Tozo Mpya: Kwa tabia za Watanzania, Rais Samia kazia hapohapo

Kama mnazifisadi vibaya kodi zetu nasi tutazidi kuzikwepa Ili twende sawa. KILA mmoja atakula kwa urefu wa kamba yake Ili twende sawa
 
Huoni zikitumika ipasavyo barabara zinajengwa kwa hela yako? Gharama za ada form five na Six zinafidiwa kwa hela yako? Madeni ya mikopo yanalipwa kwa pesa yako?

Kwani pesa inatoka wapi?. Serikali haina pesa, pesa zinatoka kwa wananchi punguza dharau.
 
Kwa iyo dawa za mahospitali unanunua wewe, barabara za tarula unajenga wewe kwa pesa yako, madaraja unajenga wewe kwa pesa yako? Madeni ya mikopo ya nje ikiwemo wa ujenzi wa SGR unalipa wewe kwa pesa yako?

Mbona wengine walijenga barabara na maflyover bila kutoza watu tozo za kijinga?. Unakopa kila siku, unalipwa Kodi, misaada na tozo juu.
 
Mbona wengine walijenga barabara na maflyover bila kutoza watu tozo za kijinga?. Unakopa kila siku, unalipwa Kodi, misaada na tozo juu.
walikopa na hayo madeni ndo yanalipwa sasa so lazima kuwe na tozo ili zipatikane hela za kulipa hayo madeni
 
Hizo barabara mnajenga kama sehemu ya kutakatishia kodi zetu, nyingi zipo chini ya kiwango kwa kwa kushirikiana na wachina corrupt
Ili mpate percent, baada ya mda mashimo kibao.
Kwani barabara zote zinazojengwa ni mbovu?
 
Watu tunahitaji maendeleo kwa kasi ya 5G, yaani huduma za maji, barabara etc. Hivi karibuni tumeshuhudia utitiri wa magari Morogoro Road, barabara inahitaji kuongezwa ukubwa hivyo fedha zitatoka kwa wananchi wenyewe...maendeleo hayana chama.
Sahihi kabisa
 
Kwani barabara zote zinazojengwa ni mbovu?
Nyingi zake ndani ya mda mfupi zinafumuliwa,toka lini Mchina akajenga barabara.Kwann mnakwepa kampuni za kizungu jibu ni kwa sababu wazungu awataki rushwa ya michezo ya wanasiasa wao wanajali CV kupitia standard kwa kujenga barabara imara Ili imtangazie market kesho wapate Kazi zingine kimataifa, Mchina anaangalia pesa ya leo. Thus wapo bega kwa bega na tawala corrupt za kiafrica kunufaika kutakatisha kodi za wananchi.
 
Acha porojo, rasilimali tulizonazo bado hazitoshi kumaliza matatizo yetu yote ilhali watu wengi hawalipi kodi.
 
ili mradi zote ni mapato ya serikali. Tafsiri kaa nayo tu
Mh ngoja nikuache...nikusihi sana ogopa sana biashara uliyowekeza kidogo afu ukapata pakubwa kuliko uwekezaji wake..siku ukipata hasara jua tuu utapoteza faida uliyoipata na mtaji wote ulio wekeza...kila la kheri.
 
Acha porojo, rasilimali tulizonazo bado hazitoshi kumaliza matatizo yetu yote ilhali watu wengi hawalipi kodi.
Unajua thamani halisi ya raslimali mfano zilizopo wilaya moja tu zinatosha kufuta kabisa deni la taifa kama zote zikitumika ipasavyo.
Tatizo sio ukosefu wa ajira tatizo ni upofu wa kuziona fursa sababu ya mifumo yetu mibovu ya elimu na malezi.Mbona wageni wao wanakuja nchini masikini na wanatajirika.
Unajua uchumi wa Thailand, Sri lanka, India unajengwa na madini yetu plus mazao yetu mfano korosho, mbaazi, nk. Wao wanachukua malighafi zetu wanaziprocess kisha wanaenda uza Ulaya wanapiga pesa mara nne. SAsa kwann sisi wenyewe tusiprocess na kuuza direct ulaya kwa standard watakayo ulaya, na sio raslimali zetu ziende kwanza Asia au China kisha ndo ziende Ulaya.
Kama watu wengi awalipi kodi maana yake awazalishi, wajengee uwezo wa kuziona fursa Ili wazalishe kisha ndo udai kodi. Unadai kodi kwa maiti.
 
Naunga mkono hoja,huwezi kuwa na jamii ya walalamishi was kila kitu,wanalaumu kila kitu,wanalialia Kwa kila kitu..

Hakuna mjomba was kutuletea Maendeleo na Wala Maendeleo hayaji kwa lelemama..

Naunga mkono Hoja,kazia hapo hapo hakuna kurudi nyuma na atakayeleta fyoto fyekelea mbali,Maslahi ya umma walio wengi ni muhimu kuliko vilio vya individuals.
 
Hii sio sababu, serikali inaweza kutumia njia nzuri tu kutatua tatizo
 
Huoni zikitumika ipasavyo barabara zinajengwa kwa hela yako? Gharama za ada form five na Six zinafidiwa kwa hela yako? Madeni ya mikopo yanalipwa kwa pesa yako?
kufuta ada form six ni wazo la kijinga,,na lisiloweza kuboresha elimu kama mazingira ya walimu hayajaboreshwa,,jambo la msingi ilikuwa ni kutafuta wanafunzi ambao hawawezi kuendelea na masomo ya kidato cha sita kwa kukosa ada na mahitaji mengine,,
Hivyo wangelipiwa ada na mahitaji mengine,,,wale watoto ambao wazazi wao wanajiweza wangeendelea kujilipia ada.

Hiyo tsh 70 elfu kwa mwaka ingesaidia kuboresha miundombinu ya shule pamoja na sekta ya afya,,au hata kuzipeleka kwenye kilimo zingeleta tija.

Unafuta ada wakati kuna shule hazina madarasa ya kutosha,,kuna shule watoto wanakaa chini kwa kukosa madawati,,unafuta ada kuna watoto tena wakike wanatembea umbali mrefu kufuata shule hivo kupelekea njiani kurubuniwa na bodaboda ,,kwanini tusijenge mabweni kwenye shule kadhaa ili watoto hasa wa kike wakae bwenini,,,

Hii ni kutafuta tu cheap popularity kwa wajinga ili uwe mtaji wakura 2025,,kuna ya msingi zaidi ya kuyafanya ili kuboresha elimu kabla ya kufuta ada,,
kuna wakati shule zinakosa karatasi mpaka chaki kutokana na ruzuku kiduchu ,,halafu mtu anasimamia anashingilia kufutwa ada kidato cha sita bila kujua shule zina changamoto zipi za msingi.
 
Ukitaka kufa na presha basi lazimisha wananchi wafuate kama unavyotaka wewe, wnanchi na TRA ni sawa na paka na panya hakuna siku utawaelimisha wananchi kuhusu TRA wakusikie😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…