapato

Niliandika uzi humu kwa namna gani Watanzania hawajali suala la kuhakikisha wanalipa kodi ili kuhakikisha nchi yao inapata mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Leo hii mfano mdogo tu mtu kwenye duka ana bidhaa zenye thamani ya milioni zaidi ya 5 au 10 ila hana mashine ya efd, kama anayo mashine basi kaiweka uvunguni imejaa vumbi anauza bidhaa za mamilioni mwezi mzima ila hakuna hata risiti anayotoa.

Kwa wananchi pia, pamoja na matangazo kibao ya TRA kwenye radio na television kuwa wanaponunua wadai risiti ila unamkuta mtu anafanya manunuzi na hajali kama anatakiwa kudai risiti ili nchi ipate mapato kwa shughuli za maendeleo.

Siku ya mwisho wanaishia kuumizwa wafanyakazi kwa kukatwa kwenye mishahara yao kwa sababu wananchi hawataki kutimiza wajibu wao kwenye kulipa kodi

With wangu, Rais wangu Mama Samia usicheke na nyani utavuna mabua, wanataka bima ya afya kwa wote, elimu bure hadi form six, madaraja yajengwe, barabara zijengwe sasa wasipolipa kodi utapata wapi hela za kufanya yote hayo?

Kazia hapo hapo Mama yangu!
Watu tunahitaji maendeleo kwa kasi ya 5G, yaani huduma za maji, barabara etc. Hivi karibuni tumeshuhudia utitiri wa magari Morogoro Road, barabara inahitaji kuongezwa ukubwa hivyo fedha zitatoka kwa wananchi wenyewe...maendeleo hayana chama.
 
Lakini hizo bidhaa za madukani zishalipiwa kodi viwandani , kwenye usafiri na mashambani, unataka ziwe na kodi ipi tena. Tatu Hakuna mtanzania yeyeto asiyelipa kodi. Kodi zipo za aina mbili direct na indirect tax hii utozwa kupitia matumizi ya bidhaa au huduma, thus hata mtoto mchanga analipa kodi si anatumia pampas, nepi, poda, mafuta, uji vyote hivi tayari vishatozwa kodi viwandani ambayo tunailipa kupitia bei ya kununulia.
 
Kwa raslimali zilizopo nchini tele tungepata viongozi wanaofikiri wala wasingekimbizana na mambo ya kukamua kodi watu masikini hata basic needs to mtihani. Kama mkoloni aliweza tuletea maendeleo makubwa Sana nchi pasipo kutegemea kodi sisi tunashindwa vipi.
 
Hao wasimamizi wa kodi zetu je wqnatimiza wajibu wao kwa wananchi? wanasimamia vizuri matumizi ya kodi zetu? Wanachukua hatua dhidi ya wapigaji?
 
Kama barabara hazijengwi na kama wanafunzi wanasoma kwa kulipa ada hadi form six basi kweli kodi zinachezewa
Hizo barabara mnajenga kama sehemu ya kutakatishia kodi zetu, nyingi zipo chini ya kiwango kwa kwa kushirikiana na wachina corrupt
Ili mpate percent, baada ya mda mashimo kibao.
 
Kwa namna nikienda kwenye maduka ninavyoona Wafanyabiashara wanafanya mauzo bila kutoa risiti na Wananchi wananunua bidhaa bila kudai risiti napenda kusisitiza, Mama yangu Samia kazia hapo hapo.

Nchi inahitaji kodi ili huduma za maendeleo ziweze kutolewa na kama wananchi hawako tayari kushiriki kwenye njia za kawaida kabisa katika kuhakikisha wanalipa kodi stahiki ili nchi ipate mapato basi njia hizi zingine kama kuweka kodi kwenye miamala ya kibenki hazina budi kutumika ili tupate mapato

Niliandika uzi humu kwa namna gani Watanzania hawajali suala la kuhakikisha wanalipa kodi ili kuhakikisha nchi yao inapata mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Leo hii mfano mdogo tu mtu kwenye duka ana bidhaa zenye thamani ya milioni zaidi ya 5 au 10 ila hana mashine ya efd, kama anayo mashine basi kaiweka uvunguni imejaa vumbi anauza bidhaa za mamilioni mwezi mzima ila hakuna hata risiti anayotoa.

Kwa wananchi pia, pamoja na matangazo kibao ya TRA kwenye radio na television kuwa wanaponunua wadai risiti ila unamkuta mtu anafanya manunuzi na hajali kama anatakiwa kudai risiti ili nchi ipate mapato kwa shughuli za maendeleo.

Siku ya mwisho wanaishia kuumizwa wafanyakazi kwa kukatwa kwenye mishahara yao kwa sababu wananchi hawataki kutimiza wajibu wao kwenye kulipa kodi

With wangu, Rais wangu Mama Samia usicheke na nyani utavuna mabua, wanataka bima ya afya kwa wote, elimu bure hadi form six, madaraja yajengwe, barabara zijengwe sasa wasipolipa kodi utapata wapi hela za kufanya yote hayo?

Kazia hapo hapo Mama yangu!
Hivi unajua tofauti ya kodi na Tozo??
 
Wakati mwingine mjifunze kukaa kimya bila kuandika takataka.

Hao wafanyabiashara hizo EFD Machines wanazo.?

Serikali yako ndo inawakumbatia. mmeshindwa kupata Kodi huko.
Mmehamia kunyanga'nya wananchi pesa Kwa nguvu.

mnasema magufuli alikuwa anapora pesa watu. Ivi kinachofanyika Sasa ninkitu gani?
 
Unadhani hayo madeni ya hizo hela zinazokopwa yanalipwa na yatalipwa kwa pesa gani wakati hutaki kushiriki vizuri katika kulipa kodi ili nchi ipate mapato?

Ukope wewe na mzigo wa kulipa uwatwishe wananchi, kweli una roho mbaya.
 
Back
Top Bottom